HABIBA ZARALI, PEMBA
WAANDISHI wa habari nchini, wametakiwa
kuacha kuandika habari kimazowea na
badala yake wajikite kuandika habari za uchunguzi (Investigative
Journalism), ili kuweza kufichua maovu na kuisaidia jamii, kupata matokeo chanya.
Kauli hiyo
imetolewa Septemba 09, mwaka 2022 na Mkufunzi Mwandamizi kutoka shirika la Intenews Tanzania Alakok Mayombo
alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu ya uandishi wa habari za uchunguuzi, yaliyoendeshwa na shirika hilo kwa njia ya kielektroniki ya zoom, uliowashirikisha
waandishi wa vyombo mbalimbali vya Tanzania bara na visiwani.
Alisema
waandishi wa habari walio wengi
hawaandiki habari za uchunguzi ingawa ni eneo muhimu lenye nguvu katika
kuasaidia kufanya maamuzi mazito na
kuleta mafanikio ya haraka.
Alifahamisha
kuwa ni vyema kwa waandishi wa habari kuwa habunifu kwani habari hizo zinahusu
mtu mmoja mmoja na wakati mwengine serikali hivyo kila mmoja anauwezo wa
kujikita katika eneo hilo.
“Nguvu za
habari za uchunguzi ni kubwa na mara nyingi habari hizi zinakuwa zimejificha na
waandishi hamutakiwi kulala fichueni kwa malengo mema”,alisema.
Kwa upande
wake mkufunzi kutoka shirika la Intenews Erick Kabendera alisema mbali na
changamoto nyingi walizonazo waandishi wa habari bado wana jukumu la kuwa na
moyo wa kuandika habari za uchunguzi.
Alisema
kusudio la habari za uchunguzi si la kumripua mtu isipokuwani kuonesha uhalisia
wa jambo na kuweza kuleta matokeo yenye faida kwa jamii na nchi nzima.
“Waandisi
tusianagalie tu kuandika stori kwa ajili ya kesho pekee na hizi za uchunguzi
lazima tuhakikishe tunaziandika kwa lengo jema kabisa”,alifahamisha.
Katika
hatuwa nyengine kabendera alishauri waandishi wa habari hizo kuwa na uwelewa wa
kitaalamu ,waweze kujifunza , wafanye uchunguzi kwa kina (research), waweze kuwa
na vyanzo vingi vya habari, vyanzo nyaraka ili kupata habari zenye ukweli .
“huwezi kuwa
mwandishi mzuri wa uchunguzi kama kama hutokuwa na moyo wa ustahamilivu na
kuweza siri ya kile unachokifanya,hivyo ni lazima kila mmoja kutimiza wajibu
wake na sio kuleta woga”alisema.
Akizungumza
na waandishi hao baada ya kumaliza mkutano huo mkufunzi mkuu wa Internews
Temigunga Mahondo alisisitiza kuzingatia maadili, na kutenda haki kwa waandishi
wa habari ili kujenga uwajibikaji unaofaa kwa jamii.
Alisema
iwapo waandishi wataandika habari hizo za uchunguzi zitasaidia kuondowa maovu
ikiwemo ya rushwa,udhalilishaji na maovu mengine mengi yanayoikabili jamii na
nchi kwa ujumla.
“Licha ya
kuwa kazi hizi ni hatari lakini kama waandishi watakubali kunyamazishwa na
wasipofichua basi uwajibikaji hautokuwepo”,alieleza.
Wakitowa
shukrani zao kwa shirika la Intanews washiririki wa mafunzo hayo walisema mafunzo
hayo ni muhimu kwani kufanikiwa kuandikwa kwa habari hizo ni mafanikio ya
kuleta matokeo mazuri hasa kwa jamii isiyo na sauti.
Hata hivyo
waliliomba shirika la Internews kuendelea kutowa mafunzo mbali mbali kwa
waandishi wa habari kwani kunawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Mwisho.
Comments
Post a Comment