Na Salma Lusangi
KATIBU Mkuu wizara ya Maji, Nishati na Madini Joseph Kilangi, amewataka watendaji wote wa wizara hiyo kuwajibika katika kuwahudumia wananchi huduma ya maji, Nishati na Madini ili kuwaondolea kero inayowakabili katika kupata huduma hizo.
Aliyasema hayo katika ukumbi wa ZURA wakati akizungumza na watendaji hao kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa wizara anayoisimamia, ili kupunguza malalamiko ya huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Zanzibar.
Alisema Maji yanaweza kupatikana kila kona ya Zanzibar lakini anashangazwa kwanini watu hawapati maji huenda kuna watu wanafunga maji kwa makusudi ili watumia magari kwa ajili ya kufanya biashara ya maji huku wananchi wakiteseka, jambo ambalo sio sahihi hata kwa Mwenyezi Mungu.
“Kila mfanyakazi ndani ya wizara hii akiulizwa nafasi yake ya kazi aseme mimi nawatumikia wananchi kupata huduma ya maji kwa hiyo mfanyakazi yeyote atakayemuona mtu anafunga koki ya maji basi atowe taarifa kwa kiongozi wake haiwezikani watu wakosema maji, Mtu akipiga simu maji yanfunguliwa ni wazi kama kuna mchezo unachezwa! Suala la maji linaniumiza kichwa,” alisema Kilangi.
Katibu Mkuu Kilangi aliwataka watendaji hao kila mmoja kuwajibika katika majukumu aliyopewa bila ya kusubiri kusukumwa na uongozi kwasabau kila mfanyakazi apewa majukumu yake (Job Description).
Alisema kinachohitaji katika kutekeleza majukumu hayo ni mashirikaina ya karibu ndio yatakayoleta maendeleo katika wizara hiyo.
Aidha alimuagiza Mkurugenzi Utumishi na Uandeshaji kufunga mfumo wa alama za zidole haraka iwezekanavyo ili kuangalia kwa karibu mahudhurio ya wafanyakazi kwani nidhamu inaanza na mahudhurio ya mfanyakaza wakati wa kuingia na kutoka kazini.
“Sitaki kusubiri ripoti ya makaratasi nitazidiwa akili nataka ikifika mwisho wa mwezi na print biometric system inioneshe kwa jina mfanyakazi aliingia saa ngapi kama saa 2.30 au saa 3.00 na muda aliyotoka,''alieleza.
Nahao wasio sikia Mkrugenzi Utumishi watwange barua kama mtu umemwita hataki kusikia mpe barua, hatukusudii kuharibiana lakini kama mtu hataki kubadilika basi sheria za utumishi zitumike.
Naye Naibu katibu Mkuu Mwanajuma Majid Abdalla alisema kama wanananchi hawapati huduma ya maji basi wizara hii itakuwa haina uwajibikaji hasa ukiangalia huduma hii ni muhimu sana kwa kila mtu kwani bila ya maji hakuna mtu atakaweza kuishi.
Alisema wafanyakazi msiridhike na majibu ya mafundi ya kusema maji hayatoki, bila ya kueleza sababbu ya msingi kwa sababu kuna watu wanancheza na akili za watu utadhani hawajui kama huduma ya maji inathawabu
Comments
Post a Comment