Na Mwandishi Wetu::::::
WAPO baadhi ya watu huwatumia watu wenye ulemavu kama ni mtaji wa kuwapatia kipato hali ambayo imechangia kuwepo kwa idadi ya ombaomba kwa watu wenyeulemavu Zanzibar.
Kwa kuliona hilo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewaonya wenye tabia hiyo ya kuwatumia watu wenyeulemavu kwa shughuli zao binafsi ikiwemo za ombaomba watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na idara maalum SMZ Masoud Ali Mohamed, anasema serikali inafahamu kuwepo kwa watu wanaowatumiya watu wenye ulemavu kwa ajili ya kujipatia kipato binafsi.
Waziri huyo anasema serikali inafahamu kuwepo kwa matukio ya aina hiyo ambapo tayari baadhi ya watu wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kuwatumiya watu wenye ulemavu.
Anasema watu hao waliokamatwa wamekutwa wakiwahifadhi watu wenyeulemavu katika nyumba moja visiwani Zanzibar na huwasambaza katika maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar kwa ajili ya kuomba ili kupata fedha.
Anasema jumla ya watu watano wamekamatwa katika eneo la Mboriborini Unguja katika nyumba moja wakiwa wamewaweka watu wenye ulemavu kwa ajili ya kuwatumiya kwa shughuli za ombaomba katika maeneo mbalimbali ya mjini.
Anasema kwa mujibu wa sheria ya watu wenye ulemavu namba nane ya mwaka 2022 ni makosa kuwatumiya watu wenye ulemavu kwa ajili ya shughuli binafsi ikiwemo kuwapa majina mabaya na kuwatumiya kwa maslahi yao.
‘’Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha inaitumiya sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2022 ambayo imewabana watu wanaowatumiya watu wenyeulemavu kwa maslahi yao binafsi na kujipatia kipato ikiwemo shughuli za ombaomba’’anasema.
Aidha anasema matukio ya ombaomba sio silka na mila za utamaduni wa wananchi wa Zanzibar kwa hivyo vitendo hivyo vinatakiwa vidhibitiwe.
Anasema katika kudhibiti kitendo cha ombaomba hasa kwa watu wenyeulemavu serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kufanya shughuli mbalimbali za ujasirimali kwa lengo la kuepukana na matukio hayo.
‘’Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar tutahakikisha tunapambana na matukio ya ombaomba katika maeneo mbalimbali ambapo tumejipanga kuona kwamba watu wenye ulemavu tunawawezesha katika vikundi mbalimbali kukomesha matukio hayo’’alisema.
Katibu wa baraza la Taifa la watu wenyeulemavu Zanzibar, Ussi Debe anasema baadhi ya watu wanawatumia watu wenyeulemavu kama ni mtaji jambo ambalo si sahihi na linavunja utu na heshima kwa watu wenyeulemavu.
“Utawaona watu wenyeulemavu hasa wale wenye umri mkubwa au watoto wanaongozwa kupitishwa katika maduka wakiomba pesa kwa kweli kitendo hiki kinaniskitisha sana maana huwafanya kama ni mtaji wao”anasema.
Aidha Mkurugenzi huyo anasema ulemavu usiwe kigezo cha kutumikishwa au kudhalilishwa kwa sababu wanahaki ya kutafuta kipato kwa njia zinazokubalika kama walivyo watu wingine.
Mwenyekiti wa shirikisho la watu wenyeulemavu Zanzibar, Mwandawa khamis vitendo vya udhalilishaji au utumikishwajwi wa watu wenyeulemavu vinahitaji kupigwa vita na kila mmoja.
Anasema kuenelea kwa vitendo vya Ombaomba kwa watu wenyeulemavu kunasababisha kuongezeka kwa vitendo vya udhalilishaji kwa watu hao hivyo ni vyema vikakomeshwa.
Aidha anasema watu wenyeulemavu wanahitaji kuwezeshwa kwa kupatiwa mititaji kwa ajili ya kufanya biashara na kumudu gharama za maisha.
Comments
Post a Comment