IMEANDIKWA NA KHAULAT SULEIMAN, SUZA
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Leila Muhamed Mussa amesema, kupitia
viwanja vya michezo vitasaidia kuleta mageuzi katika Serekali na kuibua vipaji kisiwani Pemba .
Aliyasema hayo katika hafla ya ufunguzi wa mradi wa ujenzi wa viwanja vya mpira katika uwanja wa skuli ya Sekondari Mchangamdogo wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema kuwa, mtaala wa elimu ya michezo utasaidia kwa asilimia kubwa kutoa watalamu
na vipaji mbali mbali kutoka skuli
na hata mitaani kwa kuwajengea uwezo wa kitaalamu na kufanya mazoezi kwa wingi, ili kuleta mabadiliko katika sekta ya michezo.
"Wizara ya Elimu
imejizatiti kusaidia kutumika viwanja hivyo kwa kuleta mabadiliko kwa wanafunzi
hususan masuala ya michezo, kwani michezo ni afya ambayo itawawezesha vijana hao kujiajiri wenyewe,” alisema Waziri huyo.
Alisema kuwa, sasa ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha mnatoa ushirikiano kwa walimu na watoto wenu kuachana na
dhana mbaya ya kuwa michezo ni uhuni na kupoteza muda na badala yake waiondoe,
ili waweze kupata mabadiliko.
Aidha aliishukuru Wizara ya Habari kwa kushirikiana na Serekali ya Ujerumani na mkandarasi wa ujenzi huo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Maendeleo ya Jamii kwa kuanda mradi huo wenye lengo la kukuza sekta ya michezo kisiwani Pemba.
“Viwanja hivyo vitumike kuleta mabadiliko katika jamii, vijana ambao wapo mitaani sasa kuitumia fursa hii kwa kuunda vikundi na kufanya mazoezi katika viwanja hivyo, ili kupunguza idadi ya vijana ambao hawana jambo la kufanya mitaani na kupunguza vitendo ya uhalifu ikiwemo ubakaji, wizi na madawa ya kulevya,” alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Wete Hamad Omar
Bakar aliwataka wanafunzi na walimu kukihifadhi kiwanja hicho pindi tu watakapokabidhiwa mara baada ya kukamilika.
"Viwanja hivi vitumike
kuleta mabadiliko kwa watoto wenu na sio kuwafanyia mambo mengine ambayo yatakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa, tunaona namna Serikali inavyochukuwa juhudi za kutosha, ili lengo la kuleta mabadiliko liweze kufikiwa.
Mapema Afisa Mdhamini Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau alieleza kuwa, viwanja hivyo viwe sehemu ya kuunganisha watu wala wasibaguane kwa kuweka makundi, kwani watu wote wana haki ya kushiriki katika michezo.
Mapema mwakilishi kutoka Shirika la Ujerumani Luisa
Scheuber alieleza kuwa, Serikali ya Ujerumani kwa kushirikiana na Serikali ya Zanzibar ipo tayar katika ujenzi wa viwanja ya michezo Unguja na Pemba, hivyo wanatarajia wananchi kuvitumia kwa kuleta mabadiliko.
“Viwanja hivi view chachu ya kuleta mabadiliko
kwenye jamii, kwani michezo ni mazoezi, michezo ni ajira, hivyo sekta ya
michezo tuipe umuhimu mkubwa katika kuleta maendeleo,” alisema.
Nae mwalimu Mkuu wa skuli ya Sekondari Mchangamdogo Maryam Haji Othaman ameishukuru Wizara kwa kushirikiana pamoja na kuona kuwa ipo haja kwa
wanafunzi wao kujengewa kiwanja cha michezo kwa lengo la kuwajengea uwezo katika masuala mbali mbali ya michezo.
Sheha wa shehia ya Mchangamdogo
Asaa Makame Said, ameahidi kukitunza kiwanja hicho wakati watakapokabidhiwa, kwani wanaona jitihada za
Serekali katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo, hivyo ni wajibu wao kuhakikisha kinadumu kwa kuda mrefu.
MWISHO.
Comments
Post a Comment