NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MKUU wa wilaya
ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, amesema ni lazima waandishi wa habari, wanasiasa
na wanaasasi za kiraia, kuutumia vyema uhuru wa kujieleza, ili kuepusha madhara
yanaoweza kujitokeza.
Kauli hiyo ameitoa,
ukumbi wa Chuo cha Samail Gombani Chake chake Pemba, wakati akifungua semina ya
kijamii, kuhusiana na uhuru wa kujieleza, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Waandishi
wa habari Pemba ‘PPC’ kwa kushirikiana na Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari
Tanzania ‘UTPC’ na kuwashirikishi waandishi wa habari, wanasiasa, jamii na viongozi
wa dini.
Alisema, ni
kweli uhuru wa kujieleza ni haki ya kikatiba, na nivigumu mtu kumzuia kutoitumia
haki hiyo, ingawa suala la tahadhari ya kukiuka mipaka, ni jambo la kuzingatia.
Alieleza kuwa,
waandishi wa habari hutumia vyombo vya habari kama tv, redio, magazeti na vile vya
mtandaoni, ili kufikisha ujumbe kwa jamii husika.
‘’Hapa kwa
eneo hilo, la kuzingatia zaidi ni, ili kuepusha machafuko ni kuhakikisha habari
hizo kwanza ni za kweli, kisha ziwe zimefanyiwa uchunguuzi wa kina,’’alisema.
Kuhusu wanasiasa
na viongozi wa dini, alisema nao wanafanana na kundi la waandishi wa habari,
juu ya uhumimu wa kujiridhisha kabla ya kufanya mahubiri yao.
Akizungumzia
umuhimu wa semeina hiyo, alisema ‘PPC’ na ‘UTPC’ wameamua jambo jema, la kuyakumbusha
makundi hayo wajibu wao.
Mapema Mwenyekiti
wa ‘PPC’ Bakar Mussa Juma, alisema semina hiyo ni muendelezo wa majukumu ya ‘PPC’
ya kuhakikisha waandishi wa habari, wanafanyakazi zao kwa uweledi.
‘’Waandishi
wanayo majukumu yao ya msingi, ikiwemo kuhabarisha, lakini sasa lazima kabla ya
kuilisha jamii habari husika, suala la utafiti ni jambo jema,’’alieleza.
Nae Afisa
kutoka ‘UTPC’ Severin Mapunda, alisema semina hiyo ni ya kuchapuza dhana ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, juu ya umuhimu
wa majadiliano (4R).
Alisema Dk.
Samia amekuwa kila siku akihimiza umoja, mshikamano na majadiliano, na ndio
maana ‘UTPC’ sasa iko katika mikoa kadhaa, ikiendesha semina hizo.
Akiwasilisha
mada ya uhuru wa kujieleza, Mwanasheria Mohamed Hassan Ali, alisema kila jambo
ili lifanikiwe vizuri, linahitaji kulindwa kwa sheria.
‘’Kwa mfano,
suala la uhuru wa kujieleza ni haki ya msingi ya kikatiba, lakini imewekewa
ulinzi wa sheria kadhaa, ikiwemo sheria za habari, sheria ya vyama vya siasa,’’alifafanua.
Akichangia kwenye
mkutano huo, Mjumbe wa halmshauri kuu taifa ya chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa kusini
Pemba, Saleh Nassor Juma, alisema bado waandishi wa habari hawako huru kwenye
kazi zao.
Nae Meneja wa Redio Jamii Micheweni Ustadh Ali Massoud Kombo, ameikumbusha serikali kuharakisha upatikanaji wa sheria rafiki ya habari Zanzibar.
Nae sheikh Said
Abdalla Nassor, alisema njia nzuri ya kufikisha ujumbe, ni kutumia lugha ya
staha, kuchagua wakati na muundo wa maneno, kwa aina ya kundi linalofikishiwa
ujumbe huo.
Mkuu wa
wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya, alipongeza hatua ya ‘PPC’ ya kuandaa semina
hiyo, ambayo imesababisha kuwakutanisha wadau husika.
Mwisho
Comments
Post a Comment