NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
ALIYEKUWA
Mbunge wa Jimbo la Pandani kwa tiketi ya Chama cha wananchi ‘CUF’ Maryam Omar
Said, amsema kuaniza Juni 29, mwaka huu ametangaaza, kujiengua kwenye chama
hicho na kujiunga na CCM, akidai amevutiwa na utekelezaji wa Ilani ya chama
hicho, kwa miaka mitano iliyopita.
Alisema,
ameamua kurudi nyumbani, baada ya kuona yale yote aliyota ndani ya jimbo lake
la Pandani, yamekelezwa ikiwemo miradi ya elimu, afya na maji safi na salama kwa
miaka mitano iliyopita.
Akizungumza na
waandishi wa habari kisiwani Pemba alisema, hana sababu ya kubakia ndani ya CUF,
na ameamua kuhamia CCM, ili kuungana na Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Alieleza kuwa,
akiwa ndani ya CUF, hatakuwa na nafasi nzuri ya kushika bango la CCM na ndio
maana, ameamua kwa hiari yake na bila ya kulazimishwa, kurudi ndani ya chama
hicho.
Mbunge huyo
mstaafu wa CUF, alisema awali alikuwa mwana CCM, ingawa alitoka na kwenda CUF
na sasa amevutiwa mno na utendaji kazi wa viongozi wakuu.
Akizungumzia
azma ya kurudi CCM, alisema ana hamu ya kuomba nafasi nyingine, na kama akipata
ridhaa atafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wa Pandani, wanapata maendeleo.
Mapema Mwenyekiti
wa wilaya ya Micheweni kupitia CUF Mbwana Haji Mbwana, alisema walishamtambua
zamani kuwa, Mbunge huyo, kwamba anaunga mkono utawala.
Alieleza kuwa,
hawakutetereka sana kutoka kwa mwanachama wao huyo na kuhamia CCM, kwani CUF sio
mtu bali ni taasisi inayojitegemea.
‘’Taarifa za
yeye kujiuzulu kwetu hakuwa mpya, maana kwenye bunge kauli zake hazikuwa za
Mbunge mpinzani, bali kama vile za mwanachama wa chama tawala,’’alisema.
Aidha
Mwenyekiti huyo wa CUF alisema, wataendelea kupambana na kupambania haki za wananchi,
wakiwa ndani ya chama hicho, kama ilivyo katiba yao.
Mbunge huyo aliyejiuzulu,
awali alikuwa mwanaccm na kujiunga na CUF na kuwachaguliwa kuwa mbunge peeke
kwa majimbo 18 ya Pemba, na kuanzia Juni 29, mwaka huu amerejea CCM, wakati huu
uchukuaji wa fomu ukiendelea.
MWISHO
Comments
Post a Comment