NA HAJI NASSOR, PEMBA:::
WATOTO watano wa familia moja wakaazi wa kijiji cha Mtega Wawi Wilaya ya Chake chake Pemba, wamesalimika kufa baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuteketea kwa moto na kuunguza vitu vyote vilivyo kuwemo ndani.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa , wameona moshi mkubwa ukitokea kwenye mapaaa ya nyumba hiyo huku watoto hao , wakiwa nje ya nyumba yao wakipga kelele kuashiria kuomba msaada.
Mmoja kati ya mashuhuda hao Ibrahim Mohamed Ali , amesema kuwa baada ya kusikia kelele hizo, alifika kwenye nyumba hiyo, na kuwakuta baadhi ya watu wengine wakianza kuokoa vitu vilivyokuwa ukumbini .
Alieleza kuwa wakati huo baadhi yao wameshapiga simu Kikosi cha zima moto na uokozi na baada ya dakika 10 kilifika na kuanza kuuzima moto huo ingawa nyumba yote iliteketea kwa moto.
“ Moto ulikuwa mkubwa sana na vyumbani kulizidiwa na moshi mkubwa mweusi ambao ulituzuia kuweza kuingia kwa ajili ya kuokoa vitu vyengine , ‘’ alieleza .
Nae shuhuda Hassan Mohamed Hassan alisema , kama moto huo usingeanza juu ya mapaa kikosi cha zima moto na uokozi chenge fanikiwa kuuzibiti .Mapema Mkuu wa Kikosi cha Zima moto na uokozi Chanjaani Wilaya ya Chake chake Inspekta Mwichande Hassan Khamis ,Alisema kuwa walipokea taarifa hizo majira ya saa 10 : 30 jioni na dakika 10 baadae waliwasili kaika eneo la tukio na kuuzima moto huo .
“Moto ulikuwa ni mkubwa mno na engekuwa twengepata taarifa mapema zaidi twenge fanikiwa kuudhibiti moto huo na nyumba isinge teketea yote,’’alieleza .
Hata hivyo amewataka wananchi kuwasiliana na kikosi chake moja kwa moja linapotokea tukio la moto au janga jengine kwa kupiga simu namba 114 ambayo ni bure.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Abdalla Hussein Mussa alikiri kutokea kwa tukio hilo jana Julai 20 , mwaka huu majira ya saa 10 : 30 jioni wakati mmiliki wa nyumba hiyo Mwalim Juma Yahya na mke wake wakiwa kazini .Kamanda huyo alieleza kuwa, nyumba hiyo pamoja na vitu vyake kadhaa vimeteketea kwa moto ingawa hakuna majeruhi wala mtu aliye poteza uhai.
“Sisi jeshi la Polisi tunawashukuru wananchi kwa kutoa taarifa za haraka kwa tukio hili ingawa , ushauri wangu kwao wajiwekee vifaa vya kuzimia moto majumbani mwao ,” alifafanua.
Mratibu wa Maafa Pemba, Khamis Arazak Khamis alisema kuwa, hadi sasa hawajapata tathmini halisi ya hasara iliyopatikana katika tukio hilo .
Hili ni tukio la tano kuwahi kutokea kwa mwaka huu kisiwani Pemba ambapo tukio la kwanza ni Skuli ya Sekondari ya Utaani ,nyumba ya mwananchi Wete , Madungu , Chuo cha ufundi Kengeja na nyumba hiyo ya Wawi.
Mwisho .
Comments
Post a Comment