NA SAID ABDULRAHMAN, PEMBA@@@@
Msaada huo umetolewa na Mkaguzi wa Polisi
Jamii shehia ya Pandani, Inspector Khalfan Ali Ussi baada kutembelea kambi ya
wanafunzi hao na kuona hali halisi ilivyo wakati unapozima umeme, jambo ambalo
linawapa usumbufu wakati wanapopitia masomo yao.
Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa
hivyo alieleza kuwa, vitaweza kuwasaidia wanafunzi hao katika kujisomea wakati
umeme unapokata kwenye mabweni yao.
Inspector Khalfan aliwataka
wanafunzi hao kujitahidi katika masomo yao, ili waweze kufaulu vizuri na kuwa wakombozi katika
familia zao na taifa kwa ujumla.
Aidha alieleza kuwa, wako tayari
kufuatilia nyenendo za wanafunzi hao na yeyote ambae atapatikana na hatia ya
kutohudhuria kwenye masomo, adhabu kali itatolewa dhidi yake.
"Kwa
wanafunzi ambao mnakaa kambi katika skuli zetu hizi, ni vyema tukafuata muda
ambao umepangwa ili kuondosha matatizo ambayo yanaweza kuepukika", alieleza.
"Kwa wale ambao wamekimbia skuli,
niwaombe wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto hao wanarudi skuli kuendelea na
masomo yao na hili sio ombi ni lazima", alifahamisha Khalfan.
Sambamba na hayo Inspekta huyo
aliwasisitiza wanafunzi hao kuacha rushwa muhali kwani inarudisha nyuma
maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
"Pale ambapo kutatokezea tatizo
lolote ambalo liko kinyume na maadili yetu, ni vyema tukatoa taarifa mapema ili
jambo hilo liweze kuchukuliwa hatua na wala tusione aibu kusema ukweli",
alisema Inspekta Khalfan.
Mapema Mratibu wa Polisi Jamii Mkoa
wa Kaskazini Pemba Inspekta Makame Ali Makame alifahamisha kuwa, lengo la kuanzishwa
Polisi jamii nchini, ni kuhakikisha wanaondosha vitendo vya uhalifu ambavyo
vimekithiri katika jamii.
Inspekta Makame alieleza kuwa,
katika jamii kumekuwa na matukio mbali mbali ya uvunjifu wa amani, hivyo
aliwasisitiza wanafunzi hao kutoa taarifa kwa wakubwa wao pale ambao wataona kuna
viashiria vibaya.
Sambamba na hayo Inspekta Makame
aliwasisitiza wanafunzi hao kutumia muda wao mwingi katika kushughulikia masomo
yao, kwani ndio msingi bora wa maisha yao ya baadae.
Nae Kaimu mwalimu Mkuu wa skuli ya
msingi Pandani Halima Khalifan Said aliupongeza uongozi wa Polisi jamii hehia
ya Pandani kwa kuwapatia wanafunzi hao msaada, ambapo umewapa faraja na furaha.
Aidha Halima aliahidi kushirikiana
pamoja na uongozi wa Polisi Jamii shehia ya Pandani, ili kuona kero ambazo zipo
katika skuli zao zinatatulia kwa mashirikiano ya wote.
"Tunamshukuru sana Inspekta
Khalfan kwa msaada wake aliotupatia, hii inaonesha dhahiri kuwa ana upendo wa
dhati kwetu", alisema Halima.
Nae mwanafunzi Fatma Salim alitoa
shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake na kusema kuwa kutatuliwa changamoto
hiyo iliyokuwa ikiwakabili, imewapa matumaini makubwa kuendelelea na masomo
yao.
"Tulikuwa tunapata shida sana
wakati unapozimwa umeme, hivyo kwa vifaa hivi ambavyo tumepatiwa , tutavitunza
ili kuona kwamba vinadumu kwa maslahi yetu ote”, alisema mwanafunzi huyo.
MWISHO
Comments
Post a Comment