NA MARYAM NASSOR, PEMBA@@@@
MAHAKAMA
maalum ya kupambana na makosa ya udhalilishaji, Mkoa wa kusini Pemba,
imemuachia huru Abdillah Haji Suleiman (Lowasa) mkaazi Chanjaani wilaya ya Chake
chake, kutokana na ushahidi
uliowasilishwa mahakamani hapo kutomtia hatiani.
Akisoma uwamuzi mdogo,(Ruling) hakimu wa Mahakama hiyo Zired Abdull-kadiri
Msanif, alisema kuwa katika kesi hiyo mahakama ilisikiliza mashahidi wanne na
kielelezo kimoja.
Alisema kuwa, katika mashahidi wote hao, hakuna ushahidi mzuri ambao
unaweza kumtia hatiani mtuhumiwa, hivyo amemuachia huru chini ya kifungu cha 2015 cha sheria nambari 6 ya mwaka 2018.
Alisema kuwa, mshitakiwa huyo, alishtakiwa kwa makosa mawili, likiwemo la kuingilia kinyume na maumbile, ingawa muhanga alipokuwa anatoa
ushahidi wake, hakusema ni lini na wapi aliingiliwa na mtuhumiwa huyo.
Kwa upande wa askari Polisi mpelelezi, alipokuja mahakamani alisema
kuwa, muhanga alibakwa kwenye kishugu cha mawe na nje ya nyumba yao, majira ya
saa 4:00 usiku, ingawa ushahidi huo ni wa kumsaidia tu muhanga, lakini
mwenyewe hakueleza chochote.
Hakimu huyo, alisema kuwa kosa la pili lilikuwa ni kubaka, lakini pia
ushahidi haukujitosheleza, ambapo haunaoneshi, mtoto ni kwa namna gani
alivyobakwa.
‘’Kwa mfano, shahidi nambari mbili, shangazi wa mtoto, aliiambia mahkama
kuwa, yeye alikuwa mtu wa mwisho kuingia ndani, na ndie aliyefunga milango,
hivyo hakusema ni kwa vipi muhanga alitoka nje alikodai kubakwa,’’alisema Hakimu huyo.
‘’Hivyo, kama mlango ulifungwa na shangazi, suali la kujiuliza je mtoto
alitokaje nje usiku huo, wa saa 4:00 ambao unaosemekana ndio wakati aliobakwa,”alihoji
Hakimu.
Hakimu huyo, alifafanua kuwa, hivyo ushahidi uliyokuwepo mbele ya Mahakama
hiyo, hauoneshi kuwa mtuhumiwa ana kosa la kujibu na badala yake, anachia huru.
Awali mtuhumiwa huyo, Abdillah Haji Suleiman ‘Lowasa’ alishtakiwa kwa
makosa mawili, likiwemo la kuingilia kinyume na maumbile na kubaka, ambapo ni kinyume
na kifungu 108 (1) (2) ( e) na 109 (1) vya sheria ya Adhabu sheria namba 6 ya
mwaka 2018 sheria za Zanzibar.
Ilidaiwa mahakamani hapo Oktoba 11 mwaka huu, majira ya saa 4:30 usiku shehia ya Chanjaani
wilaya ya Chake chake, kuwa alimuingilia kimwili mtoto wa kike (15) jambo ambalo ni kosa kisheria.
MWISHO
Comments
Post a Comment