NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MKUU wa mkoa wa kusini Pemba, Mattar
Zahor Massuod, amewataka washairi na watunzi wa Umoja wa Washairi wa Pemba ‘UWAPE’
kutunga mashairi, yenye kuihamasisha jamii, kupiga vita vitendo vya udhalilishaji,
dawa za kulevya na majanga mengine.
Alisema,
jamii imezongwa na majanga na kukuawa kila siku, hivyo washairi wanayonafasi ya
kukemea, kushauri, kuekeza njia ya kupunguza matendo hayo, na chanzo chake
kupitia mashairi yao.
Mkuu huyo
Mkoa, ameyasema hayo Machi 19, 2023 ukumbi wa Umoja ni nguvu Mkoani, kwenye hutuba yake
iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Chake chake, Rashid Abdalla Ali.
Mkuu huyo wa
Mkoa alisema, njia ya mashairi ni nzuri na nyepesi katika kufikisha ujumbe husika
kwa jamii, hivyo ni wakati wa washairi wa ‘UWAPE’ kuliono hilo haraka..
‘’Kwa sasa,
kila mmoja ni shahidi kuwa, jamii yetu inakumbana na majanga, mbali mbali hata
migogoro ya ardhi, dawa za kulevya, udhalilishaji na mivutano ya kifamilia,
hivyo washairi waangalie kuisadia jamii,’’alieleza.
Katika eneo
jingine, Mkuu huyo wa mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, alisema wazo
la kuanzisha UWAPE, ni mzuri, maana itasaidia hata vijana kujiajiri.
Aidha
aliwataka watunzi wa mashairi kutoka umoja huo, kutumia mashairi yao, katika
kuikuza na kuiendeleza lugha ya kiswahili sanifu.
Alisema,
duniani kote wanaamini kuwa, ukitaka lugha sanifu ya kiswahili na lahaja zake, ni
Zanzibar hivyo kupitia UWAPE, iwe jukwaa muhimu na adhimu katika eneo hilo.
Hata hivyo
aliwapongeza viongozi wa UWAPE, kwa kubuni umoja huo, ambao kwa njia moja ama
nyingine, inazidi kuitangaaza kugha ya kiswahili nje na ndani.
Aidha
aliipongeza bodi ya redio Jamii Mkoani, kwa kusimamia hadi kufanikisha
kuanzishwa kwa umoja huo, ambao alitaka kuona unasambaa hadi mkoa wa kaskazini
Pemba.
‘’UWAPE
usambaae hadi wilaya za Wete na Micheweni, hii itasaidia kwanza kutangaazika
vizuri, lakini itaibua vipaji vyengine tofauti,’’alieleza.
Katibu
Tawala wilaya ya Mkoa Miza Hassan Faki, aliipongeza redio Jamii Mkoani, kwa
kuibuka washindi wa taifa, kwa matumizi bora ya lugha ya kiswani kwa mwaka huu.
Alieleza
kuwa, ushindi walioupata wakati wa kongamano la Idhaa za za lugha ya kiswahi,
Machi 18, mwaka huu ni ishara njema kwa wafanyakazi wa redio hiyo.
Akizungumzia
wanachama wa UWAPE, amewakumbusha kuwa
kabla ya kuchapisha mashairi yao, kujenga utamaduni wa kuhaririana, ili
kuepusha matumizi mabaya ya lugha husika.
Hata hivyo,
ameukumbusha uongozi wa ‘UWAPE’ kutunga mashairi yanayojenga umoja na mshikamano
miongoni mwa wananchi nchini.
Akisoma
risala, Mwenyekiti wa UWAPE Khalid Said Mohamed, alisema, moja ya changamoto
inayowakabili kwa sasa ni ukosefu wa ofisi na studio ya kurikodia kazi zao.
Alieleza
kuwa, jengine ni kukosa nyenzo za fedha za kuisambaaza ‘UWAPE’ mkoa wa
kaskazini Pemba pamoja na jamii kukosa mwamko wa kuyapokea mashairi yao.
Hata hivyo,
alisema wazo la kuanzishwa kwa ‘UWAPE’ ni kuwepo kwa kipindi cha tungo na
mashairi, kwenye redio Jamii Mkoani, ambapo watunzi walikuwa hawajuani.
‘’Kisha kwa
mara ya kwanza, tulikutana watunzi na washairi wote Septemba 24, 2022 redio
Jamii Mkoani, na kuibua wazo la kuanzisha umoja, uitwao UWAPE,’alieleza.
Mapema Mkuu
huyo wa mkoa wa kusini Pemba, Mattar Zahor Massoud, alikizindua kitabu cha
mashairi, CD na chanali ya youtube pamoja na kumkabidhi zawadi mtunzi bora wa
mashairi kutoka UWAPE.
UWAPE ambayo
imepata usajili mwaka huu, inao wanachama 25, kati ya hao wanawake 10 na
wanaume 15, ambapo lengo lao kuu ni kutoa elimu kwa njia ya mashairi, kipato,
kukikuza kiswahili pamoja na jamii kupenda mashairi.
Mwisho
Comments
Post a Comment