NA ASHA ABDALLA ,PEMBA@@@@
Afisa Mdhamini Afisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekazaji Pemb Dk., Fadhila Hassan Abdalla amewataka wananchi wa kisiwani Pemba, kushirikiana na uongozi wa mradi wa Head of Jasmine kutoka China, katika kuondoa tatizo kubwa la saratani ya mlango wa kizazi ambalo linaongezeka kwa kila mwaka .
Ameyasema hayo leo katika Hospitali ya Chakechake wakati alipokua akifungua kambi ya Madaktari wa kichina itakayo kuwepo kwa muda wa wiki mbili kisiwani hapa, kwa ajili ya kufanya matibabu ya magonjwa hayo katika hospitali na hata vijijini
Alisema kuwa wanachi hususani akina mama wawe na utayari wa kuhamasishana katika kutoa ushirikiano mkubwa, ili kupatiwa tiba iliyo sahihi na kuondokana na maradhi ambayo yanaongezeka siku hadi siku.
Akitowa takwimu ya ongezeko la saratani ya mlango wa kizazi Tanzania, alisema kuwa kumefikia ongezoko la watu 10,242 ambao nisawa na asilimia 34.4, waliopata maradhi hayo nchini hapa.
Nae Daktari kutoka China Xiaomin Qi alisema kuwa, mradi huo umesainiwa na kukubaliwa mwaka 2018 na kupata mafanikio makubwa katika kuchunguza wagonjwa na kufikia 19,000 kwa upande wa Zanzibar ambao wambao wana maradhi hayo .
Hata hivyo alieleza kua, kati ya wagonjwa 2,973 walipata huduma ya upasuaji baada ya kuonekana na matatizo mbalimbali, ambayo yanaendana na saratani ya mlango wa kizazi na mengine hayaendani na saratani, hivyo wamepata mafanikio makubwa katika kupata huduma ambayo ni muhimu katika afya zao.
Kwa upande wake Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Khamis Bilali Ali, alisema kuwa wananchi wawe tayari katika kupokea ujio huo, kwani hii ni fursa ya kipekee ambayo imekuja kisiwani hapa, hivyo wanapaswa kuwashajiisha na wengine, kwakuwapa taarifa ili wahudhurie kwa wingi katika kupata huduma hiyo .
"Wananchi nawaombeni muhamasishane kuhudhuriya kwa wingi, kwani hawa wenzetu wamejitolea kuja kutupa huduma hii bila ya malipo yoyote, lengo lao ni kutaka wazanzibar kuwa na afya nzuri,''alieleza.
Miradi huo unaendeshwa baina ya wizara ya Afya na ushirikiano mkubwa wa madaktari kutoka China ambao utatoa huduma hiyo katika Wilaya zote nne za Pemba.
MWISHO
Comments
Post a Comment