NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@@
WIZARA
ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, imeshauriana na kukubaliana na
kampuni ya Reform spots, kwamba sasa uwanja wa mpira wa mkoa wa kaskazini Pemba,
uhamishiwe eneo la Kinyikani, badala ya Kishindeni.
Hayo
yalifahiamika jana, kwenye ziara ya Waziri wa huyo, Riziki Pembe Juma na Katib Mkuu
wake Mattar Zahor Massoud, baada ya kutembelea ujenzi unaozorota wa uwanja wa
mkoa huo, eneo la Kishindeni.
Akiwa eneo
hilo, Waziri huyo na ujumbe wake, walieleza kushangaazwa kwao, na kuzorota kwa
ujenzi wa uwanja huo.
Waziri
Pembe, alisema haiwezekani uwanja huo kuwenda mwendo wa kusuasua ujenzi wake,
ingawa baada ya kuelezwa sababu, alishauri kuhamishiwa ujenzi wake.
Alisema,
kama inawezekana, kusiwe na gharama za nyongeza kwa ujenzi wa eneo la Kishindeni,
kutokana na uwepo wa hatarishi ya eneo hilo kuvamiwa na maji.
Alifafanua
kuwa, kama wizara inalo eneo la Kinyikani na ni tambarare, ni vyema ujenzi wa
uwanja huo, sasa kuhamishiwa hapo.
‘’Nashauri,
kama hapa Kishindeni inabidili ili kujengwa uwanja wa mpira wa miguu, mjenzi
aongezewe gharama, ni vyema tutafuta eneo mbadala,’’alifafanua.
Waziri huyo
pamoja na ujumbe wake, baada ya kulitembelea na kujionea eneo la Kinyikani, na
kisha kushauriana na kampuni, wazo lilipita kuhamishia eneo hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari, baada ya kushauriana na kampuni ya ujenzi wa uwanja huo
ya Reform Spotrs, Waziri Pembe, alisema sasa uwanja huo utajengwa eneo hilo.
‘’Niwambie
wananchi na wapenda michezo, sasa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa mkoa wa
kaskazini Pemba, utajengwa Kinyikani na sio tena Kishindenei,’’alifafanua.
‘’Hata
eneo hili la Kinyikani nalo ni serikali, na liko tambarare, sasa
tumeshakubaliana kuwa, ujenzi wa uwanja wa mkoa utahamishiwa hapa Kinyikani,’’alifafanua.
Wakati huo
huo, Waziri Pembe, alisema maandalizi ya ujenzi huo, alitaka uanze kuanzia leo Disemba
17, mwaka huu na kumtaka Afisa Mdhamini kupita kila wakati.
Mapema
Katibu Mkuu wizara hiyo, Mattar Zahor Massoud, alisema serikali haipendi kutumia
gharama kuwa, ikiwa uwezekano wa gharama ndogo upo.
Katika hatua
nyingine, Katib Mkuu huyo aliwataka wanachi kuendelea kushirikiana, na wajenzi,
pindi ujenzi utakapoanza.
Alieleza kuwa,
Rais wa Dk. Mwinyi amekuwa mwanamichezo mkubwa, na kupelekea kuhakikisha, anasambaaza
viwanja vya kisasa ngazi ya mkoa na wilaya.
Kaimu
sheha wa sheha ya Kinyikani Othman Maalim Othman, ameishukuru wizara, kwa
uamuzi wake, wa kuhamishia ujenzi wa uwanja huo, shehiani humo.
‘’Sisi
serikali ya shehia, tumefurahi mno, kuona sasa mradi mkubwa wa ujenzi wa uwanja
huu wa mkoa, wa kaskazini Pemba, utajengwa eneo hili,’’alifafanua.
Kijana wa
eneo hilo Hamad Khatib Salim, alisema ujio wa uwanja huo shehiani mwao, itawapa
ari na hamu zaidi sasa ya kupenda michezo.
‘’Kwanza
hatunabudi kumshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Hussein Ali Mwinyi, kwa kasi yake ya ujenzi wa viwanja vya michezo kadhaa,’’alifafanua.
Mapema
Mshauri Elekezi kwenye mradi wa ujenzi wa viwanja hivyo, Fesal Soud, pamoja na
Meneja wa mradi kutoka kampuni ya Reform Sprts, Mohammed Oobbsoglu,
wamekubaliana na ushauri wa wizara hiyo.
Meneja
huyo, alisema eneo hilo ambalo ni tambarare, ni zuri zaidi, hasa kwa vile hata
gharama yake itakuwa nafuu.
‘’Eneo la
Kishindeni linahitaji kwanza, liwekewe kifusi ili kupatikana tambarare, maana
linakabiliwa na uwezekano wa kuingia maji ya mvua kwa wingi, tofauti na hapa,’’alifafanua.
Waziri
huyo wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja na ujumbe, wake walitembelea
ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu, Micheweni, Mchanga mdogo, Kinyikani,
Pandani na kuzitembelea Idara zilizochini yake.
Mwisho
Comments
Post a Comment