NA SALMA LUSANGI, ZANZIBAR
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mhe.Rahma Kassim Ali ameuagiza uongozi wa Kamisheni ya Ardhi Zanzibar kushirikiana na ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Magharibi "B" kuirudisha serikalini eka iliopo Fujoni kufuatia kutumika kinyume na utaratibu.
Eka hiyo inayomilikiwa na bw Faki Rashed Faki lakini anadaiwa kuikata viwanja na kuviuza kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kinyume na matumizi ya shughuli za kilimo yaliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mhe.Rahma ametoa agizo hilo alipofanya ziara kuitembelea eneo hilo mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa mwananchi kuhusiana na uuzwaji wa eneo hilo la eka ya serikali.
"Hatua ya kurudisha serikalini eka hii itakua ni funzo kwa wale wote ambao walipewa eka kwa ajili kuziendeleza kwa shughuli za kilimo na badala yake kuzitumia eka hizo kwa kuzikata viwanja na kuuza"Alisisitiza waziri Rahma.
Ameongeza kuwa Wizara ya Ardhi Zanzibar itahakikisha inazifatilia kwa makini eka zote za Serikali na yoyote atakaegundulikana anakwenda kinyume na matumizi sahihi ya eka hizo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Hata hivyo Waziri Rahma amewataka wananchi wanapotaka kununua maeneo kufika Kamisheni ya Ardhi Zanzibar kwani Taasisi hiyo imeundwa kisheria katika kusimamia masuala yote yanahusiana na ardhi na umiliki wa Ardhi Waziri Rahma alifafanua kuwa hatua hiyo itasaidia kueupusha migogoro ya ardhi Zanzibar inayoweza kuepukika endapo wananchi watafuata sheria.
Aidha waziri rahma alisisitiza mwananchi yoyote aliyepewa eka na anataka kubadilisha matumizi ya ardhi afuate taratibu zikizowekwa.
Naomba niwaeleza wananchi wanaomiliki ekari za Serikali, Wizara ya Ardhi imeweka utaratibu maalum wa kuwasilisha mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa kamisheni ya Ardhi na Wizara iwapo yatakwenda sambamba na mpango wa Serikali haitokuwa na pingamizi maamuzi hayo" alisema waziri rahma
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kaskazini " B" Hamidi Seif Said ameahidi kulitekekeza agizo hilo kwa vitendo na amesema wilaya hiyo haitosita kumchukulia hatua mtu yoyote atakaekwenda kinyume na maagizo ya Serikali katika matumizi ya ekari hizo kwa maslahi ya nchi na taifa kwa ujumla.
Nae ndugu Faki Rashed Faki ambae anadai kuwa eka hiyo amerithi kutoka kwa mzazi wake na amekata viwanja kwa kuuza kwa watu wawili tofauti amedai kuwa alikua hajui kama eka za Serikali hazitakiwi kuuzwa na kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Katika hatua nyengine Waziri Rahma. alipata nafasi ya kumtembelea Mzee Hafidh Ali Mdachi huko Bumbwisudi alielitoa eneo lake kupisha Mradi wa ujenzi wa hospital ya Wilaya huko jang'ombe kwa binti hamran na kuagiza kamisheni ya ardhi kutafutia ufumbuzi tatizo la eneo alilopewa fidia kuwa tayari limeshaendelezwa.
Mwisho.
Comments
Post a Comment