Skip to main content

MOHAMED KHATIB KHAMIS, MJASIRIAMALI ANAENDESHA MAISHA YAKE KWA UFUGAJI NYUKI, ANA MIZINGA 75




IMEANDIKWA NA HAJI NASSOR, PEMBA:


SASA ni saa 5:40 asubuhi, nipo pembezoni mwa nyumba ya mjasiriamali wa ufugaji nyiki, hapa kijiji cha Kidutani shehia ya Chumbageni, wilaya ya Mkoani Pemba.

Nilichukua dakika 35 kwa gari binafsi, kutoka katikati ya mji mkuu wa Pemba Chakechake, hadi hapa anapoishi mjasiriamali huyu.

Mohamed Khatib Khamis miaka 46, kwa sasa anaishi katika nyumba ya miti, mbele ya nyumba yake ameshusha baraza, ndogo alioijenga kwa miti na mabaki ya mbao.

Hapa anayobiashara ndogo ya viazi mbatata, vitunguu, mchele na sukari, ametengeneza mabao mithili ya daraja, hutumia kiti cha plastiki rangi ya bluu kuwasubiri wateja.

Hapa Kidutani, wapo wengine ni wafanyakazi serikali, ingawa kazi kubwa ya wakaazi wa eneo hili nimearifiwa, ni kilimo cha migomba, mihogo, michungwa na minazi.

Wapo wengine wakiwa na mashamba makubwa ya mikarafuu, na wachache wasiozidi watano, wamejiajiri kama alivyo mwenyeji wangu Mohamed Khatib Khamis.

Safari yangu wala haikushia hapo kwenye makaazi yake ya kudumu, sasa tulivaa viatu maalum na kukunja suruali zetu kuekelea anakofugia nyuki.

“Pita mbele, hapana pita wewe mwenyeji, aaa pita wewe ili siku ya pili uje peke yako, maana ni njia moja kwa moja, hadi eneo la Kitopeni nnakofuga nyuki,”ndio maneno yaliokuwepo wakati tukiondoka kwenda huko.

Safari nyengine ya dakika 20 ilianza, tukakikimbia kijiji cha Kidutani na tukaelekea Magharibi ya kijiji hicho, tukakiuka mabonde, mifimbi ya maji na vilima vidogo vidogo.

Kijua kilikuwa wastani, stori ndogo ndogo mimi na yeye zilianza, na wakati safari yetu tumeshaigawa nusu, na ilisita wakati tulipofika kilima cha kuteremka kikiwa na mtelezo kidogo.

“Pita kwa huku mwandishi, kamata hicho kigogo, angalia, hapo pana mfimbi wa maji na hapo mbele pana tope, kamera yako iangalia isije ingia topeni,”alinitahadharisha.

Dakika 25 zilipomalizika, tulifika kwenye eneo la Kitopeni, ukimnya na upepo mwanana, ndio ualiotukaribisha, ingawa nilikuwa nashuhudia nyuki wachache wakikatiza mbele yangu.

“Ngoja nikukaguze mizinga yangu 10 ilioharibika baada ya wadudu kama sisimizi kuvamia, na kupata hasara kama chupa 70 za asali,”alinieleza.



Hapo sasa kalamu na note book yangu, nikaitoa kwenye mkoba, ananipa kinaga ubaga kuwa, ameanza kazi hiyo ya ufugaji wa nyuki miaka 15 sasa.

Mohamed Khatib akiwa anahema hema kiasi, anasema alifikia uamuzi huo, baada ya kuona pato analohitaji ili kuendeshea maisha yake, halimtoshi.

Aliingia kwenye ujasiriamali huo kwa uzoefu tu, wala sio kwamba alishapata elimu, kama walivyo watu wengine kwenye kazi nyengine.

“Mimi tokea ninakotoka kwa vile ilikuwa hakuna ufugaji wa nyuki, nilikuwa mtaalamu wa kuvuna tena peke yangu, hivyo baada ya kuona matunda, nilipata hamu ya kufuga yangu,”ananieleza.

Alianza na mizingi 10 kwa hatua za awali, na alikuwa akiipitia mara kwa mara, hasa ilipokuwa karibu ya msimu wa kuvuna, na siku ilipofika, alivuna na hamu ya kuongeza mizinga ilimjia.

