NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WAUMINI wa dini ya
kiislamu kijiji cha Mtemani, shehia ya Wawi wilaya ya Chake chake Pemba, wamekumbushwa kuyaendeleza mema yote waliyokuwa wakiyatenda
katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, kwani amri na makatazo hayo waliyokuwa
wakiyatii, bado yanaendelea kuwepo.
Hayo yameleezwa na khatibu wa
msikiti wa Mtemani Wawi wilaya ya Chake chake Salim Nassor, wakati akitoa
hutuba mbili za swala ya Edi-l Fitir, mara baada ya kukamilika kwa swala hiyo,
iliyofanyika msikitini hapo leo April 10, 2024.
Alisema, hipendezi na haingii akilini kuona waumini wa dini ya kiislamu waliokuwa wakifuata maamrisho ya Muumba,
katika mwezi mtukufu wa Ramadhan na kisha sasa amri hizo, kuzipindua na kufanya
watakavyo.
Alieleza kuwa, Muumba aliyekuwepo
katika mwezi uliomalizika, ndio yule yule aliyepo katika miezi mingine, hivyo
ni wajibu wa waumini hao kuendelea kumtii, ili kupata radhi zake.
Khatib huyo alifafanua kuwa, katika
kipindi cha mfungo, kila mmoja alikuwa laini mbele ya mwenzake, na kutoonekana
kwa walevi, wizi, zinaa, ngoma, kutukanana ambapo amri zote hizo, bado zinatakiwa
kutekelezwa katika miezi mingine.
‘’Mimi niwausie waislamu wa Wawi na
wingine duniani kote, katika mataifa mingine, bado amri za Muumba, ndio zile zile zilizokuwepo
katika kipindi cha mwezi wa Ramadhan, na sasa zinaendelea hivyo ni wajibu wa
kuzitii,’’aliwakumbusha.
Katika hatua nyingine Khatib huyo,
aliwakumbusha waumini wa dini ya kiislamu, kwa siku ya leo ya sherehe ya sikukuu
ni kula, kunywa, kuvaa na kutembelea maeneo yaliohalali, ili kuzitakasa nyoyo
zao.
‘’Kwa mfano siku ya leo, unaweza
kuwatembelea wagonjwa, wenye hali ngumu za maisha, mayatima kwa ajili ya
kuwafariji kama sehemu ya sherehe na sio kufanya maasi,’’alifafanua.
Hata hivyo, amewakumbusha wazazi na
walezi, kuwavisha mavazi ya staha watoto wao hasa wa kike, na kuacha
kuwafunganisha na watoto wenzao wingi, ili kuepusha majanga.
‘’Kila mmoja ni shahidi kuwa, kwa
siku hizi vyombo vya usafiri hasa vya maringi mawili ni vingi, lazima kwa mtoto
mmoja asizidi mtoto mmoja, ambapo kufanya hivyo, itakuwa rahisi kwenye
udhibiti,’’alieleza.
Baadhi ya waumini wa dini ya
kiislamu, waliozungumza na mwandishi wa habari hii, wamewashauri waumini wenzao,
kuyaacha kwa vitendo makatazo ya Muumba, ili iwe ni nusra katika maisha yao ya leo na baadae.
Omar Faki Hamdan wa Wawi, alisema
hata mfano wa hutuba iliyotolewa katika msikiti uliopo Mtemanani, ni aina ya
ukumbusho mzuri kwa waumini.
Nae Ridhiwan Othman Hamdu
alisisitiza, haja kwa wazazi na walezi kuwasomesha watoto dini yao ya kiislamu,
ili wajue namna bora na iliyoridhiwa na Muumba ya usherehekeaji wa sikuu za kiislamu.
Waumini wa dini ya kiislamu wa
shehia ya Wawi na vijiji jirani, wameungana na waumini wingine dunini kote, leo
Arpili10, 2024 katika sherehe ya sikuu ya Edi-lfitir, ambayo huja baada ya kufunga
aidha siku 29 au 30 za mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Mwisho
Comments
Post a Comment