|
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
KUNDI
la watu wenye uziwi kisiwani Pemba, limetoa raia kwa mamla husika, kuacha
kuwachanganya na wengine bila ya wakalimani, wanapowafikishia taaluma za
kitaifa.
Wanasema, wamekuwa
wakiishia kucheka na kupiga kofi, kwenye vikao na mikutano ya kutoa elimu, kwa
kule kukosekana kwa mkalimani.
Wameonya kuwa, kwa mfano
kwenye elimu ya ugonjwa wa Uviko19, samba mba na ujio wa chanjo yake,
hawakutengewa mikutano yao ya kielimu, wakiwa na wakalimani.
Asha Suleiman, mkalini
anayetambulika kisiwani Pemba, anasema hakuwahi kushirikishwa na wizara husika,
juu ya kuwakusanya viziwi kupatiwa elimu hiyo.
Hilo, anasema lilisababisha
kundi la viziwi kukosa taarifa za sahihi za chanjo ya Uviko19, jambo ambalo
liliwakoseha kufanya uamuzi sahihi.
‘’Shughuli kadhaa za
kitaifa huwa nashirikishwa na kundi la watu wangu, lakini kwenye elimu ya
chanjo ya Uviko19, hautukuwahi kuitwa,’’analalamika.
WANATOA
RAIA GANI KWA SERIKALI
Anasema, kama mikataba
iliyosainiwa ina malengo ya kweli na kundi hilo, wasisite kuwashirikisha katika
vikao na mikutano maalum ya elimu.
‘’Inawezekana kundi la
viziwi lilishirikishwa, lakini halikupata ushirikishwaji, maana walichanganywa
na wengine na wao wakaishia kupiga kofi,’’anasema.
Anaona njia iliyotumiwa na
wizara ya Afya ya kuvamia makundi ya watu na kuwapa elimu, katika vijijini pasi
na kuzingawatiwa kwa viziwi, haikuwasaidia.
Mohamed Khamis Shehe
Mratibu wa Chama cha Viziwi Zanzibar ‘CHAVIZA’ wilaya ya Chake chake, anasema
njia rahisi ni kuwashirikisha.
Anaziomba mamla husika, kuvitumia vyama vyao
moja kwa moja, wanapotaka kutoa elimu ya kitaifa, na sio kuwachanganya na
makundi mengine.
‘’Tunaweza kuchangaywa na
makundi mengine, lakini lazima waandaji wawasiliane na mkalimani
wetu,’’anashauri.
Asha Haji Hassan wa kisiwa
cha Makoongwe wilaya ya Mkoani, anasema hata watoa elimu ngazi ya vijiji ‘CHV’
ni vyema wakawezeshwa, ili kuwafikia.
‘’Kwa mfano CHV’ wamekuwa
wakijitahidi kusambaaza elimu ya chanjo ya Uviko19, lakini tunaposhiriki na
sisi ili tuhapati elimu, huwa vigumu maana hawajui lugha ya alama,’’anasema.
Mzazi mwenye vijana watatu
wenye uziwi mkaazi wa Kisiwa Panza wilayani humo, anasema alilazimika kuwapatia
elimu ya juu juu vijana wake.
‘’Ni kweli kundi la wenzetu
wenye uziwi, halikupata elimu ya moja kwa moja ya chanjo ya ugonjwa wa Uviko19,
na ilitulazimu sisi wazazi tuwaelekeze,’’anasema.
Mjumbe wa Kamati tendaji ya
Jumuiaya ya wanawake wenye Ulemavy Zanzibar ‘JUWAUZA’ Hidaya Mjaka Ali, anasema,
njia ya wenzao wenye uziwi kufikiwa ni kuendesha mafunzo chini ya mkalimani.
‘’Wenzetu wenye uziwi ni
tofauti na sisi watu wenye ulemavu wa viungo, albinazim hawa wanawakalimani
wao, kila kwenye vikao wawepo,’’anashauri.
Mratibu wa
Baraza la Taifa la watu wenye Ulemavu Zanzibar ofisi ya Pemba, Mashavu Juma
Mabrouk, anasema, iwapo taarifa za kitaifa zitakosa wakalimani, kundi la viziwi
litaendelea kuzikosa.
Anakiri kuwa,
ile elimu rasmi ya Uviko19 na hasa inayoambatana chanjo, kutoka kwa wataalamu
wa afya, watu wenye uziwi imefika kwa kundi dogo mno.
