NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
KAMISAA wa sensa ya watu na makaazi
Balozi, Mohamed Haji Hamza, amesema baada ya matokeo ya sensa kutoka,
anavitegemea sana vyombo vya habari, kuielezea jamii umuhimu wake.
Kamisaa huyo
aliyasema hayo Machi 7, 2023 ukumbi wa kiwanda cha Mafuta Makonyo Wawi wilaya
ya Chake chake, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye mafunzo ya
matumizi ya takwimu za sensa za mwaka 2022.
Alisema, kwa
vile jukumu moja wapo la vyombo vya habari ni kuelimisha, hivyo ni wakati sasa
kutumia wajibu huo, kuwaeleza wananchi umuhimu wa takwimu hizo.
Mapema
Mtakwimu mkuu wa serikali Zanzibar Salum Kassim Ali, alisema ili nchi ipange
mikakati na mipango thabiti ya maendeleo, takwimu ni jambo la msingi.
‘’Bila ya
takwimu sahihi na kisha kutumika vyema, hakuna jambo ambalo litafanikiwa, liwe
la maendeleo ya haraka au ya muda mrefu,’’alieleza.
Kaimu
Mtakwimu mkuu ofisi ya Pemba, Said Mohamed alisema serikali imetumia gharama
kubwa, kufanikisha sensa ya watu na makaazi, hivyo ni lazima sasa zitumike.
Hata hivyo,
alisema waandishi wa habari ndio watumiaji wakuu wa takwimu, kwa kule
kuwaelimisha wananchi, juu ya changamoto au mafanikio ya taifa.
Wakizungumza
kwenye mafunzo waandishi wa habari akiwemo Mchanga Haroub Shehe, alisema ni
vyema waandishi watakaozitumia takwimu, wawe makini.
Nae Mkuu wa
Shirika la Magazeti ya serikali Pemba Bakar Mussa, alisema matumizi ya takwimu
ni jambo zuri, wakati waandishi wanapotayarisha habari, makala na vipindi.
Nae Meneja
wa redio Jamii Micheweni Ali Massoud Kombo, alisema wakati umefika kwa
watendaji wa ofisi hiyo, kuwa karibu na vyombo vya habari.
Akifunga
mafunzo hayo, Mdhamini Tume ya Mipango Pemba Khamis Issa, alisema kazi
zinazofanywa na waandishi ni kubwa, hivyo ni wakati kuzitumia takwimu za sensa.
Kwa mujibu
wa sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022, idadi ya watanzania wote ni milioni 61,741,120, wanaume wakiwa 30,053,130 na wanawake ni 31,687,990, ambapo kwa Zanzibar
imebainika kuwepo watu 1,889,773,
kati ya hao wanaume 915, 492 na
wanawake 974,281.
Mwisho
Comments
Post a Comment