NA ASHA ABDALLA, PEMBA@@@@
MJUMBE wa Baraza kuu la Taifa umoja wa Vijana CCM kusini Pemba, Amriya Seif Saleh Amewataka vijana kuhudhuria kwa wingi katika kuchangia Damu salama kila ifikapo muda kwani kufanya hivyo nikuondoa changamoto mbalimbali ambazo zinajitokeza kwa Mama Wajawazito na ajali mbalimbali zinapotokea.
Ameyasema hayo leo 25/4 /2024 huko Uwanja wa Gombani Wiilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba wakati walipokua na zoezi la uchangiaji Damu Salama ikiwa ni shamra shamra za maazimisho ya mika 60 ya Muungano wa Tanzania.
Alisema kua vijana ndio nguvu pekee katika kuendeleza Muungano katika nchi nao wana uwezo mkubwa wa kuchangia Damu salama hivyo nivyema kuhamasishana na kuhudhuria kwa wingi kwani kufanya hivyo ni umoja na mshikamano katika kuujali Muungano.
"Ndugu zangu niwambieni kwa sasa changamoto ya damu imekua ni yakudumu kitaifa na kimataifa sio kuwa ni ya Tanzania pekeee bali ni yadunia mzima "Alieleza
Aidha aliwapongeza vijana wote na Wananchi kwa ujumla kwakuhudhuria kwawingi katika kufanikisha zoezi zima la uchangiaji Damu salama kwani wamefanya jambo kubwa na la kiuzalendo na ushujaa wa hali ya juu.
Hata hivyo aliwaomba Vijana hao wawe ni Mabalozi wema katika Familiya zao na jamii kwa ujumla kwa kuwapa Elimu ya kutosha juu ya Uchangiaji Damu kuwa iwe ni muendelezo mzuri kwa kila baada ya muda kuchangia ili kuokowa Maisha ya Tanzania na maslahi ya Taifa.
Nae Mratibu wa kitengo cha Damu salama kutoka Wizara Afya Pemba, Khalfan Ali Massoud alisema kuwa wao wizara ya Afya wanawataka Wananchi wote wahamasishane zaidi kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kuchakungia Damu kila baada ya muda ili wapate kuwasaidia akinamama waja wazito na ajali mbalimbali ambazo zinajitokeza siku hadi siku .
Aidha alisema kuwa kuhudhuria kwawingi katika kuchangia Damu ni ule umoja na mshikamano ambao vijana wanakuwa na ndio wanaotegemewa katika kuendeleza Muungano.
Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza kuu Wazazi Taifa Mkowa wa kusini Pemba Juma Kheri Khamis aliwashauri vijana waendelee kuhamasishana katika kuchangia Damu kama nimuendelezo wa shamra shamra za miaka 60 ya Muungano kwani vijana ndo kiungo kikubwa ambacho kinategemewa katika kuudumisha Muungano.
Mapema Diwani wa jimbo la wara katika Wilaya ya chakechake Kassim Juma Khamis aliwapongeza vijana kwakuja kwa wingi katika kuchangia damu kwa hiari na wasichoke waendeleze kujitolea kwani kuchangia damu nimoja katia ya kueka hakiba pale yanapotokea majanga mbali mbali.
Nae Mchangiaji Damu salam Nassor Hamad Omar Alipongeza serekali kwa kupitia wizara ya Afya kwa kuwajali sana wananchi wake kuweka siku maalumu ya uchangiaji damu kwani hii itapelekea kusaidia watu mbalimbali ambao wanauhitaji mkubwa wa Damu wakiwemo wajawazito ,walopata ajali tofauti watapata kusaidiwa kupitia Damu hizo.
Jumla ya chupa 55 za Damu salama zichangiwa kutoka watu mbalimbali katika wilaya ya mkoani na Wilaya ya Chake, wakiwemo umoja wa Vijana CCM, vijana wa kambi ya JKU Pamoja na wananchi wa kusini Pemba.
Comments
Post a Comment