“Kwa hatua za awali nilipata wastani wa chupa 50, na baada ya kuuza, nikajitilia kibindoni shilingi milioni 1 kama ucheza tu vile,”ananieleza.

Hapo sasa, idadi ya kuongeza mizinga hadi kufika 30, ndio iliokuwa kazi yake, na alihamia msituni na vichakani kuyatafuta mizinga ya mabao.

Mizinga amabayo anayatengeneza mjasiriamali huyo, ni mabao ya miti minene, ambayo huwa na uwazi au sehemu ambayo huwaruhusu nyuki kuweza kuishi.

“Hivi karibuni, baada ya kufuatilia kwa kina na kusikia elimu fulani, hata yale matairi ya gari huwa nayakata na natumia na wananasa nyuki,”anaeleza.

Anakiri kuwa, tokea aanze kazi hiyo, hadi leo hawajahi kupewa elimu yoyote na shirika wala serikali, bali, hufuatilia vyombo vya habari na kujisomea vitabu kadhaa.

Binafsi anaamini amekuwa akipata mafanikio kila mwaka, kutokana na kazi yake hiyo, na sasa anasema kila kitu chake kinatokana na nyuki.

“Mimi nyumba yangu nyuki, nguo zangu, za watoto na mke wangu ni nyuki, lakini hata maisha yangu yanategemea uwepo wa nyuki ninazofuga,”anasema.

Mjasiriamali huyo, anasema wastani wa shilingi milion 10 tokea aanze kazi hiyo miaka 15 sasa, ameshajipatia ingawa ameshazitumia kwa mambo tofauti.

Kama engekua hajatumia fedha hizo, zinazotokana na uuzaji wa asali, basi leo engeesabu machenji ya shilingi milioni 15, lakini zimeshamsaidia kimaisha.

Mizinga hiyo anasema, anaifuga kwenye msitu ambao sio milki yake, lakini anaamini ni pori ambalo wenyewe hawalitumii kwa muda mrefu sasa.

“Hili pori ambalo mnamizinga yangu ifikayo 75, sio langu lakini wenyewe hawalitumii, hivyo mifugo yangu ya nyuki, haiathiriki na imetulia,”anasema.

Kutokana na ukosefu wa elimu ya ufuga nyuki, anaona ndio maana, hujitokeza mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kukosa utaalamu wa kuwakimbiza wadudu kama sisimizi na koyo koyo (MAJI MOTO) kushambulia mizinga yake.

Anakiri kuwa, wizi bado haumjasumbua sana, maana siku za mavuno ya asali, hukikimbia kitanda na kuzunguruka msituni kila baada ya muda.



“Hapa tatizo langu la kwanza, ni kukosa njia ya kuwadhibiti wadudu, maana wameshanitia hasara kama mizinga 10 mwaka jana, ilikimbiwa na nyuki,”ananifafanulia.

Laiti kama sio mizinga yake kuvamiwa na wadudu, basi engepata wastani wa chupa 70 za asali, na kujitilia kibindoni shilingi milioni 1.7 lakini ndio amezikosa.

“Unajua kila mzinga huvuna kati ya chupa saba au tano, na mizinga 10 mwaka jana, nilipofika imekimbizwa na wadudu, ni hasara iliotokana na ukosefu wa elimu,”anasema.

Tatizo hilo hasa ameligundua kipindi cha mvua za mwaka jana, ambapo wadudu hao, hukosa sehemu za machumi, ndio maana hushambulia asali.

Changamoto nyengine, ambayo anakabiliana nayo kwenye ujasiriamali huo, ni kukosa mizinga ya kisasa aina ya masanduku kwa ajili ya ufugaji.

Anasema mizinga hiyo ambayo ni ghali, lakini ndio mizuri kwa ufugaji na nyuki, huhifadhika hata kwa siku za mvua au wadudu kama sisimizi sio rahisi sana.

“Mizinga ninayotumia mimi ni hii ya kawaida na kuokota bao lenye uwazi, na kulichimba chimba kisha napaka nta kwa ajili ya kufugia nyuki,’’anasema.

