NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@
MKURUGENZI Rasilimali watu utawala na mipango wa Tume ya Utangazaji
Zanzibar ‘TUZ’ Zainab Sheha Khamis amesema, kushirikishwa kwa wadau mbali mbali
katika kuchangia kanuni ya maudhui na udhibiti wa vituo vya utangazaji,
kutasaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa na tume hiyo.
Aliyasema katika mkutano wa mafisa wa Jeshi la Polisi wa
kitengo cha kupambana na uhalifu wa mtandaoni, kuhusu udhibiti wa maudhui kwa
vituo vya utangazaji, kuelekea uchaguzi mkuu 2025 uliyofanyika ukumbi wa
mikutano ZBC Mkoroshoni Chake Chake Pemba.
Alieleza kuwa, kwa kushirikiana na wadau hao kutasaidia
kufikia malengo husika, ya kupambana na uhalifu wa kimitandao, kuhusu maudhui
kwa vituo vya utangazaji, ili kuepusha migogoro inayoweza kutokezea.
"Tumeona wadau hawa ni muhimu, katika kushirikiana nao
kwani wao ni sehemu moja wapo ya kuhakikisha wanadhibiti maudhui yaliyokua siyo
na kupambana na uhalifu katika mitandao,"alifafanua.
Hivyo, aliviomba vyombo hivyo, kufanyakazi kwa karibu ya ‘TUZ’,
ili kuona kila mmoja anaishi kwa amani na utulivu bila ya kuchafuliwa
mtandaoni.
Mjumbe wa bodi ya tume hiyo Khamis Dadi Khamis, akizungumza kwa niaba ya Afisa Mdhamini wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, alieleza kuwa, mkutano huo wa siku tatu, una lengo la kuskiliza mapendekezo na ushauri ili kuyafanyia kazi na kuandaa kanuni zitakazowawezesha kubaki salama.
Alifahamisha kuwa, TUZ inakuwa na wadau wake mbali mbali, na
haiwezi kutengeneza sheria wala kanuni pasi na kuwashirikisha kwa njia moja ama
nyingine.
Akiwasilisha maelezo mafupi Mrajis, Tume hiyo Ali Hussein Ayoub alieleza kuwa, tume ina kila sababu ya kuhakikisha inatimiza majukumu yake, ikiwemo kusimamia na kulinda sera, usalama mila utamaduni wa mzanzibari.
Alifafanua kuwa, jukumu jingine ni kukagua vituo ya
utangazaji, kutoa leseni, kuvismamia na maadili ya utangazaji.
"Tume kwa sasa ipo katika mapitio ya sera ya
ugangazaji, kanuni ya maudhui ya utangazaji, kanuni za kuriporti habari wakati
wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025,"alieleza.
Afisa sheria kutoka tume hiyo Khadija Mbarouk Hassan
alieleza kuwa sheria za tume ya utangazaji katika kusimamia vituo vya habari na
maudhui, ambayo yanatayarishwa na watangazaji, ili kuzuiya na kupambana na uhalifu
wa mitandaoni unaoweza kujitokeza.
MWISHO.
Comments
Post a Comment