Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Riziki Pembe Juma ameitaka Bodi ya Ushauri ya Watoto Taifa kuwa na umoja moja katika mapambano ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto.
Ameyasema hayo jana wakati
alipokutana na bodi hiyo Ofisini kwake Kinazini Mjini Unguja. Amesema hivi sasa
inaonekana watoto wa kiume kuharibiwa kwa kasi. Hivyo Mhe. Riziki amewataka
wajumbe wa bodi hiyo kunganisha nguvu ya pamoja katika
mapambano ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na Watoto.
Mhe. Riziki amefahamishwa
kwamba Wizara anayoisimamia imeundwa kwa ajili ya kushughulikia masuala mbalimbali ya kijamii nchini, ikiwemo masuala
yanayowahusu watoto, hivyo ameitaka bodi hiyo kuhakikisha changamoto
zinazowakabili watoto kuziwasilisha
katika Wizara hiyo ili kuweza kupatiwa ufumbuzi.
Aidha amewataka kuhakikisha wanabadilisha mitazamo ya baadhi ya watoto wanokataa kushiriki katika vikao au wito wowote kwa kuona kwamba hakuna malipo ya fedha au zawadi kwani hali hiyo inaweza kutoa fursa kwa watu wabaya kutumia mwanya huo na kuwaharibu.
Amewahakikishia kuwa
changamoto zinazowakabili katika bodi
kupitia Wilaya zao, Wizara itajitahidi kutazifanyia kazi kadiri hali
itakavyoruhusu ili kuona mafanikio yanapatikana juu ya kunzishwa mabaraza hayo.
Naye Makamo Mwenyekiti wa
bodi ya Ushaui Taifa ndugu Tatu Khamis Ramadhan ameelezea kufurahishwa kwake
kwani ni mara ya kwanza bodi hiyo
kukutana na Waziri wao, na kuelezea changamoto zinazowakabili ikiwemo ndoa za
utotoni, baadhi ya vijiji kutofuatwa
ipasavyo sheria ya mtoto sheria no.6 ya mwaka 2011 ambayo inaeleza haki za
mtoto.
Pia wameomba kufanya
uwezekano wa kuwekwa vituo vya one stop center katika hospitali mbalimbali ili
iwe rahisi kupatiwa huduma za matibabu kwa waliopata tatizo la udhalilishaji.
Mwisho
Comments
Post a Comment