NA SALMA
OMAR, PEMBA @@@
ANGOZA
kwa kushirikiana na Mashirika ya kiraia pamoja na serikali, zimeiasa jamii kushirikiana kwa pamoja katika
kukabiliana na changamoto za haki ya tabia ya nchi.
Hayo
yamesemwa katika mkutano wa mafunzo na majadiliano yaliyoshirikisha jamii na
taasisi mbalimbali zikiwemo asasi za kiraia, pamoja na wawakilishi kutoka
serikalini katika ukumbi wa Samail Gombani Chake chake Pemba.
Mwenyekiti
wa ANGOZA Hassan Khamis Juma, amesisitiza jamii kushirikiana kwa pamoja katika
kukabiliana na haki za tabia ya nchi, ikiwemo kujiepusha na uharibifu na
uchafuzi wa mazingira.
Alieleza kua
kwani, kufanya hivyo kunaweza kupelekea
athari kubwa katika jamii na kusababisha maafa baadae, na jamii kuishi katika
mazingira magumu.
‘’Niwaombe
sana wanajamii, kwanza waziunge mkono asasi kama ANGOZA, maana zinakuwa na
wajibu wa kuhakikisha wanawakinga wananchi na majanga kadhaa, yakiwemo ya
athari za mazingira,’’alisema.
Kwa upande
wake, mwakilishi kutoka Jumuiya ya Community Forest Pemba, Omar Mtarik, amesema
utunzaji wa misitu na mali asili katika jamii, ni muhimu kuzingatiwa kwa kina.
Alifahamisha
kuwa, kwani zinaleta tija na faida kubwa za kiuchumi na kimaendeleo, katika
jamii na taifa kwa ujumla, ikiwemo
utunzaji wa mikoko na bahari na hata utengenezaji wa bidhaa kama viungo.
Nae mwakilishi kutoka serikailini alieshiriki
katika majadiliano huo, Ali Said Awesu amesema serikali, imejipanga kikamilifu
katika kuhakikisha inashirikiana na asasi za kiaraia na jamii kwa ujumla.
Alisisitiza kuwa, hata ndani ya Ilani ya chama
cha mapinduzi CCM ya mwaka 2025/2030 katika kukabiliana na haki ya tabia za
nchi, katika kuandaa mazingira mazuri kwa jamii ikiwemo kuwapatia fedha wajasiriamali
wadogowadogo, hasa akinamama na watu wenye mahitaji maalum na vijana.
Katibu Mkuu wa klabu ya waandishi wa habari
Pemba, PPC Ali Mbarouk Omar, alisema jamii yenyewe inatakiwa kuwa mstari wa
mbele, katika kuhakikisha uharibifu na
uchafuzi wa mazingira hautokei.
Alifahamisha
kuwa, kwani wao ndio chanzo cha uharibifu wa mazingira, kwa kuwepo tabia za
baadhi ya watu, kwa ukataji wa mikono, uchimbaji
wa mawe na matofali pamoja ukataji wa misitu ya juu.
Mshiriki Kauthar Is- Haka, ameushukuru uongozi
mzima wa ANGOZA kwa kushirikiana na COMMON WEALTH FOUNDATION kwa kuandaa
mafunzo hayo, yanayohusu mabadiliko ya haki ya tabia za nchi, kwa kuwajengea
uwezo wanawake katika kuwaongoza na kuwasimamia katika kazi zao za kila siku.
Aidha aliishukuru serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, katika kuwasaidia wanawake suala la kukabiliana na mabadiliko ya
tabia za nchi, kwa kufanyakazi pamoja kwa kushirikiana na asasi za kiraia
katika kuiendeleza jamii iliyo bora.
mwisho




Comments
Post a Comment