NA HAJI NASSSOR, PEMBA@@@@
WANANCHI 1876, wakiwemo wanawake
1,122 na wanaume 750, kutoka shehia za wilaya ya Chake chake Pemba, wengi wao
wakiwa watu wenye ulemavu, wanatarajiwa kufikiwa na taaluma ya kujikomboa
kiuchumi, kupitia mpango wa kuweka akiba.
Watu hao,
watawezeshwa kupitia vikundi maalum vitakavyoanzishwa katika kila shehia ya
wilaya hiyo, ambapo kila kikundi, kitakuwa na wastani wa wanachama kati ya 25
hadi 30.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi, Msaidizi afisa mradi wa kijaluba Mohamed Salim
Khamis, alisema watu hao wanatokea kwenye vikundi 72, ambavyo vyote
vitawezeshwa kimafunzo.
Alieleza
kuwa, vikundi hivyo baada ya kuanzishwa kitaalamu namna ya uwekaji akiba, kisha
vitapewa elimu ya ujasiriamali, pamoja na kuunganishwa na taasisi za kifedha.
Alifafanua kuwa,
mradi huo unakuja kuondoa dhana kuwa watu wenye ulemavu hawezi, badala yake
unakuja kuwawezesha, kuanzia mafunzo na kimbinu.
Alifahamisha
kuwa mradi huo, utakuja kuionesha jamii namna ambavyo watu wenye ulemavu,
wanaweza kupata mafanikio, kupitia fedha zao walioziweka kama akiba.
Alisema,
fedha hizo watafundishwa namna ya kuziendeleza kwa ajili ya kujikwamua na
umaskini, kupitia vikundi vya uzalishaji watakavyoviendesha wenyewe.
‘’Mradi huu
ambao utajumuisha pia watu wasiokuwa na ulemavu, watafanyakazi kwa pamoja, na
lengo ni kuona kuwa watu hao, wanaweza kujikomboa,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine, Msaidizi huyo afisa mradi huo, alifafanua kuwa, pamoja na kuwawezesha
kiuchumi watu wenye ulemavu, lakini pia wataongezewa, uwelewa juu ya uongozi.
‘’Kwa mfano,
katika nafasi sita za uongozi kwenye vikundi hivyo vya kuweka akiba, nafasi nne,
lazima zishikiliwe na watu wenye ulemavu,’’alieleza.
Alisema hilo
linatokana na kwa sasa, kutengwa na jamii, juu ya suala la uongozi, na
kuonekana kama vile hawana hadhi ya kuwa viongozi.
Hata hivyo
alisema, ndani ya vikundi hivyo, kutakuwa na mfuko maalum wa jamii, ambao
utawasaidia pale wanapokumbwa na majanga mbali mbali, katika maisha yao.
Kwa upande
wake, afisa utawala kutoka shirikisho la jumuiya za watu wenye ulemavu
SHIJUWAZA kisiwani Pemba Aisha Abdalla Juma, alisema wamefurahishwa, na ujio wa
mradi huo.
Alieleza
kuwa mradi huo, utakwenda kuwaamsha watu wenye ulemavu, juu nafasi yao katika jamii,
katika kujikwamua na umaskini unaowakabili.
Nae
mwezeshaji wa vikundi vya watu wenye ulemavu ‘CRP’ Fatma Abrahman Ali wa shehia
ya Ole wilaya ya Chake chake, alisema anasimamia vikundi tisa, vyenye wanachama
wastani wa 25 hadi 30 kwa kila kimoja.
Alisema,
katika vikundi hivyo kwa mfano chenye wanachama 30, ni lazima 20 wewe wenye
ulemavu, kwani ndio hasa malengo ya mradi huo.
‘’Kwa saa
tunaendelea na mafunzo sisi waalimu, kisha tutakwenda kwa jamii, kuwahamasisha
namna ya uundaji wa vikundi vya kuweka akiba, ili sasa wapate
kujikomboa,’’alifafanua.
Nae mwalimu
wa vikundi hivyo kutoka ‘SHIJUWAZA’ Fatma Abdalla Issa, alifafanua kuwa, kutokana
na mafunzo waliokwishapatiwa, sasa wako tayari kwenda shehiani.
‘’Tunakwenda
kuvifundisha vikundi jumuishi vya kuweka akiba, ili sasa wapige hatua kwenye
kukua kiuchumi, kwa kule kuanzisha biashara ndogo ndogo hapo baadae,’’alieleza.
Mratibu wa
TAMWA-Pemba Fat-hya Mussa Said, alisema kazi yao kubwa katika mradi huo, ni
kuwaunganisha waandishi wa habari katika mradi huo, ili kutoa habari mbali
mbali.
‘’Sisi kama
TAMWA, tunawajibu wa kupatia haki zao watu wenye ulemavu, na ndio maana
tunafanyakazi kwa karibu na vyombo vya habari, ili sasa kuutangaza mradi na
nafasi ya watu wenye ulemavu, katika kukuza pato lao,’’alieleza.
Mradi wa
Kijaluba, ni jumuishi unaolenga kuwawezesha watu wenye ulemavu kiuchumi, kwa
kule kuwajengea uwezo kuhusu maisha yao na jamii zao.
Mradi huo
unatarajiwa kukuza uwezo wa kundi hilo, samba mba na kujenga mitazamo chanja,
juu ya ushiriki wao, kujiingiza katika shughuli za kujipatia kipato.
Aidha mradi
huo wa ulioanza mwaka 2022, ukitarajiwa kumalizika mwaka 2024, utakwenda
kushughulikia vikwazo vinavyowarudisha nyuma, watu wenye ulemavu.
Kwa sasa
mradi huu, anatekeleza wilaya ya Kusini Unguja na Chake chake kisiwani Pemba,
kama eneo la majaribio, ambapo walengwa wakuu ni watu wenye ulemavu wakiwemo
vijana, watoto kwa asilimia 60 na 40 na watu wengine.
Mwisho
Comments
Post a Comment