NA NIHIFADHI ISSA, ZANZIBAR.@@@@
WAANDISHI wa habari wanajukumu la kuendelea
kufanya uchechemuzi wa mabadiliko ya sheria zenye mapungufu na ambazo sio
rafiki kwa tasnia ya habari ili kutoa fursa ya upatikanaji wa sheria zilizo
bora.
Yamebainishwa hayo na Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari
Wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar Dkt.
Mzuri Issa nakusema kuwa Sheria
nambari 5 ya Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu ya mwaka 1988, ambayo
imefanyiwa marekebisho sheria namba 8 mwaka 1997 sheria hii licha yakuwa ni
kongwe imekuwa na mapungufu mengi yanayokwamisha haki na uhuru wa vyombo vya
habari Zanzibar.
Akizungumza katika kikao cha kujadili
mapungufu ya sheria zinazokwamisha uhuru wa habari huko katika ukumbi wa
TAMWA Tunguu amesema Demokrasia sahihi hutegemea uhuru wa
vyombo vya habari unavyoweza kusimamia maslahi ya jamii, ikiwemo
uhuru wa kutoa maoni na kujieleza bila
ya kuingiliwa pamoja kusambaza taarifa
na mawazo ya aina mbalimbali kwa kufuata kanuni
zilizowekwa ni haki inayotambuliwa na sheria za kitaifa na kimataifa.
“ikiwa
Zanzibar imo ndani ya Tanzania na imeridhia mikataba mbalimbali ambayo inalinda
tasnia ya habari ipo haja kufanyika marekebisho kwa sheria ambazo haziendi
sambamba na uhuru wa habari ikiwemo
sheria hii” alisema Dkt Mzuri.
Kwa mujibu wa Sheria nambari 5 ya wakala wa habari, magazeti na vitabu ya mwaka 1988, yenye marekebisho ya sheria namba 8 mwaka 1997 katika sheria hii vipo vifungu
ambavyo havijatowa uhuru kwa waandishi pia kwa vyombo vya habari kikwemo
kifungu cha 14 (1) kilichompa mamlaka mrajisi kumtaka mchapishaji gazeti
kupeleka kopi mbili kila siku kwa gharama zake kwa madai ya kuweka kumbukumbu.
Afisa mradi
wa Uhuru wa Habari kutoka TAMWA Zanzibar
Zaina Abdalla Mzee amesema uwepo wa sheria
hiyo unakinza dhana ya demokrasia na utawala
“kwanza hii sheria ni kongwe imefikia wakati irekebishwe ili kuchapuza uhuru wa habari
ambao tunautaka,”
Ameendelea kuwa “Sheria
hizihaziwagusi waandishi tu bali hata wanachi wanaotumia vyombo vya habari
kutoa malalamiko au shida zao zinapowakabili
huingiwa na woga na hivyo kukosa
uhuru wa kujieleza” ameeleza Zaina.
Waandishi wa habari ndio wahusika wakuu
katika hili, Khatib Suleiman ni mwandishi
wa habari wa Gazeti la Habari Leo anasema vifungu hivyo vya sheria vinarudisha
nyuma utendaji wa kazi wa mwandishi wa habari “kwa mfano chombo cha habari
hakipati mapato kinapata wapi fedha za kupeleka nakala kila siku kupeleka kwa
mrajis mimi mawazo yangu ofisi ya mrajis iwe na mtu maalum wa kufuatilia izo
habari kama wanataka kuendelea na hiyo sheria” amesema Khatib.
Kwa upande wake mwandishi mwanandamizi Hawra Shamte
amesema licha ya kuwa kuna sheria zinazosimamaia sekta ya habari lakini
kiuhalisia zinaonekana hazifanyi kazi ipasavyo ya kulinda usalama wa waandishi
wa habari hivyo zinahitaji kufanyiwa marekebisho.
“Tanzania ni moja kati ya nchi iliyoridhia mikataba
mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo inalinda tasnia ya habari, waandishi
wa habari, watetezi wa haki za binadamu hivyo wajibu wa Serikali kuendeleza uhuru wa habari kama ya;ivyo
makubaliano hayo,” Hawra.
Salim Said Salim ni mwandishi mkongwe Zanzibar amesema
waandishi wanakutana na vikwazo wakati wa kutekeleza majukumu yao”Vyombo vya
habari hufikia wakati mwengine kufungiwa na kushindwa kuendelea na kazi zao za
utangazaji kwa kipinmdi kadhaa au
kupigishwa faini hii inachukiza,”alisema Salim .
Wananchi wanayo haki ya kupata habari kupitia vyombo mbalimbali Mfaume Muhammed anasema ikiwa vyombo vya habari vitaekewa
vikwazo au vizuizi ambavyo si vya lazima
itawia vigumu kupata habari “lazima
vikwazo vingine vitatuliwe ambavyo vinaonekana havina ulazima sana izo nakala
mbili ni nyingi wakishindwa kuchapisha na sisi wasomaji wa magezeti tutakosa
kusoma habari” alifafanua Mfaume.
Akitoa maoni Mwanasheria kutoka Tume ya
kurekebisha Sheria Zanzibar Sabra Mahmoud Iddi amesema wanategemea mchakato
Sheria ya habari utafanyiwa marekebisho ili kupata sheria bora zinazozingatia
maslahi ya waandishi na uhuru wa vyombo vya habari.
“Hili jambo ni la muda mrefu na linapitia
hatua kwa hatua lazima waandishi muwe na subra kwa lengo la kupata sheria bora
zinazokwenda na wakati”amesema Sabra.
Comments
Post a Comment