NA HAJI NASSSOR, PEMBA@@@@
UONGOZI wa Jumuiya ya uhifadhi wa mazingira ya
kijiji cha Kambini Kichokochwe, wilaya ya Wete Pemba, umesema kuwa, ukitaka
kufanikiwa katika utekelezaji wa jambo lolote, ni vyema kuwashirikisha
waandishi wa habari.
Ulisema, kutokana na kuwa na suati pana na ya
haraka, wanaweza kufanikisha kampeni yoyote, ambayo jumuia, jamii au serikali
kuu imeamua kuwafikia wananchi wake.
Kauli hiyo imetolewa leo Mei, 19 na Katibu wa Hifadhi
hiyo, Bakari Suleiman Juma, wakati akizungumza na wanachama wa jumuiya ya
waandishi wa habari Pemba ‘PPC’ na wananchi wingine, kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari dunia, ambapo waandishi hao, waliiadhimisha
kwa upandaji wa mikoko.
Alisema, waandishi wa habari, wamekuwa na
mchango mkubwa, katika kufakikisha kila kitu, mfano zoezi la uhamasishaji upandaji
miti hiyo, hivyo kwa tukio hilo, limewapa hamasa.
Alieleza kuwa, aanamini jamii ya Tanzania,
itapata mwanga wa kuhakikisha wanapanda miti katika maeneo yaliokumbwa na mabadiliko
tabia nchi, kufuatia tukio la waandishi wa habari kushirikiana nao.
‘’Kwa hakika uongozi wa ‘PPC’ na wadu wenu
Umoja wa Vilabu vya Habari Tanzania ‘UTPC’ mmefikiria jambo jema na zuri, la
kuadhimisha siku yenu, kwa upandaji miti katika eneo la bahari ya hindi, hapa
Kambini Kichokochwe,’’alieleza.
Kwa upande wake, Mwenyikiti wa Klabu ya
waandishi wa habari Pemba ‘PPC’ Bakar Mussa Juma, alisema waandishi pamoja na
kazi yao ya kuandika habari, wameona ni vyema kuungana na jamii, katika zoezi
hilo.
Alieleza kuwa, mara nyingi tukio hilo
hupendelea kuadhimisha kwenye kumbi za mikutano, ingawa kwa kutambua umuhimu wa
upandaji miti na faida zake, wameamua kujitoa,’’alieleza.
Alifahamisha kuwa, mwaka jana wanachama wa ‘PPC’
walishiriki katika zoezi la usafi, katika fukwe ya bahari ya Vuma wimbi mkoa wa
kaskazini Pemba, kwa dhamira ya kuziweka safi.
‘’Waandishi wa habari, nao ni waathirika wa
joto lenye ujazo mkubwa, na ndio maana tumehamasika kuzihama ofisi kwa muda na kulirejeshea
uasili wake eneo hili la Kichokochwe kwa upandaji miti,’’alieleza.
Akizungumza kwenye zoezi hilo, Mwenyekiti wa taasisi
ya Community Forest Pemba ‘CFP’ Kombo Seif Khamis alisema, wamefarajika, kuona
wameungana na waandishi wa habari, katika zoezi hilo.
Alieleza kuwa, kwani suala la athari za
mabadiliko tabia nchi haziwakumbi wavuvi, wakulima, wafugaji pekee, bali hata
kundi la waandishi wa habari, wakati wanapotekeleza majukumu yao.
Wananchi wa kijiji hicho, Fatma Shaame Hamad
na Asha Ali Mussa, wamesema wamepata ari na kasi ya utunzaji wa mazingira,
kufuatia tukio la waandishi wa habari, kuungana nao.
Walisema, ijapokua wao ndio waathirika wakubwa
katika eneo hilo, lakini janga likiwa la kitaifa, kila mmoja anakuwa anakumbana
na changamoto.
Kaimu Katibu wa ‘PPC’ Mchanga Haroub Shehe,
aliwakumbusha waandishi wa habari, kuendelea kuyaibua maeneo kama hayo, ili
wenye mamlaka wachukue hatua.
‘’Kupanda miti kama hivi leo, ni zoezi moja muhimu
sana, lakini tuhakikishe, tunazidi kuyaibua, ili wanaofanyakazi zao, wabuni
njia mbadala la kuzuia athari zaidi,’’alifafanua.
Mwandishi wa habari Hassan Msellem na mwenzake
Maryam Salum Habibu, wamesema ni vyema kwa uongozi wa ‘PPC’ kwa kushirikiana na
wadau wao, kufanya zoezi kama hilo, kila fursa inapopatikana.
Katika zoezi hilio, mkiti aina ya mikoko
10,000 imepandwa kwa mfumo wa mbegu, katika eneo la bahari ya hindi, ambalo
miaka 25, eneo hilo lilikuwa sehemu ya nchi kavu.
Mwisho
Comments
Post a Comment