NA BAKAR KHAMIS, PEMBA@@@@
Waumini wa dini ya kiislamu,wametakiwa kuazimisha mwaka mpya kwa kulinganisha na historia ya uislamu.
Hayo yameelezwa na imamu mkuu wa msikiti wa ng'ambwa wilaya ya chake chake mkoa wa kusini pemba sheikh Abdallah said mara baada ya khutba ya ijumaa
Amesema waumini wa kweli hawana budi kujitathmini katika kipindi cha mwaka uliopita iwapo kuna mema waliyoyafanya waendeleze na mabaya wajikataze
"Kwa kweli hatuna budi kujitathmini katika kipindi cha mwaka uliopita wa 1446 kama kuna mema tuliyokua tukiyafanya tujitahidi kuyaendeleza na kuzidisha katika mwaka huu wa 1447 hijria kama shukran zetu kwa mola wetu"
"Na pia maovu yote ya siri na ya dhahiri tujitahidi kuyaepuka ili tupate neema na salama".
Kwa upande wake khatibu wa zamu Zahor Yahya Muhdhari, amesema maadhimisho mema ya mwaka mpya ni kusimamia malezi ya watoto na usimamizi wa familia.
"Hakika watoto na wake zetu ni mtihani mkubwa kama ambavyo Allah s.w amesema kwa hivyo tujikite katika kuazimisha mwaka mpya kwa kuwalea na kuwatunza wake zetu na watoto ili tupate mafanikio ya dunia na akhera".
Nao waumini waliohudhuria swala mskitini hapo wamesema wameyaelewa waliyoyapata kwa wawili hao na watayafanyia kazi kwa jitahada na malengo.
MWISHO
Comments
Post a Comment