NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo
Zanzibar, Riziki Pembe Juma, ametoa mwezi mmoja na nusu, kuanza ujenzi wa vyoo
vya wanawake na wanaume, katika uwanja wa mpira wa kikapu Tenis Chake chake.
Alisema, haiwezekani kama wafadhili wamesaidia kujengja
uwanja huo, kisha kuwasubiria kujenga na vyoo, hivyo ni vyema, jambo hilo likaratibiwa
na wizara husika kwa haraka.
Waziri Pemba, alitoa agizo hilo jana, wakati alipofika uwanjani
hapo, kukagua uwanja huo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu kisiwani
Pemba, tokea alipochaguliwa.
Alisema, anataka kuona ndani ya mwezi mmoja na nusu, iwe
harakati na maandalizi ya vyoo hivyo umeshaanza kwa kasi, ili kuona wapi wamekwama
na kusaidia.
Alieleza kuwa, kama taasisi ya kimataifa ya ‘GIZ’ imeshasaidia
kujenga viwanja vya aina hiyo Unguja na Pemba, na kama hawakufanikiwa kujenga
vyoo, wizara hiyo ifanye.
Waziri Pemba, alifafanua kuwa mwezi mmoja na nusu unatosha
kwa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Pemba, kuviendeleza vyoo vilivyopo.
‘’Kama vipo vyoo ambavyo walikuwa wakitumia wale
waliokuwa wakijenga uwanja huu, ni wakati sasa kwa wizara hii Pemba, hilo kulifanyia
kazi,’’alifafanua.
Aidha Waziri Pembe, alisema uwepo wa vyoo hivyo utasaidi
kuimarisha kwa wanamichezo wakiwemo wanawake na wanaume, kupata pahala pa
kujistiri.
Wakati huo huo Waziri huyo, alipongeza ushirikiano uliopo
ndani ya wizara hiyo, na kufanikisha ujenzi wa viwanja kadhaa vya michezo.
Mapema Afisa Mdhamini wa wizara hiyo Pemba, Mfamau Lali Mfamau,
alimueleza Waziri huyo kuwa, walikuwa wanafuatilia kwa ‘GIZ’, juu ya ujenzi wa
vyoo hivyo.
Alieleza kuwa, wako kwenye mazungumzo ya muda mrefu, na
kwa vile eneo hilo la Tibirinzi ilikuwa sio ujenzi wa moja kwa moja, bali ni ukarabati.
Kamisha Idara ya Michezo Zanzibar Ameir Mohammed Makame,
alifahamisha kuwa, ukarabati kama huo, pia umefanyika eneo la skuli ya Regeza Mwendo.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mattar Zahor Massoud, alisifu
umoja na mshikamo wa watendaji wa wizara hiyo, unaofanikisha miradi kadhaa.
Alieleza kuwa, wizara hiyo imekuwa tegemeo kwa wananchi,
katika kuendeleza, michezo, utamaduni na Sanaa kwa maslahi mapana ya taifa.
Aidha, alimueleza Waziri huyo, wazo la kujenga wenyewe
choo katika uwanja huo wa Tenis, ni jema na watalifanyiakazi.
Awali Sheha wa shehia ya Kichungwani wilaya ya Chake
chake, Yussuf Saleh Salim, alisema uwanja huo umekuwa msaada mkubwa kwa vijana,
katika kukuza vipaji vyao.
Hata hivyo, alimuomba Waziri huyo kuujengea kinga uwanja
huo, ili usitumike hovyo, na watoto ambao hupitisha baiskeli na kupiga miserereko.
Katika ziara hiyo,
Waziri Pembe na ujumbe wake, walitembelea ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu
Ukutini, Kangani, Gombani na Wakala wa Uchapaji ofisi ya Pemba.
mwisho
Comments
Post a Comment