WIZARA YA AFYA
Afisa
Mdhamini wizara ya Afya Pemba Khamis Bilali Ali, anasema walichokifanya ni
kukutana na wakuu wa Jumuiya za watu wenye ulemavu, ili kuwapa elimu.
‘’Naamini
katika elimu ya kujikinga na Uviko19, hakuna mtu aliyeachwa nyuma, na hasa
wenzetu wa makundi maalum, tulikuwa na mkakati malum,’’anasema.
Anasema,
jambo ambalo linawezekana kuwa, wale wakuu wa jumuiya za watu wenye ulemavu,
hawakuwashushia elimu hiyo, wenzao wenye ulemavu, licha ya wizara kukutana nao.
Eneo jingine,
hadi leo hii wameweka utamaduni wa kuyataka makundi yote, yawaalike wataalamu
wa afya popote walipo, ili wapatiwe elimu ya Uviko19.
‘’Inawezekana,
kwa mfano, wenye uziwi wapo kisiwani na kufika mjini ni shida, kwa mujibu wa
mazingira yao, sasa wawasiliane na maafisa wetu wa afya wa wilaya na watafuatwa
walipo,’’anasema.
Ingawa upande
mmoja, Mratibu wa kitengo cha elimu ya Chanjo cha wizara hiyo Pemba Bakar
Hamad, anasema utaratibu wao ulikuwa, ni kuyaenda makundi kuyapa elimu.
‘’Kwa mfano
tunakwenda kwa vikosi vya ulinzi na usalama, wanafunzi wa skuli, vyuo vikuu,
waandishi wa habari, wakulima, watumishi wa umma na viongozi wa dini,’’anasema.
Hivyo anasema
hakumbuki kuwa, na mpango maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa uziwi peke
yao, bali walikuwa na mikutano ya elimu kwa makundi mchanganyiko.
Anakiri kuwa,
kwa Pemba, hakuna hata kundi moja ambalo halikufikiwa na elimu ya Chanjo ya
Ukivo 19, ingawa akaweka wazi kuwa, kama litajipanga kundi la watu wenye viziwi
wakiwa na mkalimani wao wako tayari.
NINI
ATHARI YAKE?
Himid Mcha
Khamis kiziwi mkaazi wa kisiwa kidogo cha Fundo wilaya ya Wete, anasema ni kuwa
rahisi wao kushambuliwa na uogonjwa wa Corona au mengine ya mfumo wa hewa.
Aisha Haji
Makame wa kisiwa cha Makoongwe, anasema wamevunjiwa haki zao ambazo zimeainishwa
kwenye mikataba na sheria mbali mbali.
Afisa
Mdhamini wizara ya Afya Khamis Bilali Ali, anasema moja ni kukumbwa na
maambukizo kwa wepesi, kama hawakuwa na elimu ya kujikinga.
Afisa wa
Chama cha Viziwi wilaya ya Chake chake Mohamed Khamis Shehe, anasema ni
kuwaweka wao katika msingi wa kukumbwa na magonjwa.
MIKATABA
INAVYOHESHIMU HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU
Mkataba
wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu,
ambao Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliusaini, Machi mwaka 2007
na kuthibithisha mwaka 2009, unalazimisha huduma za afya kwa watu wenye ulemavu.
Ibara ya 25, inasisitiza nchi wanawachama, zitumbue
kuwa, watu wenye ulemavu wanayo haki ya kunufaika kwa
kiwango cha juu, huduma za afya bila ya ubaguzi wowote.
Mkataba ukafafanua, nchi husika zitachukua hatua zinazostahiki, kuhakikisha
watu wenye ulemavu wanapata huduma bora za afya.
‘’Nchi wanachama, zitatoa huduma za afya, zinazohitajika kwa watu
wenye ulemavu, hasa kutokana na aina ya ulemavu wao, yakiwemo maeneo ya
vijijini,’’umefafanua Mkataba huo.
Ukaongeza kuwa, nchi hizo zitawataka wataalamu wa afya, kutoa
huduma za kiwango sawa, kwa watu wenye ulemavu, kama zinavyotolewa kwa watu
wengine, ikiwa ni pamoja na misingi ya kutoa ridhaa kwa uhuru na ufahamu wa
kutosha.
Mwaka
1983 hadi 1992 hatua mbali mbali zilichukuliwa, ikiwani pamoja na maamuzi ya
mwisho ya Umoja wa Mataifa, kuitangaza Disemba 3 ya kila mwaka, iwe ni siku ya kimataifa
ya watu wenye ulemavu duniani.
