NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@
ARV ni dawa zinazopambana na virusi vya VVU kwa mtu anayeishi na maambikizi ya virusi hiyo.
Wataalamu wa afya mwanadamu wanakubali kuwa, dawa hizo zinasaidia mno
kumpa uhakika wa kusihi, mtu anayeishi na
VV.
Wanakubali kuwa, zenyewe hazitibu VVU,
bali huzuia virusi kuongezeka na kulinda kinga ya mwili.
Lengo ni
kupunguza virusi hadi kufikia kiwango cha kutogundulika (undetectable).
Wataalamu wa afya wanasema dawa za ARV, zinaingia ndani
ya seli za kinga na kuzaliana, na kisha hukatiza
hatua za uzalishaji wa virusi kwa njia hiyo.
Kitaalamu kuna madaraja mbali mbali ya ARV, lakini huwa
hutolewa kwa pamoja kama mchanganyiko.
Mfano,’T+L+D’ huu ni mfumo wa kitaalamu ambao ni mchanganyiko
wa kidonge kimoja chenye dawa tatu, ambapo daktari
huchagua dawa kulingana na afya ya mgonjwa.
Daktari Khamis Hamad Ali ambae ni Mratibu wa
kitengo cha maradhi ya Ukimwi, homa ya Ini, Kifua kikuu na Ukoma Pemba, anasema
moja ya faida za matumizi ya ARV ni kupunguza kiwango cha virusi (viral
load).
Anasema hii ni kulinda na kurudisha kinga ya mwili
kupanda kwa seli za ‘CD4’ kupunguza hatari ya kuambukiza wingine.
MAAJABU YA MINGINE YA ARV
Mratibu huyo anasema, tafiti mbali mbali zilizofanywa na wataalamu wa
afya na hata kuthibitishwa na WHO, kwamba sasa dawa hizo ni kinga ya VVU kutoka
kwa mama kwenda mtoto.
Haya yatawezekana ikiwa mjamzito mwenye VVU atafuata maelekezo ya
wataalamu wa afya, yakiwemo ya matumizi sahihi ya dawa za ARV.
Anathibitisha kuwa, dawa hizo sio tu kuwa na uwezo wa kumkinga mtoto,
bali hata mama mwenyewe kufubaza (kupunguza) na hata wakati mwingine
kutoonekana kwa virusi mwilili.
Kumbe ARV zikitumika vyema na chini ya uangalizi wa daktari, uwezekano
wa kuzaliwa mtoto akiwa salama ni mkubwa kwa asilimia zaidi ya 90.
Anasema sio tu ARV zinamkinga mtoto huyo anapokuwa na maisha ya tumboni,
bali hata wakati wa kuzaliwa na kunyonyeshwa.
Ili kumkinga mtoto huyo pamoja na mama kutumia dawa za ARV,
wanahakikisha wakati anajifungua damu zao hazichinganyiki wawili hao.
Daktari Khamis anasema mara baada ya kuzaliwa kwake mtoto huyo,
hufanyiwa vipimo, ili kugundulika ikiwa ana VVU au laa.
‘’Lengo ni kugundua afya, na ikiwa ameambukizwa haraka kuanzishiwa dozi
ya ARV, yenye lengo la kupunguza makali na ikiwa hana, anaweza kurejeshwa tena
kwa uchunguuzi,’’anasisitiza.
Akawakumbusha mama wenye VVU kuhakikisha wanawanyonyesha watoto wao
chini ya maelekezo ya wataalamu wa afya, na sio zaidi ya miezi sita.
‘’Ikimalizika miezi sita, mama huyo hutakiwa kumuanzishia vyakula vya
lishe, ambayo vitakavyosaidia kuimarisha afya na makuzi yake,’’anasema.
Shuhuda wa hili ni Maryam Salim wa Chake chake, ambae anaishi na VVU kwa
zaidi ya miaka 17 sasa, amepitia hatua hii ya kupata watoto bila ya maambukizi.
‘’Ni kweli ninao watoto wanne, ni mmoja tu mwenye VVU kwa kule
kunyanyapaliwa, nilikosa matumizi sahihi ya ARV na kumuambukiza,’’anasema.
Anakiri kuwa, mimba zake nyingine baada ya kukubali ushauri wa wataalamu
wa afya, aliwabebea mimba na kuwanyonyesha na hadi sasa wako salama.
‘’Matumizi ya ARV kama utayafuata kama wataalamu wanavyotaka, mbona ni
kinga tosha ya kutomuambikiza mtoto na VVU,’’anakiri.
Kumbe nae anakiri kuwa, miezi sita ilitosha kwa kila mtoto wake
kumnyonyesha, na kisha kuwaanzishia mlo kamili, uliojenga afya zao.
Muume wa Maryam Sabri Issa Mbega, ambae hadi sasa yuko salama, anakiri
kuwa ARV ndio mwarubaini wa kuwa na watoto watatu bila ya VVU.
