NA ASHA ABDALLA, PEMBA@@@@
WAUGUZI wameshauriwa kuwa na maadili mazuri katika kufanya kazi zao, ili kuendelea kutoa huduma nzuri zinazo stahiki na kuwapa faraja wagonjwa wakati wanapohudhuria katika vituoni mwao.
Hayo yameelezwa jana Mei 9, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, ukumbi wa chuo cha Samail Gombani Chake Chake, Pemba wakati alipokua akizungumza na wauguzi katika kuelekea kuadhimisha siku ya wauguzi duniani, ambayo kilele chake rasmi ni Mei, 12 mwezi huu.
Amesema kuwa na maadili, mazuri katika kufanya kazi ni muhimu, kwani kunapelekea kupata umaarufu kwa watu na kuitia hadhi mzuri taasisi kwa ujumla.
"Tujitahidi tuwe na maadili, kwani tunapokuwa kazini taasisi tunazo zifanyia kazi zina tudai maadili mazuri na watu ambao tunawapatia huduma katika Taasisi hizo na kujijengea umaarufu mzuri katika kazi zetu", alieleza.
Kwaupande wake Mkurugenzi Idara ya Uuguzi na Ukunga Wizaraya Afya Mwanaisha Juma Fakih aliwataka wauguzi hao kufanya kazi kwabidii na uweledi mkubwa, kwa kutoa huduma zilizobora na zenye udhati ndani yake ili kupata malipo mazuri kutoka kwa Muumba .
Hata hivyo aliwaeleza kuwa wawe tayari katika kufanya utafiti kwenye kazi zao, ili kuleta mabadiliko mazuri ambayo yatasaidia kupata muonekano mzuri ambao utaweza kuongeza ushirikiano mkubwa katika jamiii.
Nae mtoa mada katika hafla hiyo Mohamed Ali Salim alisema kua, wauguzi wanatakiwa kuwatibu wagonjwa kwa nia nzuri, kwani wanapata fadhila kubwa kwa Allah SWT, pamoja na kuwa na uhusiano bora katia ya mgonjwa na muuguzi wakati wanapotoa huduma za matibabu.
Nae msomaji risala kutoka kituo cha Afya Mzambarauni Farida Breki Karama, ameipongeza Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia rais Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kujenga vituo vingi vya afya na kupelekea hali ya uuguzi kuimarika siku hadi siku .
Alisema pamoja na kuwepo vituo vingi vya afya, kuna changamoto mbalimbali ambazo zinawakabiliwa ikiwemo uhaba wa wauguzi na wakunga katika vituo vya Afya, hali hiyo inapelekea kufanya kazi nyingi na kukosa muda wa mapunziko.
Baada ya hafla hiyo kufanyika alikabidhiwa zawadi ya cheti cha ufanyakazi bora na fedha taslimu muuguzi kutoka katika kituo cha afya Maziwango'mbe Bivite Hamad Haji ambayo iliandaliwa na jumuiya ya Wauguzi Zanzibar.
Madhimisho hayo hufanyika kila ifikapo Mei 12 na kaulimbiu ya mwka huu ni "Wauguzi wetu ndio mustkbali wetu ".
MWISHO
Comments
Post a Comment