NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya
ACT- Wazalendo Othman Massoud Othman, amesema kama akipata ridhaa ya kuiongoza
Zanzibar, atakuza uchumi, kwa kulibinafsisha zao la karafuu.
Mgombea huyo wa urais wa aliyasema hayo leo Septemba
30, 2025, uwanja wa mpira wa Daya Jimbo la Mtambwe wilaya ya Wete Pemba, wakati
akizungumza, kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho, jimboni humo.
Alisema, Zanzibar katika eneo moja la kukuza uchumi
ni wakulima wa karafuu, hivyo atahakikisha analiimarisha zao hilo kwa
kulibinafsisha.
Alieleza kuwa, anachohitaji ni kupewa ridhaa kutoka
kwa wananchi, ili kuhakikisha zao la karafuu analiongezea thamani na kurudi
mikononi kwa wakulima.
Alieleza kuwa katika eneo hilo, atahakikisha anaongeza
pia bei na kufikia kilo moja shilingi 20,000 ili kuhakikisha linamnufaisha mkulima.
Aidha mgombea huyo wa urais, alisema ili kuhakikisha
mkulimana anafaidi zao hilo la taifa, nni kulibinafsisha.
‘’Mkinipa ridhaa nitahakikisha zao la karafuu,
kwanza tuliongezea thamani, lakini pia tutalibinafsisha ili kila mmoja awe na uhuru
nalo,’’alifafanua.
Katika hatua nyingine Mgombea huyo wa urais wa
Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo Othman, Massoud Othman, alisema anakusudia
kuifanya Mtambe kuwa kitovo cha uzalisha za viungo, ikiwemo vanilla.
Alisema, anaompango wa kweli wa kuhakikisha
anaoundoa umaskini kupitia uwekezajiwa kilimo ikiwemo cha viungo.
Alieleza Mtambwe, itakuwa ndio kwa Zanzibar ambapo
watu wingine wanakuja kujifunza katika kilimo cha viungo.
Mapema Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar
Ismail Jussa Ladu, alimtaja muasisi wa wao Maalim Seif Sharif Hamad, kama mkombozi
wa wananchi wa Zanzibar, kwa ile hamu na tunu yake.
‘’Leo tunaendeleza mapambano ya kupigania haki za
wananchi wa Zanzibar, ni dhahiri kuwa, tunae Othman Massoud, lakini hatutoacha
kumkumbuka marehemu Maalim Seif,’’alifafanua.
Katika hatua nyingine, aliwataka wasimamizi wa uchaguzi
kutoka ndani ya ACT-Wazalendo, kusimamia haki za wananchi, ili wawe chanzo kwa
chama hicho, kushinda.
‘’Niwaambie wenzetu wa ACT-Wazalendo ambao
watashiriki kwenye uchaguzi, lazima wawatumikie wapiga kura, na wahakikishe
wanasimamia kura kwa mujibu wa sheria zilivyo,’’alifafanua.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Omar Ali Shehe,
alisema tayari mgombea huyo, ameshafanya mikutano katika majimbo 22 ya Unguja
na Pemba.
Alisema, katika mikutano hiyo ya hadhara, pia amefanya
mikutano ya kukutana na makundi mbali mbali, wakiwemo wajasiriamali na
watumishi wa umma.
‘’Leo tukiwa hapa jimbo la Mtambwe, kwa mgombea wetu
hili ni jimbo la 22, na tayari mikutano yake imeshaonesha dalili za ushindi,
kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu,’’alisema.
Katika hatua nyingine, Naibu Katibu Mkuu huyo,
alisema ili kuhakikisha hilo kwa vitendo, ni vyema kila mmoja ahakikishe kura
yake, ni kwa wagombea wa ACT-Wazalendo.
Kwa upande wake Mbunge mstaafu wa Jimbo la Mtambwe
Khalifa Mohamed Issa alisema, tayari kwa mikutano hiyo 22 ambayo ameshaifanya
mgombea wao, ishara ya ushindi iko wazi wazi.
Aidha, alimtaka mgombea huyo, pindi akipata ridhaa, ahakikishe
anaimarisha miundombinu ya wavuvi, ili bahari iwe kimbilio kwao.
‘’Wananchi wa Zanzibar na hasa hawa wa Mtambwe,
wingi wao ni wavuvi na maisha yao wanayetegemea moja kwa moja kwenye eneo hilo,
hivyo kama ukipata ridhaa, uwaone kwa jicho la huruma,’’alifafanua.
Kuhusu sifa za mgombea huyo wa urais wa Zanzibar kwa
tiketi ya ACT-Wazalendo Othman Massoud Othman, alisema ni mtu wa watu, mwenye
utu, anaeyafahamu mazingira ya wananchi wa Zanzibar.
‘’Mgombea wetu huyu ni mtetezi wa haki za watu na ushahidi
pale alipokuwa Mkurugenzi wa Mashtaka, kesi kadhaa za uzushi alizifuta ili haki
itendeke,’’alifafanau.
Mbunge wa Ubunge jimbo la Mtambwe Mohamed Rashid,
amewaomba wananchi kumpa kura, ili kuwaletea maendeleo.
Kabla ya
mkutano huo, wasanii kadhaa akiwemo Cholo ganuni, walinogesha mkutano huo,
pamoja na vikundi kadhaa vya burudani, kutoka mji wa Wete na vitongoji vya mji
huo.
Mwisho
Comments
Post a Comment