‘’Kwanza nilikuwa nafikiria tu kwamba ARV ni kwa ajili ya kupunguza makali
kwa mke wangu mwenye maradhi ya Ukimwi, lakini kumbe ni kinga kwa watoto
wangu,’’anasema.
JAMII
Issa Ali Khamis wa Wete, anasema wamekuwa na woga kufunga ndoa na kuzaa
na wanawake wenye VVU, kwa hofu ya kuambukizwa wao, na watoto wao.
‘’Mimi ninachokifahamu kuwa ARV ni kwa ajili ya kufumbaza makali ya VVU,
lakini kumbe sasa watalaamu wamebaini, ni kwa kinga ya mtoto ni jambo
jema,’’anasema.
Wahida Omar Haji wa Wawi, anaona kama kivuli anaposikia ‘ARV’ kuwa sasa
zimekuwa kinga ya ‘VVU’ kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,’’anaeleza.
Mchanga Said Kombo wa Chake chake, anakiri kuwa hata jirani yake,
ameshazaa watoto wawili na kuwanyonyesha miezi sita sita na sasa wako salama.
TUME YA UKIMWI
Ali Mbarouk Omar ambae ni Mratibu wa Tume ya Ukimwi Pemba, anasema ARV
sasa ni zaidi ya dawa ya kufubaza makali ya ukimwi, kwani imegeuka kinga ya VVU
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
‘Tunawahimiza wajawazito wenye maambukizi ya VVU, kutuma dawa kwa
usahihi, ili kujenga afya yake na magonjwa mingine nyemelezi, na kumkinga mtoto
aliyeko tumboni,’’anasema.
TAKWIMU
Wapo watoto 500 tayari wameshazaliwa wakiwa hawana maambukizi ya VVU
kutoka kwa mama, ambao wanaishi na maradhi hayo.
Idadi hii iliyothibitishwa na Mratibu Khamis Hamad Ali ni kwa mwaka 2024
kutoka wilaya nne za Pemba.
Anasema wote hao wazazi wao walikubali kufuata kikamilifu ushauri,
maelekezo na miongozo ya watalaamu wa afya.
Ingawa kwa kipindi hicho pia, wapo wingine saba ‘7’ ambao wazazi wao
walikuwa wagumu kwanza, kutumia ARV, na ushauri mwingine na hatimae
kuwaambukiza wakati wa kujifungua au kuwanyonyesha.
WHO
Shirika la Afya
Duniani (WHO) na mashirika mingine ya
afya yalipendekeza, mama mwenye
VVU kunyonyesha mpaka mtoto atakapofika miezi sita ‘6’ au chini ya
hapo.
Kwenye mataifa yanayoendelea Tanzania ikiwemo, familia
zisizokuwa na kipato kikubwa, zinaweza kuhitimisha miezi sita na kisha kuwaanzisha
vyakula vya lishe.
WHO inakiri kuwa faida mojawapo kubwa ya kunyonyesha mtoto
ni kumpatia kinga imara, kupitia
katika maziwa ya mama ili kupambana na vimelea mbalimbali vya magonjwa.
MITANDAO YA KIJAMII
Katika taarifa mpya ya ‘BAN’ matokeo yanaonesha kwamba hatari ya maambukizi ya VVU
huongezeka mara mtoto anapoacha kunyonya akiwa na miezi sita.
Katika
kukabiliana na hili, Shirika la Afya Duniani linapendekeza kwa mama mwenye
maambukizi ya VVU kuendelea kumnyonyesha mtoto wake mpaka atakapofikisha mwaka mmoja.
Katika
tafiti hii ambayo ilifanyika nchini Malawi katika kipindi cha mwaka 2004/2010, daktari. Denise J. Jamieson, kutoka kituo cha kudhibiti na kuzuia
magonjwa, (CDC) cha huko Atlanta, nchini.
Hitimisho katika
tafiti hiyo ilikuwa kwamba kumuachisha mtoto kunyonya maziwa ya mama mapema
siyo njia salama na sahihi, kwani mikakati ya
kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa watoto.
WIZARA YA
AFYA
Wizara ya
Afya ya Tanzania imefanya juhudi kubwa kupunguza maambukizi ya
VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, na kiwango
cha maambukizi kimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2010 hadi
asilimia 8.1 kwa mwaka 2023.
Wizara
imeanzisha kampeni za uhamasishaji ili kuongeza ufahamu kuhusu umuhimu wa
kapimana magonjwa kadhaa kwa
wajawazito.
Hii
inasaidia kuhakikisha kuwa wanawake wanaoishi na ugonjwa huo, wanapata amatibabu sahihi ili kuzuiya maambukizi kwa watoto
wao.
Ushirikiano
na washirika wa maendeleo,Wizara inashirikiana na mashirika kama USAID na tume
ya taifa kudhibiti ukimwi (TACAIDS), ili
kuimarisha mikakati ya kupambana na vvu.
Kiwango cha maambukizi ya VVU, kutoka kwa
mama kwenda kimepungua kwa zaidi ya asilimia
95 ya watoto waliozaliwa na bila maambukizi.
MWISHO.
Comments
Post a Comment