Mjasiriamali huyo, kwa sasa malengo yake kwenye ufugaji wa nyuki, ni kuigawa mizinga yake, ambapo nusu kuibakisha misituni na mengine kufugia nyumbani.

“Kutokana na fedha niliopata hapa nimeshanunua eneo la kujenga nyumba, na nimeshapanga kuweka vyumba kama vitatu kwa ajili ya kufugia nyuki,”anasema.

Ameshafanya utafiti na hata kuzungumza na baadhi ya wafugaji nyuki, kwamba inawezekana kuifuga ndani na bila ya kuleta athari kwa jamii.

Anaamini kazi yake hiyo, itamuimarishia uchumi wake, na kufikia mafanikio makubwa kwake yeye, familia na taifa kwa ujumla.

“Maisha hayamtafuti mtu, bali maisha ndio yanataka yatafutwe na mtu, sasa na mimi hapa nimeshaanza na kama mambo yatakwenda kama nilivyojipangia, basi nna hakika hata kuajiri watu wengine hapo baadae,”anasema.

Kwake yeye mjasiriamali huyu wa ufugaji wa nyuki, anasema hajafikiria na wala hana mpango wa kujiunga kwenye vikundi vya ufugaji kama Jumuia, kutokana na msimamo wake.

Anaamini moja ya kuzima ndoto za maisha kama yake yeye ya nguvu kazi, ni kujikusanya pamoja, kutokana na watu waliowengi kwa Karne hii, wamepoteza uaminifu.

“Sipingi kuwa umoja na ni nguvu, lakini naamini pia upeke ni silaha maana sasa wizi, utapeli, ujanja na kutokuwa waaminifu ndio jamii kubwa ya leo,”anasema.

Kwa sasa mjasiriamali huyo tayari ile nyumba yake ya miti na yenye bati, ameshajiungia huduma ya umeme, na hata kuvuta huduma ya maji kwa mfereji wa nje.

Aidha ameshaanzisha biashara ya genge la chakula kama vile mchele, sukari, mbatata, tungule na kuza juisi ambapo mtaji huo wa shilingi laki 500,000 umetokana na mauzo ya asali.

Amekuwa akiuza chupa moja ya asali kwa wastani wa shilingi 20,000 hadi shilingi 25,000 ambapo anasema hana tatizo la soko hata kidogo.

“Haimalizi wiki napigiwa simu watu wanataka asali, maana kwanaza kwa sasa kumejaa utapeli kwa asali ya kupika, sasa sisi wafugaji watu wanatuamini sana,”anasema.

Mjasiriamali huyo alieanza kazi hiyo miaka 15 sasa anafamilia ya watu tisa, wanaomtegemea na anamiliki mizinga 75 peke yake, ingawa mwaka jana mizinga 10 ilishambuliwa na wadudu.

Binafsi yeye wala watoto wake, hakumbuki siku aliowapeleka hospitali kwa sababu ya kushikwa na homa ndogo ndogo, maana sasa amekuwa akitumia asali.

Wanaomfahamu mjasiriamali huyo kijijini hapo, wanasema amekuwa na msimamo wa kazi kuliko maneno na kubakia barazani muda wote.

Mohamed Haji Juma, anasema licha ya changamoto anazopitia, lakini ameonesha moyo wa kweli katika kuyasaka maisha, hadi amekuwa mfano kijijini kwao.

Asha Mussa Makame, anasema Mahamed Khatib amekuwa mkombozi kwao, kutokana na kutoadimikiwa na asali ambayo ni ya uhakika hasa kwa ajili ya dawa.

“Sisi tukitaka asali ya kweli, wala hatuendi mbali sasa twapiga hodi kwa Mohamed, na hapo huuziwa asali safi na ya uhakika, ndio faida kubwa kwetu,”anasema.

Kijiji cha Kidutani shehia ya Chumbani wilaya ya Mkoani Pemba, wapo vijana kadhaa waliojiari akiwemo Omar Amin na Rashid Ali wanaofuga kuku, Omar Ali Makame akijishughulisha na kilimo cha mboga mboga.

Lakini hata Mtumwa Mohamed Bakar akijishughulisha na biashara ndogo ndogo kama vile ya uji na maandaizi.

                  mwisho 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...