NA
HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MADEREVA
na makonda wa gari za abiri kisiwani Pemba, wamewalalamikia abiria, kuendelea
kutoa nauli za zamani, na kuacha nyongeza ya shilingi 100, iliyoongezwa na
serikali mwaka jana.
Walisema, baada ya serikali kuongeza nauli mwaka jana
wastani wa shilingi 100, kutoka nauli za zamani, bado baadhi ya abiria wamekuwa
wazito, kutimiza haja hiyo ya kisheria.
Wakizungumza na mwandishi wa habari mjini Chake chake,
walisema kwa mfano nauli ya kutoka Chake chake hadi Mtambile ni shilingi 1,300,
bado abiria wanalipa kati ya shilingi 1000 hadi shilingi 1,200.
Mmoja kati ya dereva huyo, Mohamed Khamis, anayefanyakazi
barabara ya Chake chake –Mkoani alisema, hata nauli mpya ya shilingi 1,800 kutoka
Chake chake hadi Mkoani, abiria waliowengi wanalipa shilingi 1,500.
‘’Ukiwauliza kuwa mbona hawalipi nauli mpya, anakujibu
kuwa hana chenji, lakini hajui kuwa sisi tunapokwenda sheli kutia mafuta, hilo
jambo hilipo,’’alisema.
Nae dereva Abdalla Omar anayefanakazi Mwambe- Chake
chake alisema, hata nauli ya kutoka Mwambe hadi Mtambile kwa sasa ni shilingi
600, ingawa abiria wanalipa shilingi 500.
‘’Mafuta yapenda na ndio maana serikali, iliamua
kupandisha nauli kidogo, ingawa bado abiria wanalipa kwa nauli ya zamani,’’alilalamika.
Nae dereva anayefanyakazi barabara Chake chake –Wete
Himid Khalfan, anasema wamekuwa wakishambuliana na abiria, ndio baadhi yao,
hulipa nauli kamili mpya.
‘’Tumebandika ndani ya gari zetu nauli mpya
zilizotangaazwa na serikali tokea mwaka jana, lakini bado abiria wanapuuza
nauli hizi na kutulipa za zamani,’’alieleza.
Abiria Aish Mjaka Haji wa Kiwani alisema, sio sahihi
kuwa wanalipa nauli kongwe, bali wanachokifanya baadhi ya makondakta, ni
kuongeza zao za juu.
‘’Kwa mfano nauli kutoka Chake chake hadi Mgagadu ni
shilingi 800, lakini ukiwapa shilingi 1,000 hawarejeshi chenji, na ukiwauliza
wanasema mafuta yamepanda,’’alieleza.
Nae Mwanakhamis Haji Mcha wa Mwambe alisema, kwa sasa
baadhi ya makondakta wanawalipisha nauli ya shilingi 700 kutoka Mwambe hadi
Mtambile, badala ya shilingi 600 ya iliyotangaazwa.
Zuhura Khamis Omar na mwenzake Mwanaisha Kheir Nassor
wanaotumia barabara ya Konde -Chake chake, walisema makondakta katika barabara
yao, nauli zao hazitabiriki.
‘’Abiria wakiwa wengi na gari chache, au kama siku ya kuja
meli hapo nauli hupandishwa na kuivuuka ile elekezi ya serikali,’’alisema
Zuhura.
Katibu wa Jumuiya ya wamiliki wa gari za mizigo na abiria
mkoa wa kusini Pemba, ‘PESTA’ Hafidh Mbarka Salum, amerejea kauli yake ya
kuwataka wananchi, wanaonyanyaswa na makondakta kuwaripoti kwao.
Aidha, amesema dereva ambaye atabainika kukiuka maagizo
ya serikali, kwa makusudi, ‘PESTA’ asitegemee kuwa itasimama kumtetea, na
badala yake sheria, itachukua nafasi yake.
Katika eneo jengine Katibu huyo, amewataka abiria
kukamilisha nauli iliyowekwa na serikali, na sio nyingineyo, kwani gari hizo,
zinatumia gharama kubwa hadi kuweko barabarani.
Mwezi Septemba mwaka 2022, serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, ilitangaaza kupandisha nauli mpya kwa gari za abiria, wastani wa
ongezeko la shilingi 100, kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta, ambapo mara
mwisho kutangaazwa nauli, mpya ilikuwa ni mwaka 2019.
Nauli mpya iliyotaangazwa mwaka jana,
ilikuwa kwa daladala zenye umbali wa kilomita 1 hadi 12, imepanda kutoka shilingi
400 hadi shilingi 500.
Ambapo kwa umbali wa kilomita 19 hadi 21,
nauli imepanda kutoka shilingi 800 hadi shilingi 900, wakati kwa zenye umbali
mfupi wa kilomita 1 hadi kilomita 14, imepanda kutoka shilingi 500 hadi shilingi
600 na kwa umbali mrefu wa kilomita 60 hadi 70 nauli imepanda kutoka shilingi
2,300 hadi shilingi 2,500.
Mwisho
Comments
Post a Comment