NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
TUME ya Utangaazaji Zanzibar ‘TUZ’, imewataka wasimamizi na wamiliki wa vituo
vya redio nchini, kukubali kubadilika kwa haraka, na kutoka mfumo wa sasa wa
kidijitali na kuacha mafumo wa zamani wa analogia, kwani jamii imehamia huko.
Hayo
yameelezwa jana, na Afisa kutoka Tume hiyo Zanzibar, Abubakar Mohamed Chwaya,
alipokuwa akitowa mafunzo kwa wadau wa vituo vya radio katika ukumbi wa Shirika
la Utaanzaji Zanzibar ‘ZBC’ Mkoroshoni Chake chake Pemba.
Alisema mfumo
mpya wa kisasa ‘digital’ utawawezesha wasambazaji hao, kurahisisha kuondosha
muingiliano ya miundo mbinu ya sauti na kazi zao, baina ya kituo kimoja
na chingine.
Alieleza kuwa, kutumia mfumo huo utaondosha matumizi makubwa ya gharama katika
urushaji wa maudhui ‘content’ na utarahisha na matumizi madogo ya miundombinu.
"Mfumo mpya wa kisasa ya kidigitali, utawawezesha wasikilizaji wako, kujua mapema kupitia kioo cha radio kupata kujua jina la radio, pamoja na kujua masafa yako yaani ‘frequency, "alifafanua.
Afisa huyo alifahamisha kuwa, chombo chochote kitafanya kazi kwa mujibu wa
sheria, na Tume itaendelea kusimamia na kufuatilia kazi zao, ili kuhakikisha
hakuna uvunjifu wa maadili.
Alisema kuwa hawatolazimishwa sana kutumia
mfumo mpya wa kisasa ‘digital’ kutokana na miundo mbinu yao, lakini pia
mwenye uwezo wa kutumia mfumo wake wa zamani hatokatazwa.
Kwa upande
wake Issa Suleiman Othman kutoka Tume hiyo, alisema kupitia mfumo mpya wa
kisasa, itapelekea kuchakatwa kwa sauti, katika mfumo ulio bora na mzuri na
kumrahisishia msikilizaji kufaidika.
Alisema kuwa kupitia mfumo huo, utapelekea madhui na dhamira ya chombo chochote
kufikia, mbali na kuwa ni rahisi kuwafikia wasikilizaji wao.
Alifafanua kuwa changamoto nyingi zinazojitokeza kupitia mfumo wa ‘FM’ ina
gharama kubwa na masafa marefu ya kusafirishia mawimbi ya sauti.
Mratibu kutoka Tume ya Utangazaji Pemba Adam Ramadhan Kombo, aliwataka wadau wa
vyombo vya Radio, kuwa ipo haja ya kubadilika pamoja na kwenda na wakati, ili
kurahisisha kazi zao.
Alisema ni wajibu wao kuwaelimisha kutoka katika mfumo wa zamani kuingia katika
mfumo wa kisasa, ili kuingia katika kasi mpya itakayoleta maendeleo kwa
wasikilizaji.
Nao wadau wa vyombo hivyo, ameipongeza Tume ya Utangazaji kwa kuiondoshea gharama kubwa za kiutendaji wao kwani, Tume hiyo imekuwa ikileta msaada mkubwa kwa wadau hao.
Aliongezea kusema kuwa, kupitia mfumo huo ipo haja ya kueka gharama ndogo za
ulipaji wa mfumo huo, kupitia leseni zao.
|
Comments
Post a Comment