Ambapo
siku hiyo pamoja na mambo mengine, kundi la watu wenye ulemavu hujadili,
mafanikio na changamoto zao, zikiwemo huduma za afya.
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania nayo, iliunda Mkakati wa Kitaifa wa Ujumuishi wa mwaka
2010 hadi 2015 na sera ya taifa ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004, ukitaja
uhitaji wa lazima wa huduma za afya wa watu wenye ulemavu.
Ipo sera ya kitaifa ya watu
wenye ulemavu ya mwaka 2018 kwa upande wa Zanzibar, ambayo nayo kwenye Ibara ya
20, ikasisitiza uimarishwaji wa upatikanaji huduma bora na endelevu kwa watu
hao.
Kuhusiana na hatua za
kisheria, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilitunga sheria ya Watu
wenye Ulemavu ya mwaka 2010, ambapo ilikuja kuharakisha pia suala la huduma
bora za afya.
Zanzibar, ambayo ilikuwa na
Sheria ya Watu wenye Ulemavu, nambari 9 ya mwaka 2006, ambayo sasa imefutwa na
kuwa na sheria mpya nambari 8 ya mwaka 2022.
Kifungu
cha 28 (1) (c) cha sheria hiyo, kimeanisha haki ya kupata huduma za afya kwa
watu wenye ulemavu, ikiwemo matibabu, matengenezo au marekebisho yanayohusiana
na aina ya ulemavu wao.
Tanzania bara pia iliunda
Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya ambao unatoa mwongozo wa ufikiaji wa huduma za
afya kwa makundi yote yakiwemo ya watu wenye ulemavu kama viziwi.
Kwa upande wa Zanzibar,
kulikuwa na Mpango Mkakati wa sekta ya afya wa miaka tisa, ambao uliishia mwaka
2019, wenyewe ulitaja hatua za kuchukuliwa, ili kuwakinga na utapia mlo
wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.
UGONJWA
WA CORONA NA CHANJO YAKE
Wakati hayo yakifanyika,
Machi 11, 2020, Shirika la Afya Ulimwenguni ‘WHO’ iliiratibisha rasmi ugonjwa COVID-19
kama janga la dunia.
Hii baada ya ugonjwa huo wa mlipuko wa kuenea
kwa kasi duniani kote, ambao huenea kwa haraka katika mataifa na mabara mbali mbali.
Aidha WHO iligundua kuwa, watu 4,291 walikuwa wameshaaga
dunia na maelfu zaidi walikuwa wamelazwa hospitalini kwa muda mfupi.
Baada ya janga hilo, wataalamu wa afya waliibuka na
chanjo za aina mbali mbali, ambazo baada ya majaribio zikabainika kuwa,
zinaweza kuwa kinga.
Na hapo sasa wizara ya Afya Zanzibar kwa upande nwake, ilidhamiria
hadi ikiingia mwaka 2023 iwe wazanzibari 70 kila 100 wameshapata chanjo za
Corona.
Huku hayo yakipangwa, Shirika la Afya
Duniani (WHO) lilisema Julai 27, mwaka 2022 kuwa hadi kufikia Julai 25, 2022
jumla ya dozi bilioni 12.24 za chanjo ya Covid-19 zilitolewa duniani kote.
Utoaji wa
chanjo dhidi ya Covid-19 hapa nchini ulizinduliwa Julai 28, mwaka 2021 na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambapo chanjo aina ya
Pfizer, Moderna, Sinopharm, Sinovac na Jansen ziliidhinishwa kutumika.
TAKWIMU YA WALIOCHANJA
Katika kipindi cha tarehe
29 Oktoba hadi 02 Disemba, 2022, jumla ya visa vipya 442 vimethibitika kuwa na
maambukizi ya Uviko19.
Imebainika kuwa, idadi hii
ni kubwa ukilinganisha na takwimu za mwezi uliopita ambapo kulikuwa na visa
vipya 272, sawa na ongezeko la asilimia 62.5.
Hadi kufikia tarehe 02
Desemba 2022, jumla ya watu milioni 29,123,387 kati ya walengwa 30,740,928
ambao ni sawa na asilimia 94.7 wamepata dozi kamili ya chanjo ya UVIKO- 19.
Mwisho
Comments
Post a Comment