NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WATU
wawili wamefariki dunia, baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba mawe, shehia
ya Mjini Wingwi wilaya ya Micheweni Pemba.
Taarifa za
mashuhuda zinaeleza kuwa, jana majira ya saa1:30 asubuhi watu hao, waliondoka
nyumbani kwao na kwenda eneo hilo, kwa ajili ya kutafua mawe kama ilivyo
kawaida yao.
Mashuhuda
hao, wakizungumza na waandishi wa habari, walisema wakati wapatwa na ajali hiyo
wakiendelea kuchokoa mawe hayo, juu yao kulikuwa na mlima mkubwa wa kifusi.
Mmoja wa manusura
wa tukio hilo, Said Hamad Shoka, alisema wakati wanakata jiwe kubwa, juu yao
kulikua na mapande ya kifusi, na kisha kuwafunika.
‘’Ni kweli kifusi
ndicho kilichowafunika, wakati wao wakiwa chini wanachoko mawe, kwa ajili ya
kokoto,’’alisema.
Nae manusura
Khatib Juma, alisema kama sio nguvu za Muumba kuwapa pumzi za kukimbiwa wakati
kifusi kinaporomoka, idadi ya waliokufa yenge ongezeka.
‘’Wakati
kifusi kinaporoka kilikuwa mbele yangu, nilitoka mbio nyingi sana, na wenzangu
wao hawakuwahi na kufariki dunia,’’alisema.
Shuhuda
Abdalla Omar Ali, alisema baada ya kufunikwa, walipiga kelele na kuomba msaada
kwa wenzao waliokuwa karibu yao.
Alieleza
kuwa, wapo wingine waliowahi kupiga simu, kwa vikosi vya uokoaji, ingawa hata
walipofika majira ya saa 3:15 walishafariki watu hao.
‘’Tulipiga
kelele kwamba, wenzetu wanakufaa, wameelewa na kifusi, ingawa watu
walikusanyika na kuopoa wakiwa wameshafariki dunia, kwa msaada wa mashine,’’alifafanua.
Kufuatia
ajali hiyo, Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, na mkuu wa
wilaya ya Micheweni Khatib Juma Mjaja, walifika hospitali ya Micheweni na kuonana
na wafiwa.
Mkuu wa mkoa,
aliwapa pole wafiwa wa ajali hiyo, na kuwataka ndugu na jamaa wawe na moyo wa subra,
katika kipindi hichi kigumu cha msiba.
‘’Kama
wengejua kuwa leo ‘jana’ ndio kifo chao, wala wasingalikwenda kutafuta riziki,
lakini haya ni maandiko ya Muumba mwenyewe, haya makosa,’’alisema.
Mkuu wa
wilaya ya Micheweni Khatib Juma Mjaja, alisema serikali ya wilaya, imezipokea
taarifa hizo kwa huzuni na masikitiko makubwa.
Hata hivyo
alisema, serikali ya wilaya kwanza imepiga marufuku uchimbaji mawe eneo hilo,
hadi hapo itakapoangaliwa njia mbadala, ya wananchi hao kujipatia mahitaji yao.
Waliofariki
katika ajali hiyo ni Hamad Juma Makame na Shaame Hamad Shoka, wakaazi wa
Micheweni, ambapo mwezi Januari mwaka huu, mtu mmoja nae aliripotiwa kufariki
dunia, katika eneo hilo hilo baada ya kuanguliwa na jiwe wakati akichimba mawe.
Mwisho
Comments
Post a Comment