NA MCHANGA HAROUB, WMJJWW-PEMBA IMEELEZWA kuwa, uanzishwaji wa jukwaa la wanawake wajasiriamali, kutasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto zinazowakabili akina mama hao, katika shehia mbali mbali Zanzibar . Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Siti Abass Ali, wakati akizungumza kwa nyakati tofauti, na wajasiriamali wanawake wa wilaya nne za Pemba. Alisema pamoja na juhudi kubwa inayochukuliwa na Serikali katika kumuendeleza mwanamke, lakini bado imeonekana kuna baadhi ya maeneo yamekuwa ni kikwazo kufikia maendeleo yaliokusudiwa. Alieleza kuwa, pamoja na hayo, anaamini uanzishwaji wamajukwaa hayo, inaweza kuwa endelevu, ili kuwainua kiuchumi wanawake na hatimae taifa kwa juma. Mkurugenzi huyo alifahamisha kuwa, uwepo wa majukwaa hayo kutatoa fursa kwa akina mama, kupata chombo madhubuti cha kuzungumza pamoja na kuwa na sauti moja wanapotafuta dawa ya changamoto zao. Mkurugenzi...