NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo, imelipongeza Shirika la Magazeti ya serikali, kwa ubunifu wao wa
kuanzisha jarida maalum, la kutangaaza utekelezaji wa Ilani ya Chama cha
Mapinduzi kwa wananchi.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa hiyo Zanzibar, Tabia Maulid Mwita, wakati akizungumza
na masheha wa wilaya nne za Pemba, kwenye hafla ya ugawaji wa jarida hilo,
iliyofanyika ukumbi wa Mfuko wa Hifadhi Jamii Zanzibar ‘ZSSF’ Tibirinzi Chake
chake.
Alisema,
uongozi wa Shirika hilo, umezitekeleza kwa vitendo ahadi za Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, pale alipowataka wakuu wa taasisi kuwa
wabunifu, ili kuwafikia wananchi.
Alieleza kuwa,
ubunifu huo ambao umezalisha jarida la kueleza kwa upana yale yaliyotekelezwa
na serikali, utasaidia sasa kwa wananchi kuyaona kwa vitendo.
Waziri Tabia
alieleza kuwa, ingawa vyombo vya habari vya serikali vipo ikiwemo ZBC, lakini
kupitia jarida hilo, kumeongeza wigo kwa wananchi, kuyasoma yaliotekelezwa.
‘’Kwanza
nimpongeza mno Mhariri Mtendaji wa Shirika hili, pamoja na timu yake, kwa
kuanzisha jaridi maalum, ambalo kwa njia moja ama nyingine, linakuza ufahamu
kwa wananchi,’’alieleza.
Waziri huyo
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita, alisema wapo
baadhi ya wananchi, wamekuwa hawataki kuamini, kile kilichofanywa na serikali,
lakini kupitia jarida hilo, watajifunza na kuona.
Katika hatua
nyingine, amewakumbusha masheha hao kuhakikisha majarida hayo, yanawafikia
wananchi wote, ili wapate kusoma na kufahamu.
‘’Inawezekana
wapo ambao hawaamini kuwa, ndani kipindi kifupi Rais wetu wa Zanzibar, Dk.
Hussein Ali Mwinyi, ameshafanya mengi, ikiwemo ujenzi wa skuli za ghorofa,
hospitali na masoko lakini, ndani ya jarida hilo unaweza kuyakuta,’’alieleza.
Mapema Mkuu
wa Mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, amesema kama wananchi watalisoma
jarida, wanaweza kuongeza ufahamu nia ya Rais wa Zanzibar.
‘’Lakini pia
itakuwa ni fursa kwa wananchi na hata masheha na viongozi wengine, kuwepo kwa
uimarishaji katika jarida lijalo,’’alifafanua.
Hata hivyo
Mkuu huyo wa Mkoa, amewatadharisha masheha hao, kutowapa wananchi ambao hawana
nia njema, ikiwemo kilichana.
Mkuu wa
wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, alisema mfumo wa majarida kama hayo ni
muhimu, hasa kuwepo kwa habari mchanganyiko za maendeleo.
Mwenyekiti
wa Masheha wa wilaya ya Chake chake Khamis Idd Songoro, alisema jarida hilo
litawasaidia wale wanaodai kuwa, Zanzibar hakujafanywa maendeleo ndani ya awamu
hii.
‘’Sasa
tutawapa wasome wenyewe, waone kasi na Rais wa Zanzibar, katika utekelezaji wa
ahadi zake kwa wananchi, tokea alipoingia madarakani,’’alieleza.
Hata hivyo
alipendekeza kuwa, majarida hayo ni vyema kwa awamu ijayo yakongezwa, ili yawafikie
wananchi wengi zaidi katika shehia zao.
Nae sheha wa
shehia ya Kinyasini Raiye Amour na mwenzake wa Shumba Vyamboni Time Said, walisema
majarida hayo, yatasaidia kwa wananchi, kupata kumbu kumbu za utekelezaji wa
ahadi za Rais wa Zanzibar.
Katika hafla
hiyo, jumla ya masheha 129 wa wilaya nne za Pemba, kila mmoja alikabidhiwa majarida
10, ambapo wengine miongoni mwa waliokadbiwa ni wakuu wa mikoa, wilaya na
makatibu tawala.
Mwisho
Comments
Post a Comment