NA MARYAM
NASSOR, UNGUJA@@@@
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar,
imesema mageuzi ya sera na sheria
za habari nchini yaendane sambamba na
kanuni na maadili ya vyombo vya habari.
Akizungumza
katika kongamano la madhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari, Katibu
mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Fatma Hamad Rajab, akimuakilisha waziri wa wizara hiyo alisema hilo litafanikiwa.
Alisema,
Serikali ya awamu ya nane, inafanya juhudi
kubwa ya kuweka mazingira rafiki kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini, bila ya kuathiri uhuru wa mtu mwingine.
Alieleza kuwa, hivyo wandishi wa habari wanatakiwa kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria, weledi na maadili, ili kunufaika na sekta hiyo.
Nae Afisa sheria kutoka Tume ya Utangazaji Zanzibar Khadija Mabrouk Hassan, alisema rasimu ya sheria ya habari tayari inafanyiwa
kazi kwa sasa na iko katika hatua za
mwisho katika afisi ya Mwanasheria mkuu kwa hatua zaidi.
Alisema, sheria
zilizofanyiwa kazi ni pamoja na sheria ya utangazaji no.7 ya mwaka 1997 ambayo
ilifanyiwa marekebisho na sheria no. 1 ya mwaka 2010.
Alisema kuwa, na sheria ya usajili wa wakala wa habari, magazeti na
vitabu No.5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria No. 8 ya mwaka
1997.
Aidha alisema kuwa, lengo kuu la kuharakisha sheria
hizo, ni kutaka Zanzibar kuiweka katika
mazingira mazuri kwa vyombo vya habari
na wananchi kwa ujumla.
Nae, mtoa
mada ya historia ya vyombo vya habari Zanzibar, Dk. Abdallah Mohamed Juma, alisema kuwa Zanzibar, ina
historia kubwa ya vyombo vya habari kutokana na kuwa ya kwanza kuwa na
televisheni ya rangi na magazeti.
Alisema
kuwa, licha ya kupiga hatua kwa kuongezeka kwa idadi kubwa ya vyombo vya habari 67 vilivyosajiliwa Zanzibar, lakini wandishi wanatakiwa
kujielekeza katika uwandishi wa habari za vijijini, kuliko kusubiri habari za matukio.
Nao, baadhi ya washiriki wa kongamano hilo,
walisema kuwa ni kweli uhuru wa habari
upo, lakini haujatosheleza moja kwa moja
hivyo, ni vyema kuharakisha kuzifanyia marekebisho shearia zilizopo za habari.
MWISHO
Comments
Post a Comment