NA MARYAM SALUM, PEMBA
“SHIDA, dhiki na maneno makali niliyoyapata wakati
naishi kwa mjomba wangu, ndio chanzo cha kuamua kujiajiri,’’ndio maneno ya
kwanza ya mjasiriamali Noela Alfred Majia mmiliki wa saluni ya Crassiana hair salun liyopo Gereji Wawi-
Chake chake.
Hapa ndio msemo
‘mtegemea cha ndugu hufa maskini’ ulipotafsirika kwa vitendo kwa mjasiriamali
huyo mzaliwa wa Dar-es Salaam na sasa mkaazi wa Wawi Chake chake Pemba.
HISTORIA YAKE
Alikuwa
anaishi na mama yake mzazi na mjomba wake, akimtegemea kwa kila kitu kwa wakati
huo, huku mama yake akiwa na uwezo mdogo wa kuendesha familia.
Noela
alijihisi mtoto wa maana sana mbele ya mjomba wake, na aliamini anaweza kuwa
mwanga wa maisha yake, hasa kwa vile ni mjomba anayetokana na mama yake mzazi.
‘’Kwa hakika
tamaa ya kukaa na mjomba na kisha kuwa na maisha mazuri hapo baadae,
nilifikiria sana, na sikutarajia kuwa iko siku mjomba engegeuka adui wa maisha
yangu,’’anasema.
Wakati Noela
akiwa na miaka 17 alishamaliza darasa la kumi, siku moja alichokipata kutoka
kwa mjomba wake, juu ya kauli kali na chafuzu bila ya kujali umari wake.
‘’Toka hapa
kwangu, ondoka haraka sana, wewe mtu gani tafuta pahala uende, mimi sikutaki
kukuona hapa kwangu,’’ndio maneno anayoyakumbuka Noela kutoka kwa mjambo wake.
Huku
akitakiwa kuhama na mjomba wake, naye sasa baada ya kuona hilo limesimama,
alianza kubuni na kufikiria namna ya kutokana hapo na kuelekea eneo jengine
kujiendesha kimaisha.
“Kutokana na hali ilivyokuwa sikujali udogo
wangu wala umri wangu, nilikimbia na hapo nikaona bora nifanye uamuzi wa haraka
kama msichana yakutafuta njia yakupata maisha kabla familia yangu haijagombana
kwa ajili yangu,” anaeleza.
BAADA YA KUTIMULIWA NA MJOMBA WAKE
Noela
aliwasili kisiwani Pemba mwaka 2015, akiwa hana uhakika wa kula, kulala lakini
nia yake ni kupata kazi ambayo itamuwezesha kusonga mbele kimaisha.
“Mimi ni msichana
ambaye nilikuwa naishi na mama na mjomba, lakini baada tu ya kumaliza masomo yangu
mjombo alinikaripia na kuamua kufika Pemba kutafuta kazi,’’anasema.
Baada ya
kutua Pemba, alishikwa mkono na kijana mmoja, na kumpeleka kufanyakazi za
ndani, eneo la Machomane Chake chake, ingawa hakudumu.
‘’Sikudumu
maana, haikua lengo langu hasa kuendelea kufanya kazi za ndani, nilipopata
shida yangu ya shilingi 700,000 kama miezi minne niliacha kufanya,’’anasema.
UANZISHWAJI WA SALUNI YAKE
Shilingi 700,000
alipozipata zilimtosha kuanzisha ujasiriamali wa kuzipakasa nywele za wanawake
wenzake na kuwatia urembo mwengine kichwani.
Noela
anasema licha ya changamoto alizozipata ikiwa ni pamoja na kutokuwa na sehemu
rasmi ya malazi, lakini kisha alifanikiwa kupata malengo wa kukodia kuanzisha
saluni.
Alisema kuwa
mtaji wake wa kusuka nakuwa mmiliki wa saluni umemfanya kuwa mwanamke anayeweza kutafuta
maisha popote katika nchi yake bila woga.
“Kazi yangu
ya mkono inanifanya nijiamini na kuaminiwa na kila mtu kwa chochote ambacho
nitahitaji bila ya kubugudhiwa,” alieleza.
AINAYA MITINDO YA NYWELE
Kwenye
saluni yake, Noela anasema ipo zaidi ya mitindo saba, anayoweza kuwasuka wateja
wake, na hivyo hivyo inatofautiana bei.
‘’Kwa mfano
msuko aina ya roketi, minyoosho, mbinjuo na machana ya ndizi haya yote
huwahudumia wateja wake kwa shilingi 2000,’’anasema.
Lakini
anayomitindo kama ya yebo yebo kwa gharama ya shilingi 16,000 matubutu ya uzi
ni shilingi 20,000, crochet kwa gharama ya shilingi 10,000 na mabutu ya rasta
ni shilingi 30,000 na mtindo , kubiip ni shilingi 15000.
