NA HAJI NASSOR, PEMBA.
WIZARA ya Afya Pemba, imekiri kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, kwa mfanyakazi wake ambae ni daktari wa kituo cha Afya Gombani Chake chake.
Kaimu Afisa Mdhamini wizara huyo Pemba, Yussuf Hamad Iddi, alisema ingawa sio rasmi, lakini baada ya kufuatilia wamebaini kuwa hajaacha kazi, bali anashikiliwa kwa tuhma za kutorosha na ubakaji.
Alisema, ingawa taarifa za kesi hizo zaidi ziko kituo cha Polisi, lakini wanajua kwa sasa, mfayakazi wao huyo Is-haka Rashid Hadid, hayupo kazini kwa muda.
‘’Ni kweli mfanyakazi wetu ambae ni daktari katika kituo cha Afya Gombani wilaya ya Chake chake, alichukuliwa na Polisi, akiwa kazini, kwa tuhma za utoroashaji na ubakaji wa mtoto,’’alieleza.
Katika hatua nyingine, aliwataka watendaji wa wizara hiyo kisiwani Pemba, kuendelea kuheshimu maadili na sheria za kazi, ili kutoa huduma kwa uhakika.
Aidha alisema, kwa sasa wanaendelea kufuatilia hatua kwa hatua juu ya mwenendo wa kesi hiyo, licha ya kutokupokea taarifa rasmi kutoka kwa vyombo vya sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Juma Saadi Khamis, alithibitisha kupokea kwa taarifa hizo, na kusema kwamba upelelezi utakapokamilika atatoa taarifa rasmi.
‘’Mtuhumiwa tunae echini ya ulinzi, ambapo tulimpokea akitokea Jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba, na anaendelea kuhojiwa, baadae taarifa rasmi zitatolewa,’’alisema Kamanda.
Awali daktari huyo anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, alifikisha kituo cha Polisi Chake chake akikabiliwa na tuhuma za kumtorosha na kumbaka mgonjwa wake.
Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo baadea alihamishiwa mkoa wa kaskazini, kutokana na tukio hilo kutokea mkoani humo kisheria.
Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu.
Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo.
"Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje daktari fulani, kwa hiyo kesho (siku ya pili yake), atakuja kunichukua ili ukanipe dawa nyingine", alisema mtoto.
Alisema kuwa, siku ya pili wakati yupo skuli, daktari huyo alimpigia simu na kumeleza kuwa, akirudi skuli amsubiri kwa rafiki yake, mpaka atakapotoka kazini daktari huyo, ili akamchukue kwa ajili ya kumpatia dawa nyingine,
Tukio linalofafana hili, liliwahi kutokea Novemba 21, mwaka 2019, katika hospitali ya Chake chake, baada ya daktari wa kitengo cha Atrasaund, kudaiwa kuomba rushwa ya ngono kwa mjamzito, kama sharti la kumpa huduma.
Aidha Disemba 18, mwaka mwaka 2019, TBC 1, iliripoti Afisa Muuguzi msaidizi wa kituo cha Afya Mamba mkoani Katavi kushikiliwa na Jeshi la Polisi, kwa tuhuma za kumbaka mjamzito, wakati alipokuwa akimsaidia kujifungua.
Mwisho
Comments
Post a Comment