MRATIB wa mradi wa
uwezeshaji na upatikanaji wa haki, Rashid Mshamata, kutoka Jumiya ya wasaidizi
wa sheria wilaya ya Wete ‘WEPO’ amesema bado jamii, ina muamko mdogo katika vita
vya ukatili na udhalilishaji.
Alieleza hayo kwa
wanafunzi na walimu wa skuli na madarsa, za Wete ukumbi wa skuli ya Chasasa,
ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kupiga udhalilishaji katika jamii.
Alisema jamii bado
ina mila na desturi kandamizi ambazo zinawafanya wasichana na wanawake waishi
kwa hofu, na kukosa usawa na haki zao stahiki, jambo linalowapa mwenye wa
kufanya maovu.
‘’Kupitia kampeni
hii, tunawaleta vijana kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ukatili
wa kijinsia, ambapo tunawafundisha sio tu kujitambua, bali kushiriki katika
kulinda haki za wenzao na kuripoti vitendo,"alieleza.
Mshamata alifafanua
kuwa, mafanikio ya kampeni hizo skuli na madrassa, inadhihirisha kwamba vijana
wakiwa na maarifa sahihi, wanaweza kuwa chachu ya mabadiliko ya kijamii.
Alisisitiza kuwa masomoni, ni sehemu muhimu ya
kujenga jamii inayojua haki zake, hasa ikizingatiwa kuwa, vijana ndio kundi
kubwa katika jamii.
Naye Msaidizi wa
sheria kutoka jumuiya hiyo Siti Faki Ali, akielezea maana, aina, sababu, mazingira
na athari za udhalilishaji, ni muhali, kupuuza elimu ya dini, kutumikishwa
kinyume na umri wake.
Aleleza kuwa, jingine
ni uwepo wa ajira za utotoni, kukosheshwa haki za msingi kama elimu pia na
miongoni mwa athari.
‘’Jamii ni vyema kushirikiana na wadau mbali
mbali wa kupinga udhalilishaji, na kua tayari yanapotokezea matendo hayo kwa
kuyaripoti na kuyatolea ushadi, ili lengo liweze kufikiwa katika jamii na taifa
kwa ujumla,’’alifafanua.
Mapema Mwalimu wa madrasa
kutoka Wingwi Sharif Bakar Ali, alifafanua kuwa, wazazi walio wingi wapo nyuma,
katika suala la malezi yenye maadili kwa watoto wao.
"Ni wajibu wa
kila mzazi, kulea katika misingi ya kidini, ili kuepusha vishawishi vinazoweza
kuepukika, licha ya umaskini uliopo, isiwe sababu kujitumbukiza kwenye maovu,’’alifafanua.
Nao wanafunzi walio
shiriki katika mafunzo hayo, wameahidi kuyafanyia kazi kwa kuaanda makundi
maalum, ambayo yatasaidia katika kuhamashisha elimu ya kupinga udhalilishaji.
Mradi huo wa upatikanaji
haki, ‘legal empowerment and access to justice’ unaotekelezwa na
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa ushirikiano na Jumuiya ya
Wasaidizi wa sheria Wete (WEPO), wenye kauli mbiu ‘kupambana na
udhalilishaji unaanza mimi na wewe’.
MWISHO.
Comments
Post a Comment