HOTUBA
YA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE RIZIKI PEMBE JUMA
NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KUTOA TAARIFA YA KAMPENI YA KITAIFA YENYE JINA LA
“MTOTO MBONI YANGU”, SIKU YA TAREHE 25/10/2024 KATIKA
UKUMBI WA WIZARA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO - KINAZINI
ZANZIBAR
NDUGU WAANDISHI WA HABARI
ASSALAMU ALAYKUM.
Napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu
kwa kutujaalia neema ya uhai na afya njema na kutuwezesha kukutana siku ya leo
kwa ajili ya kutoa taarifa ya KAMPENI
YA KITAIFA YENYE JINA LA MTOTO MBONI YANGU.
NDUGU WAANDISHI WA
HABARI,
Wizara
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya “Ndoto
Ajira” kutoka Dar es Salaam imeandaa
kampeni ya kitaifa yenye jina la MTOTO
MBONI YANGU, ambayo itafanyika katika mikoa mitano ya Zanzibar. Lengo kuu la kampeni hii ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuizunguka
nchi nzima ya na kuielimisha, kuiasa na kuzungumza na Wazanzibari wote wakiwemo wanafunzi, viongozi
wa dini, vijana, watoto na jamii kwa ujumla juu ya kupinga vitendo vyote vya
ukatili na Udhalilishaji wa Kijinsia kwa Watoto, Vijana, Wanawake na Wazee. Ili
kwa pamoja tuweze kuwalinda watoto na vijana wetu dhidi ya mmong’onyoko wa
maadili.
Kampeni ya MTOTO MBONI
YANGU inatarajiwa kuanza rasmi leo tarehe 23 Octoba na kuendelea hadi tarehe 30 Disemba 2024, kwa ufupi ni
kampeni ya miezi miwili kuanzia tarehe ya leo.
Aidha,
kampeni ya MTOTO MBONI YANGU
itazinduliwa pia kwa mbio za Marathon
siku ya Jumamosi ya tarehe 23 Novemba 2024 katika viwanja vya Mao Tse Tung. Na
kufungwa katika visiwa vya Pemba. Ni imani yangu kwamba jamii itaunga mkono
juhudi hizi.
Kampeni
hii imekuja ikiwa na azma ya kuunga mkono juhudi za mhe Rais wetu wa Zanzibar
na M\kiti wa Baraza la Mapinduzi Dr HUSSEIN ALI MWINYI na Serikali ya awamu ya
nane ambapo tunaziona juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali yetu katika
kuleta maendeleo ya nchi yetu na kupambana na vitendo vyote viovu vya Ukatili
na Udhalilishaji wa kijinsia.
Kupitia Kampeni hii, Wizara
inategemea kukusanya
kiasi cha Tsh 650,000,000/= ambazo
zitatumika katika utekelezaji wa kampeni hiyo. Hivyo, tunaiomba jamii, kuitikia
wito huu kwa kuchangia fedha ili zoezi hili liweze kufanikiwa kwani umoja ni nguvu
na utengano ni udhaifu.
NDUGU WAANDISHI WA
HABARI,
Marathon
yetu inatarajiwa kujumuisha takriban washiriki 20,000, kutoka Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara wakiwemo watoto,
vijana, wanawake, watu wazima kwa jinsia zote na hali zote bila kumuacha mtu
nyuma (wakiwemo na watu wenye ulemavu).
Washiriki
wote wa Marathon watapewa medali baada ya kumaliza mbio za kilomita 21 (nusu
marathon), kilomita 10, na kilomita 5, huku washindi watano wa
Mwanzo watapewa zawadi za fedha taslimu.
Ndugu waandishi wa habari,
MTOTO MBONI YANGU MARATHON ni Marathon ya kwanza kufanyika
ndani ya Zanzibar. Tunaomba wananchi wote na wadau wote kujitokeza kuchangia
kampeni hii. Tutoe wito kwenu pia ndugu wana
habari kuwa wa kwanza kujitokeza kuchangia
kwani shilingi yako moja ndio mwanzo wa hesabu. Hii ni nafasi ya kipekee kwa
kuunga mkono juhudi za Serikali yetu ya Mapinduzi Zanzibar ya awamu ya nane
katika kulinda vizazi vyetu viwe vyenye maadili mema kwa maendeleo ya taifa letu.
Gharama ya kujisajili kwa mtu mmoja mmoja ni Tsh 30,000
ambapo mshiriki atapata Tshirt na namba yake.
Pia kwa mara ya kwanza tumeleta package kwa makampuni na Taasisi mbalimbali kuchangamkia package hizi ambazo ni :
i)
Package
ya milioni 1,000,000 ambapo kampuni au taasisi itaweza kupata T-shirt 10 za
marathon, logo zao kuonekana kwenye red capert, kukaa sehemu maalumu siku ya
marathon pamoja na kutunukiwa cheti maalumu.
ii)
Package
ya 500,000 ambapo kampuni au taasisi itaweza kupata T-shirt 5 za marathon, logo
zao kuonekana kwenye red capert, kukaa sehemu maalumu siku ya marathon na
kutunukiwa cheti maalumu.
Kwa pamoja tukishirikiana tunaweza kulitokomeza janga
hili ndani ya nchi na Taifa letu ili kuwa na
kizazi chenye maadili mema, kinacho weza kuchangia mustakabal bora wa
taifa letu.
Zanzibar bila ya udhalilishaji inawezekana sana endapo
kila mmoja atatimiza wajibu wake.
Nakushukuruni sana kwa kunisikiliza.
Comments
Post a Comment