NA HAJI NASSOR, PEMBA
WAKULIMA wa mazao ya kilimo cha biashara
ikiwemo ndizi, chungwa na muhogo, wa shehia za Mtambile, Mizingani, Chumbagaeni
na Wambaa wilaya ya Mkoani Pemba, wamahidi kulitumia soko jipya la Mtambile,
ili kuongeza thamani ya biadhaa zao.
Walisema,
kwa sasa wamepata mkombozi wa bidhaa zao, na hwenda ikiwa ndio mwisho wa
kulanguliwa na wachuuzi wa bidhaa mbali mbali wanaosafirisha nje ya Pemba, kw
akule kuwalalia kibei.
Wakizungumza na mwandishi wa habari mara baada ya kufunguliwa
kwa soko hilo, na Waziri wa Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Shamata
Shaame Khamis, walisema kwa vile wameshakabidhiwa, sasa ni kulitumia kwa kuuzia
bidhaa zao.
Mmoja katuia ya wakuliuma hao anaejishughulisha na kilimo
cha ndizi za mtwike, pukusa na koroboi Haji Kassim Khamis wa Mtambile, alisema
sasa baada ya kuvuna atakimbila kwenye mdana sokoni hapo.
‘’Kwa vile tumeshaelezwa kuwa, mnada wa bidhaa kama za
ndizi utakuwepo, sitouza tena ndizi zangu chochoroni na kulaliwa kibei, kama
ilivyokuwa zamani,’’alieleza.
Nae mkulima wa mihogo kwa ajili ya biashara Issa Hamdu
Ali wa Mizingani alisema, imekuwa ni kawaida soko lao wao, limo mikononi mwa
wachuuzi na wakati mwingine kuwadanganya.
‘’Anakwambia Unguja muhogo hauna bei, maana umeingia
mwingine kutoka Tanga, lakini kumbe huwa ni waongo, hivyo sasa watatufuata
sokoni Mtambile,’’alisema.
Nae Mwanaisha Omar Mkubwa wa Wambaa alisema hata chungwa
anazolima sasa hatozipeleka tena soko la Chake chake na atalitumia soko jipya
la Mtambile.
‘’Tunaomba tua masharti ya vibali na matozo mingine yawe
chini kwa sisi wafanyabiashara wadogo, ili tusijetukalikimbia soko letu, na
kurudi kwa wachuuzi wetu,’’alisema.
Mkurugenzi Baraza la mji wa Mkoani Yussuf Kaiza Makame,
aliwaahakikishia wakulima wa mazao mbali mbali, kuwa watawekewa mazingira
rafiki, ili kuwavutia kulitumia soko hilo.
‘’Kwanza waanze kulitumia soko hili, na kisha kama kuna
changamoto zozote tukae chini kwa pamoja, na kuona jinsi ya kuzitatua na mwisho
wa siku muendelee kulitumia, maana ni kwa ajili yenu,’’alifafanua.
Kwa upande wake, Katibu mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa, serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Issa Mahafudhi, alisema ujenzi
wa soko hilo, ni utekeleza wa ahadi ya Rais wa Zanzibar, wakati alipokutana na
wajasiriamali.
Hata hivyo alisema, mji wa Mtambile umekuwa na ongezeko
la watu kila mwaka, na sasa kuchukua nafasi ya tatu kwa idadi ya watu, baada ya
Chambani yenye wakaazi 7,460, Kengeja 7,202 na Mtambile 7,000.
‘’Hivyo uwepo wa soko hili, limeandana na mahitaji ya
wananchi kwa muda mrefu na hasa suala la changamoto, iliyopo ya wafanyabiashara
kuendesha shughuli zao pembezoni mwa barabara,’’alifafanua.
Mkuu wa Mkoa wa kusini
Pemba, Mattar Zahor Massoud, alisema serikali inampango wa kujenga soko jingine
kama hilo, katika eneo shehia ya Kengeja, ili kukidhi mahitaji ya
wajasiriamali.
Soko hilo la matunda na mboga la Mtambile inavyo vikuta
40, milango 13 ya maduka, ujenzi wake ulianza mwishoni mwa mwaka 2022, na kumalizika
mwezi Julai mwaka huu.
Ujenzi huo, umegharimu zaidi ya shilingi milioni 5.88
ambapo ni fedha zinazotokana na makusanyo ya baraza la mji Mkoani, kupitia
serikali kuu.
Mwisho
Comments
Post a Comment