FAIDA YA SALUNI
Kwake
anasema kuaminiwa na wenzake, sio jambo katika maisha hasa ya siku hizi
yaliojaa watu matapeli na wengine wakishindwa kujiamini wenyewe.
Jengine
analoona kama faida kubwa kwake ni kujiamini kukopa, kuazima fedha kwa kiwango
chake anachokihitaji, jambo ambalo kabla yam waka 2015 hilo hakuwa na uwezo
nalo.
“Sasa hivi
naweza kujikwamua kimaisha kutokana na changamoto mbali mbali zinazonikabili
mimi na familia yangu bila kumtegemea mume au mtu mwengine”, alieleza.
Kutokana na
saluni yake kuwa ni ya kwaida, siku ambayo wateja wamekwenda wengine hujipatia
kati ya shilingi 40,000 hadi shilingi 50,000 ingawa kwa siku za uhafifu
huingiza shilingi kati ya 25,000 hadi shilingi 30,000.
Hata
kuongeza mtaji wa shilingi 700,000 aliaonza nao na sasa kujimilikisha mtaji wa
shilingi milioni 1, kwake sio jambo dogo.
CHANGAMOTO
Moja baadhi
ya bidhaa za rasta, wigi na dawa za kulainisha nywele au kupaka usoni
humalizimu kuzifuata Dar-es-Salaam, kutokana wafanyabiashara wa kisiwani Pemba
kutochukua bidhaa hizo.
Kuhusu wateja, anasema hutegemeana na mwezi au
siku, maana suala la urembo pia huendana na siku au mwaka mwenye shughuli
maalum.
‘’Hutegemeana
kwa mfano mwisho wa mwezi hupata wateja kati ya 10 hadi 15, ingawa kwa siku za
kawaida huwa ni katia ya watano hadi sita,’’anasema.
“Namshukuru mwenza wangu mashirikiano kwenye kazi yangu wananipa mazuri, hunipa maneno
mazuri, ili nisikate tamaa kutokana na ugumu uliopo kwenye kazi yangu,” anafahamisha.
ULIPAJI
KODI
Anasema
mazingira yaliwekwa kwao wajasiriamali wadogo, juu ya ulipaji kodi kwa biashara
yake, anaufurahia mno na kumpongeza rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi.
‘’Kodi yangu
hapa kwa udogo wa biashara yangu nalipa shilingi 50,000 serikali, ambapo hii ni
wastani maana sasa Pemba imevamiwa na milango ya saluni,’’anasema.
OMBI LAKE
Anasema kama
kuna mashirika, makampuni na tasisi za serikali ni vyema zikamuangalia, kwa
kumpa mikopo yenye masharti nafuu ili kukuza biashara yake.
Kwake anaona
mikopo wakati mwengine humpitia upande, kutokana na kuwa na masharti makubwa,
na kumuacha akiwa mnyonge kwenye eneo hilo.
MALENGO YAKE YA BAADAE
Noela ambaye
kwa sasa yumo kwenye ndoa kwa muda zaidi ya mika mine, hajabahatika mtoto,
ingawa malengo yake ni kuongeza ujuzi wa aina nyingine ya mitindo ya nywele.
Jengine anasema
ni kuwasaidia wanawake wenzake vijana, kupata ajira na hilo litawezekana ikiwa,
dhamiri yake ya kuomba mikopo yenye masharti nafuu atafanikiwa
WATEJA WA NOELA
‘’Sipendi
kutaja jina langu, lakini kwa hakika huduma za Noela za ususi wa nywele na
uwekaji dawa na urembo mwengine, yuko vizuri mno na sihami kwake,’’anasema.
Hata
mwengine aliyakataa kutoa jina lake, anasema Saluni ya Noela kwanza inautulivu
na kisha huduma zake sio ghali kama wengine, lakini kubwa zaidi ameonesha
kubobea.
Mwamtatu Hilmin
Yassiri anasema Noela ana sifa za kipekee kwenye kazi yake, ambazo hajawahi
kuzipata kwenye saluni nyingine alizowahi kupata huduma.
ALIKOTOKA NOLEA KIELIMU/MAISHA
Noela
alipata elimu yake ya msingi katika Skuli ya Mchangani Dares-Salaam, na baada
ya kumaliza, aliendelea na elimu ya sekondari
mwaka 2012 skuli ya Makumbusho,’’anasema.
Kazi hiyo ya saluni (ususi wa nywele), alianza
kuipenda tokea akiwa darasa la nne, kwa
vile ndani alimokuwa anaishi walikuwemo na wadada wakisuka na kupamba maharusi.
“Hivyo
kutokana na ufahamu wangu niliokuwa nao na jinsi nilivyokuwa napenda hivyo
vitu, sikuwa tayari kujiweka nyuma kama mfuko wa suruali, na leo najivunia nipo
na changu,’’anasema.
MWISHO.
Comments
Post a Comment