Na Nafda
Hindi, Zanzibar
Wanawake wametakiwa kujiamini na Kuwa na misimamo imara yenye lengo
la kuleta mabadiliko katika nchi.
Hayo yamesemwa na Dk. Mzuri Issa
Ali wakati akizungumza na wanawake wenye kutia nia kugombea nafasi za Uongozi kutoka vyama mbalimbali vya siasa katika hafla iliofanyika huko Tunguu Wilaya ya
Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Dk.Mzuri amesema wanawake wasirudi nyuma na kubabaishawa na maneno ya baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya wanawake kwa kuwakatisha
tama na kuwaekea vikwazo mbalimbali ili wasiweze kutimiza adhma yao hiyo.
Amesema utafi uliofanywa kisayansi wanawake wanauwezo wa kufanya
mambo mengi kwa wakati mmoja ikilinganisha na wanaume hivyo wanawake waitumie fursahiyo ili kufikia malengo yao.
Naye Mwakilishi mstaafu wa Jimbo la Magomeni Bi Hafsa Said amesema katika kupigania nafasi ya Uongozi alikutana na vikwazo mbalimbali lakini sijambo ambalo lilimkatisha tamaa bali alipambana na hatimae kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka kumi.
Bi Hafsa amesema jambo ambalo lilimfanya kudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi chote hicho ni kujiamini
,kujiheshimu pamoja na mashirikiano na wananchi bila kujali rangi, dini,
kabila wala kujali itikadi zao za kisiasa bali alihudumia watu wa aina zote.
“Mimi
sikujali watu wachama changu tu kwa sababu hata wananchi wa chama cha
upinzani walinipigia kura kwa hiyo wote ni wananchi wangu na maendeleo niliyaleta kwa wote,
na ni kauunda kamati ya sheha nikashirikisha watu wa chamac hangu cha CCM na chama cha
Upinzani tukafanyakazi” BiHapsa.
Nae Kiongozi wa Diniya Kiislam Ukhti Amina Salum Khalfan amesema dini ya kiislam haijakataza mwanamke kuwa kiongozi bali baadhi ya watu hutumia kipengele
cha dini kwa lengo la kuwakandamiza wanawake kwa malengo yao binafsi.
“Aya ya mwanzo katika kitabu kitukufu cha (Qur an) ilimfikia Bibi Khadija ambae alikuwa mke wa bwana Mtume Muhammad (S.A.W) kama vile Suratul Mujadila na Nnisai ni mfano dhahir uliotumika kuonesha mwanamke ni kiongozi , hata masahaba waliambiwa wachukuwe Elimu (kusoma) kwa bibiAysha (R.A.), Siasa isiwe sababuya kunyoosheana vidole “,alisema UkhtiAmina.
Nao baadhi ya wanawake watia nia ya kugombea nafasi za Uongozi wamesema watasimamai mara kuondosha hofu na kuhakikisha wanagombea nafasi za Uongozi kuanzia jimbo hadi Taifa kwa lengo la kuleta mabadiliko katika Taifa hili.
Comments
Post a Comment