Skip to main content

BARABARA ZA LAMI ZA VIJIJINI CHANZO HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO KUWAFUATA WANAWAKE

 



NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

NI majira ya saa 8:00 jioni, jua limeshateguka, vivuli vya miti mikubwa ndio mwemvuli wangu,

Nipo kituo cha afya cha Uwondwe shehia ya Mtambwe mkoa wa kaskazini, wilaya ya Wete Pemba.

Mbele yangu, namuoma mjamzito, akitokea chumba cha muuguzi wa afya ya mama na mtoto, huku mkononi, akiwa na gamba la kliniki, akionekana na tabasamu.

Nilipomkaribia aliniambia, sasa huduma za mama na mtoto, wanazipata ndani ya kituo hicho, na hasa baada ya kumalizika kwa ujenzi wa barabara yao ya Bahanasa- Mtambwe kwa kiwango cha lami.

Barabara hiyo, ni kati ya zile tano (5), ziilizojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Changamoto za Millenia na watu wa Marekeani ‘MCC’ na nyingine ni Kipangani- Kangani, Chwale- Likoni, Mzambarau takao pamoja na Pandani hadi Finya zenye urefu wa kilomita 35.

Wananawake wa kijiji cha Mtambwe, wanasema moja ya huduma zilizoimarika ni upande wa afya ya mama na mtoto, na sasa ni miaka 10, wamesahau machungu, dhiki na shida.

HUDUMA ZA AFYA

Wanasema sasa wamesahau kubebwa kwa magunia, gari ya Ng’ombe na Punda kupelekwa bandarini, kwa ajili ya kuingizwa kwenye mitumbwi, ili kufikishwa hospitali ya wilaya ya Wete.

Hamida Juma Mohamed (35) wa Uwondwe shehia ya Mtambwe, anasema hawakuwa na thamani wanapotaka kujifungua, maana wanaume walikuwa ndio gari zao za muda, kwa kuwabeba hadi bandarini, kabla ya kuingizwa kwenye mitumbwi.

‘’Kabla ya ujenzi wa barabara hii, iliyofadhiliwa na ‘MCC’ ilikuwa hapa Mtambwe, hakuna huduma za kujifungulia, tulilazimika kwenda Wete, tena kwa mtumbwi,’’anasema.

Mtumwa Hamd Haji, (20), anasema sasa iaibu ya kubebwa na wanume imeshaondoka, maana huduma z akujifungulia zipo kijijini kwao.

''Ni hii ilikuja baada ya kumalizika kwa ujenzi wa barabara, na hapo kabla hali ilikuwa ngumu kwetu sisi akinamama,''anasimulia.

Khadika Juma anasema alipoteza mtoto wake wa kwanza, baada ya kujifungua ndani ya mtumbwi, wakati akisafirishwa kwenda hosptali ya wilaya ya Wete.



''Wanaume ndio walisaidiana na mkunga na kunipokea, lakini kwa vile ilikuwa usiku mtoto alikosa huduma na kufariki, hadi leo sijafanikiwa kupata mtoto mwingine,''anasema.

Ingawa alishabeba mimba sita, lakini hajabahatika ten mtoto, na aliarifiwa na wataalamu wa afya, kuwa fuko lake liliharibika siku aliojifungua ndani ya mtumbwi.

Muhudumu wa afya, kituo cha afya Uwondwe Zainab Hassan Shehe, anakiri kuwa, ujenzi wa barabara yao, ndio mwarubaini wa kupatiwa huduma za uzazi kijijini kwao.



‘’Kwa mwezi, tupokea kati ya wajawazito 60 hadi 65 na kuwapatia huduma za mama na mtoto, na wanaojifungulia hapa hujitokeza kati ya 10 hadi 15, jambo linalo ni faraja, hasa baada kuwepo kwa barabara hii,’’anasema.

Anaona, mwisho wa wajawazito wa Mtambwe kubebwa kwa magunia, gari za Ng’ombe na vitanda imekoma, baada ya kuwepo wa barabara hiyo na kufuatia kujengwa kwa kituo cha kujifungulia.

Lakini sio Mtambwe pekee, wanawake wanaokiri kuimarika kwa huduma hizo, hata Mwanaisha Bakari Haji wa Kangagani, anasema sasa adha ya kwenda hospitali za Wete au Chake chake, imekwisha.

‘’MCC kutujengea barabara yetu, kutoka Kipangani hadi kijiji kwetu, imetupunguzia machungu ya usafiri, maana ilikuwa gari za Ng’ombe au kubebwa kwenye magunia, ni jambo la kawaida,’’anasema.

Asia Haji Hussein wa Pandani, anasema dhiki kubwa walikuwa wakiipata miaka tisa iliyopita, juu ya kufuata huduma za uzazi Wete na Micheweni, sasa wameshazisahu, baada ya kujengewa barabara yao.

