MAAFISA ustawi wa
jamii kisiwani Pemba, wamekumbushwa, kuongeza maarifa zaidi, ili kukabiliana na
majanga yaliomo katika jamii, kwani wao ndio wahusika wakuu, katika kuilea
jamii.
Walielezwa kuwa,
jamii imekuwa ikiwapelekea vilio vyao mbalimbali, hivyo wasipokuwa makini
kuongeza maarifa ya utatuzi wa majanga, utoaji wa ushauri nasihi na malezi ya
kisayanysi, wanaweza kupoteza uaminfu wao, kwa jamaii.
Hayo yameelezwa leo
Mei 19, 2024 na Mkurugenzi wa Mwemvuli wa asasi za kiraia Pemba ‘PACSO’ Mohamed
Najim Omar, wakati akiyafungua mafunzo ya siku tano (5), kwa maafisa walioko
serikalini na wale wa mtaani, kwenye mafunzo yanayoendelea, skuli ya maandalizi
Madungu Chake chake.
Alisema, kila siku
ndani ya jamii, kumekuwa kukiibuka majanga mapya, hivyo kama hawakuwa makini
kuongeza maarifa, ya jinsi gani ya kuisadia jamii, wanaweza kukosa kazi kuachwa
nyuma baadae.
‘’Kila siku huzuka majanga
mapya, kwa mfano watoto kubakwa, kulawitiwa, kudhalilishwa, kufanyia ukatili
kwa vipigo vya kupindukia, hivyo waongeze maarifa, ili wajue namna ya kuwasaidia,’’alieleza.
Alieleza kuwa,
mafunzo hayo anaamini yatawasaidia mno maafisa hao, katika utekelezaji wa
majukumu yao ya kila siku, kwa lengo la kuleta mabadiliko, ndani ya jamii.
Kwa upande wake, Katibu
Mkuu wa ‘PACSO’ Sifuni Ali Haji, alisema anategemea baada ya kumalizika kwa
mradi wao wa upatikanaji haki wa miaka minne, kuweko na mabadiliko makubwa
ndani ya jamii.
‘’Kwani kundi la
watoto, limekuwa likikumbwa na majanga mbali mbali na kisha hukosa ushauri
nasaha, na kuwapelekea wingine hata kukatisha masomo na nadoto zao nyingine,’’alieleza.
Aidha Katibu Mkuu
huyo aliipongeza ‘UNDP’ kwa kupatikana kwa mradi huo, kwa kiasia kikubwa
umekuja kuongeza, ufanisi kwa kundi la jamii na hasa watoto, katika kutokata
tamaa, baada ya kufanyiwa udhalilishaji.
‘’Mradi unataka
kuona kwanza, watoto wanaishi bila ya majanga, na kama yakitokezea, iwe maafisa
ustawi wawe na uwezo na mbinu za kuwarejesha katika mfumo wa maisha, ambao walidhani
umeshatoweka kwao,’’alieleza.
Mtoa mada kutika
mafunzo hayo ya siku tano, anayetoka Jumuiya ya ‘ZASWA’ Saleh Juma Mbarouk, alisema
moja ya sifa za msuluhisi au afisa usatawi, ni kujitambua kwa undani.
Alieleza kuwa,
jingine ni kujenga uaminifu, kuwa na taarifa kadhaa, takwimu na kuisoma jamii,
yake kabla ya kuanza kutoa ushauri nasaha.
‘’Huwezi kuwa Afisa
ustawi wa jamii mzuri, ikiwa kwanza hujitambui thamani yako na jamii yako, hulifahamu
kundi unalolifanyia kazi, huna taarifa sahihi na wakati mwingine hata takwimu, ‘’alieleza.
Wakichangia mada
katika mafunzo hayo, washiriki Arafa Amour Mzee kutoka Mkoani na Ali Abdalla Juma
wa Chake chake, wamesema, kazi kubwa inahitajika, ili kuwakinga watoto na majanga.
Walisema, wazazi na
walezi, lazima wasiwe sehemu ya kuwapotosha watoto wao, kwa mfano
kuwashirikisha katika mambo yasiowahusu, kwani kufanya hivyo, kunaweza
kukawavunjia ndoto zao.
Hata hivyo,
wameipongeza ‘PACSO’ na wanafadhili wao ‘UNDP’ kwa uamuzi wa kutoa mafunzo hayo,
ambayo yatawajengea uwezo wa kukabiliana na mambo kadhaa, ikiwemo viashiria vya
udhalilishaji katika maeneo yao.
Mafunzo hayo ya
siku tano, ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa upatikanaji haki, unaotekelezwa
na ‘PACSO’ kwa muda wa miaka minne, na tayari kuanzia mwaka jana, shughuli
kadhaa zimeshafanyika, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya haki za binaadamu na
utawala bora, kwa watu wenye ulemavu,
viongozi wa dini na waandishi wa habari.
Mwisho
Comments
Post a Comment