NA HASSINA KHAMIS, PEMBA@@@
JAJI Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhani Abdalla, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kusimamia na kudumisha Muungano kwa maendeleo ya wananchi wote.
Alisema hayo kwenye hafla ya utiaji saini ya mkataba wa ujenzi wa kituo jumuishi cha haki Pemba katika ukumbi wa ZRA Gombani Chake Chake.
Mkataba huo wenye ishara ya kuimarika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ulisainiwa kati ya Mtendaji mkuu wa Mahakama ya Tanzania Profesa, Elisante Ole Gabriel na Mkandarasi wa kampuni ya Deep Construction Mr, Ravinder Singh Jabbal .
Alisema ujenzi utajengwa kwa fedha za mkopo kutoka benki ya Dunia kupitia Mahakama ya Tanzania, ambapo utawawezesha wananchi wa Pemba, kurahisisha kupata haki zao bila ya usumbufu wowote.
Aidha nae Mtendaji mkuu wa Mahakama Tanzania Prof: Elisante Ole Gabriel, alisema kituo hicho jumuishi kitajegwa kwa fedha za mikopo, yenye gharama nafuu iliyoombwa na Mahakama ya Tanzania kwa awamu mbili.
"Lengo ni kutoa fursa kwa wananchi wa kisiwani Pemba, kupata huduma za haki kwa ngazi zote ikiwemo Mahakama ya Rufaani,"alisema .
Vile vile alieleza fursa nyengine ni kuweza kushajiisha matumizi ya rasilimali, huduma za tehama na kuimarisha Mahakama zote za Tanzania kama ni alama ya muungano ambapo kwa Sasa umefikia miaka 60 .
Kwa upande wake Mkandarasi wa kampuni ya Deep Construction Ravinder Singh Jabbal, alisema atahakikisha mradi huo unamaliza kwa wakati aliopangwa.
Aidha aliwataka wananchi kutoa ushirikiano wa hali na mali, ili kuhakikisha ujenzi huo unamalizika kama ilivyo kwenye mkataba.
Sheha wa shehia ya Mfikiwa Bimkubwa Rajab Tangwi ,alimtaka Mkandarasi kuzingatia nguvu kazi kwa vijana wa eneo hilo kwa kuwapatia ajira za muda na kudumu.
"Sio vyema kuona vibarua wanatoka maeneo mengine, wakati vijana ninao katika shehia yangu na wanatafuta ajira, "alisema.
Zaidi ya shilingi bilioni 9.8 zinatarajiwa kutumika katika mradi huo wa ujenzi jumuishi, ambapo fedha hizo ni kati za mkopo wa Mahakama ya Tanzania, alipata kwa awamu ya kwaza Dola milioni 65,na awamu ya pili Dola milioni 90 ,watajenga vituo jumuishi tisa, ikiwemo cha Mfikiwa kwa Pemba na Mahakama za mwazo 60.
MWISHO
Comments
Post a Comment