Kama alivyo Asia, hata Mwashamba Kombo Lali wa Finya, anasema watoto wake watatu, amejifungulia kituoni kwao, baada ya serikali kuimarisha huduma za uzazi na hasa uwepo wa barabara kwa kiwango cha lami.

‘’Baada ya kumalizika kwa ujenzi wa barabara yetu, sasa huduma za afya zipo saa 24, lazima tuwashukuru MCC na serikali ya Mapinduzi, kwa kushirikiana katika hili,’’anasema.



Bakar Faki Pandu ‘85’ mkaazi wa Chwale Madenajni, barabara ya Likoni hadi bandari ya Kojani, anasema huduma za afya zilizorota, na waliopokuwa wakitaka kumsafirisha mgonjwa kwenda hospitali ya Wete.

‘’Ujenzi wa barabara hii ya MCC kwetu wananchi wa Chwale, Likoni na Kojani imekuja kutuimarishia usafiri, na hasa tunapokwenda kwenye hospitali iwe cha Chake chake Wete,’’anaema.

Na hata Mwanaisha Hija Hamad, anasema aliwahi kuzaa njiani mwaka 2012, kutokana usumbufu wa barabara waliokuwa nao, ingawa sasa imekuwa mtelezo kwao.

Aisha Ussi Hamad, anasema pamoja na kuimarisha huduma za afya Kisiwa cha Kojani, lakini hata wanapokuwa na kesi kubwa za kwenda hospitali za Wete au Chake chake, usafiri upo saa 24.

‘’Kabla ya ujenzi wa barabara hii, ilikuwa ukipata tatizo la kwenda hospitali za Wete, kunausumbufu mara mbili, moja usafiri wa mtumbwi na kisha unakumbana na ubovu wa barabara, lakini sasa shida tumeisahau,’’anasema.

Suleiman Makame Issa wa Kojani, anasema usafiri na usafirishaji umekuwa rahisi kwao, iwe kwa wanaokwenda mjini, hospitali au kufuata huduma nyingine, makao makuu ya serikali ya wilaya.

‘’Sasa tunalala Kisiwa cha Kojani na kuwahi shughuli kama za matibabu hospitali kuu za Wete au Chake chake, jambo ambalo, lilikuwa ni adimu kwa miaka kadhaa,’’anasema.

SERIKALINI

Afisa Mdhamini wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Pemba Ibrahim Saleh Juma, anasema tokea kufunguliwa kwa barabara hizo, miaka tisa (9) iliyopita hawajawahi kuzifanyia matengenezo, kutokana na uimara wake.

‘’Matengenezo tuliyoyafanya, ni barabara ya Bahanasa- Mtambwe kwenye daraja, baada ya kuharibika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mwaka 2017 na kwa sasa barabara zote tano, ziko madhubuti,’’anasema.

Aliyekuwa kuwa Mhandisi mkaazi wa ujenzi wa barabara Pemba, wakati wa ujenzi wa barabara za MCC, Khamis Massoud Khamis, anasema uimara wa barabara hizo, ulitokana na aina ya ujenzi.

Ujenzi wa barabara hizo umetofautiana na nyingine, maana tabaka mbili za juu ‘sub base and base’ zilichanganywa kokoto nyembamba na saruji, kwa ujazo wa mita moja, kwa mfuko mmoja wa saruji.

Barabara za ‘MCC’ hazikutumia utaalamu wa lami moto ‘asphalt congreatE’ bali zilitumia mfumo wa lami ya kuchemsha ‘surface dressing’ na kisha humwagwa, baada ya muda humiminiwa kokoto zenye ujazo wa milimita 15 hadi 20, na kuzama kwenye lami hiyo.

‘’Baada ya kushindiliwa hadi kuzama kwa kokoto, humwagwa tena lami zikiwa na kokoto ndogo ndogo, zenye ujazo kati ya milimita 8 hadi 10, lengo ni kuziba nafasi ilizoachwa wazi na kokoto kubwa za awali,’’anafafanua.

Jengine ni kutumia shilingi bilioni 1.1 kwa urefu wa kilomita 1, wakati ujenzi wa barabara za kawaida kwa urefu huo, hutumia gharama ya shilingi bilioni 1.

‘’Ujenzi wa aina hii ya barabara za MCC, hutakiwa kufanyiwa matengenezo kila baada ya miaka 10, ingawa kwa kwetu zinaweza kuzidi kutokana na kutokuwepo kwa gari, nyingi zenye uzito wa zaidi tani 15,’’anasema.

Aliyewahi kuwa Afisa Mdhamini wa wizara hiyo Hamad Ahmed Baucha, anasema barabara hizo, zilisimamiwa na wenyewe kuanzia uchoraji wa michoro, hadi kwenye ulipaji wa fidia.

                                  Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...