NA HAJI NASSOR, PEMBA:::
MTOTO wa miaka 16, ambae awali
aliliambia Jeshi la Polisi kuwa, amebakwa na daktari Is-haka Rashid Hadid, na
kisha kumkana mahakamani na kuondolewa kwa kesi hiyo, sasa mtoto huyo, anashikiliwa
na Jeshi hilo, kwa kutoa taarifa za uongo.
KESI HII ILIANZIA WAPI?
Itakumbukwa
kuwa, mtoto huyo miezi mitatu iliyopita, ndie aliyeliambia Jeshi la Polisi mkoa
wa kaskazini Pemba, kuwa ni daktari huyo pekee, ndie aliyemtorosha na kisha
kumbaka zaidi ya mara moja.
Baada ya
maelezo ya mtoto huyo, ndipo Jeshi la Polisi lilipojitayarisha kirasilimali na
kumfuata daktari huyo kijijini kwao Kangagani wilaya ya Wete, na kumkamata na
kuanza kumuhoji.
Baada ya
kuhojiwa juu ya tuhma zinazomkabili, kisha daktari huyo, kuanzia Mei 18, mwaka
huu alipandishwa Mahakamani na kuswekwa rumande, hadi Mahakama ya mkoa Wete
ilipomuondoshea shataka dhidi yake juzi Julai 13, mwaka 2022.
Ambapo Hakimu
wa mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji mkoani humo, Ali Abdur-haman Ali,
alisema sababu ya kumuondoshea kesi hiyo daktari huyo, ni muathirika (mtoto) wa tukio hilo, kumkana
mtuhumiwa.
Alisema kila
mtoto anapoulizwa juu ya kumfahamu mtuhumiwa aliyemtaja akiwa Polisi, alikana
zaidi ya mara tatu, na ndio sababu ya kuondoshwa kwa kesi hiyo mahakamani hapo.
JESHI LA POLISI KWA SASA
Hapo ndipo
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi ambae pia ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya
jinai mkoani humo, Gerome Felix Ngoi, alipoamua kumshikilia mtoto huyo.
Alieleza
kuwa, kwa sasa wanaendelea kumuhoji juu ya kutoa kwake taarifa za uongo kwa Jeshi
la Polisi, na kusababisha usumbufu kwa daktari huyo.
‘’Ni kweli
baada ya kesi ya ubakaji, iliyokuwa ikimuhusisha daktari Is-haka Rashid Hadid
kuondolewa, kwa sababu ya mtoto kumkana, sasa tunamshikilia kwa tuhuma za kulidanganya
Jeshi la Polisi,’’alieleza.
Aidha alieleza
kuwa, tayari jalada lenye namba ‘IR 367’ ya mwaka 2022 limeshafunguliwa na
Jeshi la Polisi la mtoto huyo na upelelezi utakapomilika atafikishwa
mahakamani.
Hata hivyo,
amewataka wananchi mkoani humo, kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na
vyombo vyengine vya sheria, ili kukomesha matendo hayo.
KESI ILIPOKUA MAHAKAMANI
Ilidaiwa mahakamani kuwa, mtuhumiwa
Is-haka Rashid Hadid April 21 mwaka huu, majira ya saa 8:30 mchana, alimtorosha
mtoto mwenye miaka 16, kutoka nyumbani kwao, na kumpeleka nyumbani kwake
Kagangani.
Kufanya hivyo ni kosa kinyume na
kifungu cha 113 (1) (a) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya
Zanzibar.
Kosa la pili kwa mtuhumiwa huyo lilikuwa
ni baada ya kumtorosha, siku hiyo hiyo majira ya saa 3:00 usiku alimbaka,
kinyume na kifungu cha 108 (1), (2), (e) na 109 (1) cha sheria ya Adhabu
nambari 6 ya mwaka 2018.
Ambapo pia kufanya hivyo, ni kinyume
na kifungu cha 108 (1), (2), (e) na 109 (1) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya
mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.
KESI ZINAZOFANANA NA HIZI
Tukio
linalofafana hilo, liliwahi kutokea Novemba 21, mwaka 2019, katika hospitali ya
Chake chake, baada ya daktari wa kitengo cha Atrasaund, kudaiwa kuomba rushwa
ya ngono kwa mjamzito, kama sharti la kumpa huduma. Ambapo kesi hii nayo
ilifutwa Januari mwaka 2021.
Aidha
Kesi nyingine ya ubakaji ni ya mwaka huu, ya daktari Hassan Said Hassan ambayo ilifunguliwa
mahakamani Disemba 16, mwaka jana na kisha baada ya mtoto kumkana mahakamani
ilifutwa JUuni 29, mwaka huu, kwenye mahakama ya mkoa Chake chake.
Aidha
Disemba 18, mwaka mwaka 2019, TBC 1, iliripoti Afisa Muuguzi Msaidizi wa kituo
cha Afya Mamba mkoani Katavi kushikiliwa na Jeshi la Polisi, kwa tuhuma za
kumbaka mjamzito, wakati alipokuwa akimsaidia kujifungua.
Mwisho
Comments
Post a Comment