NA ASHA ABDALLA , PEMBA @@@@
MKUU wa wilaya ya Micheweni Mgeni Khatibu Yahya, ame wataka wazazi na walezi, kuwa makini katika kuwalinda watoto ili waweze kuepukana na vitendo vya udhalilishaji, ambavyo vimeshamiri nakuongezeka siku hadi siku.
Hayo aliyasema wakati alipokuwa akikabidhi misaada kwa Mayatima kwaniaba ya Mwenyekiti wa Nuru Foundation Zainab Kombo Shaib, ambae ni Mke wa Makamo wa Kwanza wa Rais wa zanzibar katika Mahafali ya 11 yaliyofanyika Madrassatu _ Nnisai iliopo Machomane Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Alieleza kuwa watoto Mayatima wanatakiwa kutunzwa vizuri na kulelewa kama Watoto wengine bila ya kubaguliwa kwani nao wana haki ya kupata Elimu ili waweze kufarajika katika maisha yao ya kila siku.
"Watoto Mayatima tuwapeni Misaada kwani nawao wanahitaji upendo nafuraha ili weweze kutimiza ndoto zao ambazo wamejiwekea kuwa viongozi wa nchi hapo baadae", alieleza.
Aidha alisema kuwa Wazazi wajitahidi kuwahimiza Watoto wao kwenda Skuli ili waweze kujipatia Elimu nakuondokana na umaskini Nchini.
Hata hivyo aliwaomba akina mama wasijiweke nyuma katika kugombea Uongozi jambo ambalo lina wasababishia kutopewa kipaumbele katika kutoa uamuzi ili waweze kuwatetea Wanawake wenzao.
"Tunamuona Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanazania ambae ni Dk. Samia Suliuhu Hassan anavoiongoza Nchi nakuwatetea wanawake wenzake juu yasuala zima la maendelo", alisema.
Kwa upande wake Katibu wa taasisi ya Nuru Foundation Zanzibar , iliyopo Gombani Biubwa Yahya Othman alisema kuwa nivyema wananchi wajitolee katika kutoa misaada kuwapa mayatima kwani kufanya hivo ni kwaajili ya Allah SWT na malipo yake watakwenda yaona kesho Akhera.
Nae Mwalimu kutoka Madrast_Nnisai Bimkubwa Habibu Sultan alisema kuwa Wazazi wawe karibu na Watoto wao ili kuwafahamisha kuhusu Udhalilishaji wa Watoto ulivo zidi kuenea.
"Watoto wanadanganywa ni watu kwa kuwapa Pipi au kitu chochote ili watimize lengo lao ambalo wamejiwekea la kuwadhalilisha watoto wetu , " alieleza .
Nae mtoa nasaha kutoka Madrasatu -Nnisai Maryam Juma Hatibu alisema kuwa ni jambo zuri kupewa misaada Mayatima wale wote waliondokewa nawazazi wao kwani mtu hajui muda gani yeye ataondoka kwa sabubu kifo kitamgusa kila binadamu.
"Tutoweni kile ambacho tumeruzukiwa na Allah SWT kwani hivyo vyote Allah ana habari navyo kama tumeviweka kwenye kibubu au benki" alifafanua
Aidha alisema kuwa kila mwenye uwezo wakutowa na akafanya ubakhili kwa kuwapa misaada Mayatima kwa ajili ya Allah huyo anajifanyia nafsi yake.
Nae msoma Risala kutoka Mdrassa hiyo Khadijja Muhammed Mussa alisema kuwa Mahafali hayo yametayarishwa na Kamati ya Wanawake kutoka Madarassat -Nnisai ambayo ilianzisha mfuko wa Mayatima kwa kuwapa sare na vifaa ambavyo vitawasaidia katika masomo yao mwaka ujao.
Hata hivyo alieleza kuwa changa moto kubwa inayojitokeza ni pale wanapotowa misaada hiyo kwa mayatima kuwa niwengi mfuko wao ukawa haukidhi haja .
Mfuko huo ulianzishwa Mwaka 2013 wakiwa namayatima 16 hadi kufikia mwaka huu wametowa kwa mayatima 100 Wakiwa Wanawake ni 47 na Wanaume 53.
MWISHO
Comments
Post a Comment