NA ASHA ABDALLA, PEMBA @@@@
WAKUU wa wilaya, Masheha na Madiwani wametakiwa kushirikiana kwa pamoja katika kuwaelimisha wananchi kuhusiana na mipango miji, ambayo itaweza kuwasaidia wananchi wote kuwa na makaazi yenye hadhi kisiwani Pemba.
Hayo yameelezwa na Salma Abdalla Ali kutoka Idara ya mipango miji na vijiji kamisheni ya Ardhi Pemba, kwanyakati tofauti, wakati walipokua wakitoa mafunzo ,huko wilayani Mkoani Mkowa wa Kusini Pemba.
Alisema kua Mipango miji imekuja kwa ajili ya kuwapimia Wananchi maeneo ambayo hajawahi kupimwa hususani yale ambayo hayajafanyiwa ujenzi, ili waweze kupunguza migogoro mbalimbali ambayo inajitokeza ndani ya jamii.
Aidha alisema kuwa Idara ya Mipango miji wanakazi kubwa ya kuelimisha jamii, kupitia vipindi mbalimbali vya redio na tv, kwani wanachi bado wanauwelewa mdogo kuhusu mipango miji.
Hata hivyo alisema kuwa, wanatarajia kupanga eneo kwa kila wilaya, ambalo litaweza kuimarisha mji ambalo litaweza kutumika kwa matumizi mbalimbali ya wananchi waliomo kwenye wilaya hizo.
"Tutajaribu kupima maeneo na kueka eneo ambalo wananchi wataweza kulifanyia shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo kilimo, mifugo, masoko kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi yetu," alifafanua.
Kwa upande wake Katibu Tawala wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, alisema kua nilazima mipango miji wawe karibu na wananchi, ili kuwapa elimu zaidi ili waweze kufahamu hiyo mipango miji nini na malengo yao ni yepi.
Nae Afisa usajili wa Ardhi kamisheni ya Ardhi Pemba Yussuf Hamad Kombo, alifahamisha kua umilikishwaji wa ardhi ndio njia pekee, ambayo inaweza kupunguza migogoro mbalimbali wananchi wanakumbana nayo katika jamiii.
"Tunapokuja mipango miji tukakupangia, upimaji, kukumilikisha na kukusajili, inakuwa ni umuhimu mkubwa kwani eneo lako litakua tayari, lishawekwa kuzuizi na hakuwezi kutokea mgogoro wa aina yoyote hataka nieneo umerithi au kuzawadiwa , "alifafanu.
Kwaupande wake Afisa wa Ardhi kutoka kamisheni ya Ardhi Hamida Juma Hamad aliwaomba Masheha na Madiwani, kujitahidi katika kushirikiana kuwapa elimu wananchi, ili waweze kulifanikisha kikamilifu zoezi zima la upimaji wa ardhi.
Nae Mkurugenzi kutoka Baraza la mji la Mkoani Yussuf Kaiza Makame, alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa wakuja mpango miji kwani kwasasa Pemba mzima, itajengeka katika muonekano mzuri kulingana na ilivo kua hapo awali.
Hatahivyo alisema kuwa Mipango Miji waweze kupima ardhi kwa kuweka alama na kutowa hatimiliki ili kuepusha udanganyifu ambao utasababisha mizozo kwa wananchi.
Nae Sheha wa Shehia ya Kengeja Mohamed Kassim Mohamed aliishukuru mipango miji kwa kuwapatia mafunzo hayo, waliowapa na kuahidi watayafanyia kazi kwa wananchi wao, na kuwaomba na wao mafunzo hayo kuwapitia wanavijiji kuaelimisha zaidi ili wapate kuelewa kwaharaka.
Kwa upande wake Diwani wa kuteuliwa Wilaya ya Mkoani Arafa Mzee Amour, alitowa ushauri kwa Idara ya Mipango Miji wakati wanapotaka kupima Miji ile wanayotaka kuekeza wajaribu kupima maeneo yale ambayo hayajajengwa yapo karibu nabarabara ili kuuweza kupata miundombinu iliyo bora .
Mafunzo hayo yaliofanyika wilaya ya Mkoani yalijumuisha katibu tawala wa wilaya ya Mkoani kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Masheha wa Shehia 36 za Mkowa Kusini na madiwani ,na Mkurugenzi wa baraza la Mji Mkoani.
MWISHO.
Comments
Post a Comment