Zanzibar: Nihifadhi Issa.
Chama Cha Waandishi wa Habari
Wanawake Tanzania -Zanzibar – TAMWA-Z kimekutana na waandishi wa Habari chipukizi,wahariri,wamiliki
wa vyombo vya Habari na wadau wa Habari kwa kuwatunuku na kuwatunza waandishi wa Habari 23 waliokuwa
kwenye mradi wa Waandishi wahabari vijana.
Mahafahali hayo yamefanyika katika
Ukumbi wa Bima uliopo Maisara Mkoa Mjini Magharib Unguja.
Khairat Haji ni Kaimu Afisa Programmu TAMWA -Zanzibar amesema
katika hatua za kumarisha uongozi kwa wanawake mradi
huu ambao hii ni awamu ya pili ambapo kwa awamu ya kwanza uliwafunza na
kuwasimamia waandishi vijana 18 kwa 2022
akieleza kuwa mwaka 2023 waandishi vijana 24 walipata fursa katika mradi
huu wa Wamawake na Uongozi”Kupitia mradi huu
ulikuwa unahitaji kazi 348 na hadi kufikia leo kazi hizo ni 347,huku magazeti
47 ,Makala za radio 117 huku Makala za mitandamo 187 ambazo zinakamilisha kazi
347” Amesema Khairat
Shifaa Said ni Jaji Kiongozi wa
Tuzo za Waandishi wa Habari Chipukizi kwenye kuhariri kazi za waandishi hao 24
zilizofika katika sehemu Majaji watatu,Ali Sultan , Husna Mohamed Khamis kwa
muda wa siku nne na Makala zilizofika 175 ndio zilizowasilishwa magez 15,radio
85 na mitandao 75 =175
Amesema Vigezo muhimu
walivyoangalia ni weledi na umahiri
katika sauti Pamoja zizosikika na umahiri wa lugha kwenye kazi hizi pamoja na upekee
wa mada na matumizi ya radio.
“pia tumeangalia mafanikio na
ukuwaji wa wanufaika wa waandishi na kufanya Makala na vipindi vyenye mabadiliko kwenye jamii ubunifu na weledi wa kuangali na sio Habari za
matokeo ila ni Habari zinazoangalia masuala ya kuibua na kujumuisha makundi ya
watu wenye mahitaji maalum”alisema Shifaa
Mkurugenzi chama cha waandishi wa
habari wanawake TAMWA Zanzibar Dkt
Mzuri Issa amesema kuwa Makala na kazi hizo zimeleta mabadiliko na kazi hizo
zimeleta kwa kuwashawishi wanawake
kuingia kwenye siasa na kupata nguvu ya kusaidia kuvunja dhana potofu kwenye
wanawake kuwa kwenye uongozi.
“waandishi hawa wamefanya kazi
kubwa ambazo zimepekelea mimi kupigiwa simu na wanawake wanataka nmwakani
waingie kwenye mchakato wa kugombania nafasi niwape njia za kufanya nijambo la
kufurahisha na kupendeza”alisema Mzuri
Mjumbe wa Bodi ya Tamwa
Zanzibar Bi Hawra Shamte amesema kuwa uwepo kwa mahafali hayo
kwa waandishi hao 23 ni kukubali kujifunza na
kuandika masuala ya wanawake na hii ni
Dhahiri kuona kwamba majukumu kwenye kuandika
masuala ya wanawake na uongozi yametamalaki
“Ninachotaka kuwaambia waandishi hawa tuendelea kaundika na kuihabarisha umma juu ya uwepo kwa Habari hizi katika kuleta mabadiliko katika jamii hii ambayo inategemea kuwa na viongozi wanawake na wanaume”alisemalizia Hawra
Berema Suleiman Nassor mwandishi
wa Zenji Fm pia ni mnufaika wa Mradi huu. Amesema kwenye
suala hili ni takwimu na upatikanaji wa kuandika na kuwasaidia na kuwafikia jamii
ilimuia vigumu
“ mwanzo nilikuwa naadika Habari za kawaida
na sasa nimekuwa na naandika Habari zenye kuleta mabadiliko usawa wa kijinsia kwanza sikuweza ila kwa sasa
nimekuwa mzoefu hii ni kutokana na juhudi za
TAMWA” alisema Berema
KHadija Rashid Nassor mwandishi wa Radio jamii Mkoani Pemba ambae
pia ni mnufaika kwa mradi huo kwa miaka
miwili sasa amesema wamekuwa kwenye
uandishi wa kuunganisha na kuwasaidia wanawake na waandishi wengine
“nimekuwa mzoefu sasa nawafundisha
wenzangu namna bora ya kuandaa Makala zenye ubora kwa kuunganisha mikataba na sera
mbalimbali”alisema Khadija
Nae mwandishi wa radio jamii Micheweni Esau Simon amesema mradi umemsaidia kufanya kazi za kuleta mabadiliko na sasa kumukuwepo kwa usawa wa mazungumza hususan kwa upande wa watu wenye ulemavu .
Mwandishi wa DW na Mhariri Salma Said na amesema suala la kuona vijana
wanakuwepo kwenye mradi hii ni kuonesha masuala ya uandishi wa Habari za
viwango na wenye kuleta mabadiliko.
“Ikiwa haya yataendelea kuandikwa
basi kutakuwepo kwa mabadiliko kwa jamii kwenye uleta uwajibikaji ,kubadilishwa
kwa sheria na haki kutendeka”alisema Salma
Sambamba na hayo Mwandishi wa Gazeti la Daily News Issa Yussuf amewasisita waandishi hao kuzingatia matumizi
ya lugha kwani ni muhimu.
“kwenye masuala ya lugha hii ni
jambo ambalo litawafikisha mbali na kuwasaidia zaidi kwenye uandishi kujifunza
na kusoma masuala ya mikataba na sheria mbali mbali” alisema Issa
Katika mahafali hayo jumla ya
washindi watatu wamepata zawadi ya cheti na kompyuta mpakato akiwemo Amina
Masoud Jabir kutoka Radio Jamii Mkoani, Hassan Mselem Pemba Online Media na
Asya Mwalim Haji kutoka Gazeti la Zanzibar Leo.
Mradi wa huo wa kuwawezesha
waandishi wa habari vijana YMF kuandika
habari za wanawake na uongozi uliowashirikisha waandishi vijana 24 unguja na pemba umetekelezwa na TAMWA
ZANZIBAR kwa kushirikiana na Shirika la National Endowment for Democracy (NED)
Mwisho.
Comments
Post a Comment