Na Mwandishi Wetu,
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya
Weka Jiji Safi Limited (WEJISA ) wameungana na wanawake wenzao kusheherekea sikujui ya wanawake inayoadhimishwa Machi 8 Kila mwaka.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bi.Nuru Hassan amesema kuwa, maadhimisho hayo yanaleta chachu ya Maendeleo kwa wanawake Kwa sababu ya Rais Samia Suluhu Hassan kuonyesha njia ya kuwa wanawake tunaweza.
Amesema kuwa Rais Samia ameweza kuweka mazingira mazuri ya wanawake kujituma na kufanya kazi Kwa bidii bila ya kuwa wategemezi , jambo ambalo limeongeza uchapakazi Kwa jinsia hiyo.
"Rais wetu Samia tunamuunga mkono kwa sababu nafasi aliyonayo amesaidia kuongeza mwamko kwa wanawake kufanya kazi na wale ambao walikua hawana kazi na kutafuta shughuli zozote ili waweze kujiondoa kwenye utegemezi," alisema Nuru.
Alisema kuwa, kampuni ya WEJISA itaendelea kushirikiana na Serikali bega kwa bega na ndo maana leo tumekuja hapa kusheherekea pamoja na kujifunza mengi kwa Wafanyakazi wetu Wanawake" alisema Nuru Seif Hassan
Aidha, amesema kuwa amepata faraja kujumuika na Wanawake hao kwani wamekuwa chachu ya Maendeleo ya Kampuni hiyo.
Wanawake hao wa WEJISA wanatoka vitengo mbalimbali ikiwemo wanaosafisha maeneo ya Jiji, ikiwemo ufagiaji, ukusanyaji wa taka na usafi wa mazingira.
Lengo la tukio hilo ni kupeana moyo kama Wanawake katika kuamua mambo katika kufanikisha utendaji bora wa kazi.
Kwa upande wake Patricia Kimelemeta Mwandishi Kimara wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Mtoto Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alitoa mada ya malezi na makuzi Kwa watoto katika tukio hilo la kusheherekea siku ya Wanawake, ambapo alisema kuwa, licha ya wanawake kufanya Kazi mbalimbali lakini pia tunapaswa kutimiza wajibu Kwa watoto wetu katika masuala ya Malezi na makuzi.
"Baadhi ya wanawake wanashindwa kutimiza wajibu wao Kwa watoto Kwa kisingzio cha kufanya Kazi, jambo ambalo limesababiaha watoto kukosa mapenzi na wazazi wao badala yake kulelewa na ndugu au jamii.
" Hivyo basi wakati kunasheherekea madhimisho haya tunapaswa kujua kuwa sisi ni mama, wazazi na walezi, hata kama tunafanya kazi lakini pia tunapaswa kutimiza wajibu wetu kama wazazi na walez", amesema Kimelemeta.
Ameongeza kuwa, watoto wenye umri kuanzia sifuri hadi miaka minane wanahitaji uangalifu wa hili ya juu na wazazi, walezi au jamii inayowazhnguka Ili waweze kukua Katika hali ya utimilifu.
Amesema kuwa, katika.maadhimisho haya wanawake wanapaswa kukumbushana na kuhimizana Ili Kila mmoja anapotoka hapa abadilikw na kujiona kuwa ana wajibu wa kumlinda, na kumtetea mtoto wake au aliyepo kwenye jamii anayoishi.
Amesema kuwa, Serikali inatekeleza mradi wa Malezi, makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) ikiwa ni pamoja na kuwataka watoto wake Katika hali ya utimilifu, wasomw katika mazingira bora na jamii ihusike Katika ulinzi na usalama wa mtoto.
Hata hivyo, baadhi ya wanawake wa Kampuni hiyo wameushukuru uongozi wa kampuni hiyo kwani imekuwa mkombozi kwao na wamekuwa wakifanya kazi moyo.
"Mie nina familia, nikitoka nyumbani naandaa kabisa chakula kwa wanangu.
Aidha, amewataka Wanawake kuzingatia sheria za Usalama barabarani kwani wamekuwa wakishuhudia matukio mengi, ikiwemo wao kugongwa.' Alisema Bi. Asha Salum.
Kwa upande wake. Sharifa Magombeka amesema kuwa, anafanya kazi ya kuzoa taka ilikupata kipato chake halali,
"Mwanamke ni kujitambua, nafanya kazi yangu ya kuzoa taka hii kupata kipato kihalali, tunamshuru Mhe Rais kuendelea kueka mazingira ya ufanyaji kazi,
Leo tumejumuika hapa tumepata elimu, lakini pia tumefuraia pamoja" alisema Sharifa.
Mwisho.
Comments
Post a Comment