NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@
JESHI la Polisi Mkoa wa kusini Pemba,
linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumshambulia mfanyabiashara Maulid
Haroub Mpemba na mke wake, katika eneo la Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa huo
Abdalla Hussein Mussa, alisema watuhumiwa hao, walikamatwa katika siku na
maeneo tofauti humo.
Aliwataja
waliowakamata kuwa ni pamoja na Saleh Mohamed Abdalla ‘Mbambe miaka 33, Mohamed
Rashid Mohamed miaka 42 wote wakaazi wa Mjiweni Kengeja na Salum Mohamed Seif ‘Rumbwi
miaka 36 mkaazi wa Tumbi Wambaa.
Alisema
kuwa, baada ya kupokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa wasamaria wema, majira
ya saa 7:00 usiku Machi 17 mwaka huu, Jeshi la Polisi liliandaa mitego na
kufanikiwa kuwakamata katika maeneo na siku tofauti.
Alisema
watuhumiwa hao, wanaodaiwa kumshambulia mfanyabiashara huyo kwa vitu vyenye
ncha kali, katika sehemu mbali mbali za mwili wake, huku mke wake
wakimshambulia kwa kumpika marungu.
Alieleza
kuwa, tukio hilo lilisababisha mfanyabiashara huyo kupata maumivu makali katika
mwili wake na hasa eneo la kichwani na kutokwa na damu nyingi, ambapo kisha alikimbizwa
hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba kwa matibabu.
“Mfanyabiashara
huyu alivamiwa usiku na watu wasiojulikana nyumbani kwake, huku chanzo rasmi
kikiwa bado hakijafahamika”, alisema Kamanda huyo.
Baadhi ya
wananchi waliokataa kutaja majina yake, walisema walisikia vurumai ndani ya
nyumba yake, ingwa hawakujua nini kinaendelea.
Walisema,
muda mfupi waliskia gari ikiondoka eneo la tukio na kutokomea sehemu
isiyojulikana na kumuacha mfanyabiashara huyo akiwa na majeraha makubwa.
Taarifa
kutoka hospitali ya Abdalla Mzee, zinaeleza kuwa baada ya kupokelewa kwa
mjeruhi kisha alihamishia hospitali nyingine kwa matibabu zaidi..
Mwisho
Comments
Post a Comment